habi alex
Member
- Dec 1, 2011
- 90
- 12
Waheshimiwa naomba kuuliza hivi: Hao mapacha watatu wana nguvu kiasi gani kiasi cha kuwatisha viongozi karibu wote, kuwafanya sehemu kubwa ya wabunge vibaraka wao, watendaji mbalimbali kuwatii na kuwatumikia?
Nadhani ni binadamu tu kama binadamu mwingine yoyote, tena waoga sana, ila kwa kuwa hamna hatua madhubuti za kuwashikisha adabu zimechukuliwa dhidi yao wataiyumbisha sana serikali hii ya swahiba wao wa zamani.
Kwa nini CCM, Rais, na wote wenye uwezo wa kutamka neno likatamkika wasitamke neno tu na Watanzania wapone na waachane na kadhia ya hao watu?
Au wewe mwenzangu una maoni gani kuhusu ujasiri wa hawa mapacha watatu?