Sajunne
Senior Member
- Jul 19, 2011
- 104
- 58
Ni miezi kadhaa imepita toka niachane na huyo msichana, nilimpenda sana lakini yeye hakuonyesha ushirikiano juu ya pendo langu kwake, kwani alifanya chocho alichojisikia akijua kuwa sita kuja kumwacha. Hakupenda kuongea na mimi kwenye cm wakati wa usiku na mchana pia wakati mwingine, ila mpaka ajisikie yeye kuongea na mimi. Baada ya hayo yote na mengine mengi kunitendea yasiyo mazuri nilichukua hatua ya kuachana nae. Na nikawa siwasiliani nae tena, ila baada ya miezi kadhaa kupita tangu tuachane amekuwa akinipigia cm na kuniuliza maswali ya kejeli kuwa beach fulani iko wapi mean nina apointment na mtu sehem hiyo . Je jamaa, ndugu na marafiki nifanyeje ili nisiwasiliane nae tena! Kwani anazidi kunitonesha kidonda alicho nisababisha yeye mwenyewe? Bt hekima na mawazo ya busara yanahitajika katika kutoa ushauri.