Elections 2010 Hivi Dr Slaa alipitishwa lini na mkutano mkuu kugombea urais?

nakushukuru sana mzee anagalau wewe umeona kitu.... najua ukipenda sana hata chongo utaona kengeza, ni makosa makubwa sana kuruhusu vidosari vidogovidogo hata kama hakuna pingamizi ndani ya chama, lakini vinaweza kutumiwa na wapinzani wa chadema kwenye kampeni, kumbuka chama hiki kinazongwa na uzushi wa aina nyingi kama ukabila, sasa udini na tena mnataka kuongeza udikteta wa kamatikuu!!

jamani siasa zina mbinu nyingi..... bado sijaridhika na majibu, ina maana pamoja na chadema kushabikiwa sana hapa jamvini, hakuna mtu anayejua utaratibu wa kumteua mgombea uais ndani ya chama unasemaje? ni ajabu na kweli!!

bado nasubiri anayejua utaratibu ukoje anisaidie....
Utaratibu unaanzia kwenye kifungu hiki: 7.7.16(a) cha Katiba yao. Ambao tayari wameufanya.
 
Katiba ya CHADEMA kwenye vifungu hivi 7.7.10(c) na 7.7.13(a)
 
Hawa nao mkutano mkuu ulifanyika lini
  1. LIPUMBA
  2. MUTAGWAYA
Hawa mikutano ya kuwateua imefanyika. Sema tu tunafunikwa sana na mambo ya CCM kwa kuwa yanatangazwa sana. Mrema alipotoka kusakata rumba ndani ya mkutano mkuu wa CCM ndipo akaitisha ule wa TLP na Mgaihywa kuteuliwa.
 
naomba kipengele cha katiba ya chadema kinachohusika nifuatilie, manake mwaka 2005 niliona mbowe alipitshwa kwa utaratibu tofauti na wa mwaka huu uliompitisha dr slaa!!1
mbana na wabunge kupitia CCM wamepitishwa tofauti na wa 2005 (mambo yanabadilika) au mbona kikwete amepigiwa kura na giza
 
Utaratibu unaanzia kwenye kifungu hiki: 7.7.16(a) cha Katiba yao. Ambao tayari wameufanya.

Katiba ya CHADEMA kwenye vifungu hivi 7.7.10(c) na 7.7.13(a)

haya nimefuatilia nimeona kama ifuatavyo....

7.7.10 Kazi za Mkutano Mkuu wa Taifa ni:-
(a) .............
(b) ........
(c) Kuteua mgombea wa Uraisi na mgombea wenza wake kwa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na mgombea Urais wa Zanzibar.

7.7.13 Kazi za Baraza Kuu zitakuwa:-
(a) Kupendekeza wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuwasilisha mapendekezo yake katika
mkutano mkuu kwa uamuzi.

7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-
(a) Kufanya utafiti wa wagombea na wa Uraisi na Mgombea Mwenza na kuwasilisha
ripoti zake kwa Baraza kuu kwa ajili ya mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu.

sasa mnisaidie, hamuoni kuwa dr slaa hajateuliwa kwa mujibu wa katiba ya chadema toleo la 2006? hamuoni kuwa kamati kuu imejivika mamlaka ya mkutano mkuu kuteua mgombea urais kinyume cha katiba ya chama? sasa akitokea mwanachama wa chadema akaweka pingamizi mtamuita msaliti?

wakuu naomba nisaidieni na hayo tafadhari

7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-
(a) Kufanya utafiti wa wagombea na wa Uraisi na Mgombea Mwenza na kuwasilisha
ripoti zake kwa Baraza kuu kwa ajili ya mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu.

Mapendekezo,siyo maidhinisho....in that case kamati kuu ina overide
 
Huenda kifungu namba 9.6 kimetumika? Tunamhitaji yule Mwanasheria wao kijana machachari Tundu Lissu atusaidie au Mnyika.
 
Utaratibu unaanzia kwenye kifungu hiki: 7.7.16(a) cha Katiba yao. Ambao tayari wameufanya.

soma ibara ya 7.7.9 ya katiba ya chadema kwani iko wazi; gonga hapa

hicho kifungu kinasema

7.7.9 Mkutano Mkuu Taifa utakutana mara moja katika kipindi cha miaka mitano. Mikutano
Mikuu maalum / dharura inaweza kuitishwa wakati wowote ikiwepo ulazima kwa
utaratibu utakaowekwa na Kanuni.

je kinatosha kuhalalisha kamati kuu kujitwalia mamlaka ya mkutano mkuu???
 
....

7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-
(a) Kufanya utafiti wa wagombea na wa Uraisi na Mgombea Mwenza na kuwasilisha
ripoti zake kwa Baraza kuu kwa ajili ya mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu.

sasa mnisaidie, hamuoni kuwa dr slaa hajateuliwa kwa mujibu wa katiba ya chadema toleo la 2006? hamuoni kuwa kamati kuu imejivika mamlaka ya mkutano mkuu kuteua mgombea urais kinyume cha katiba ya chama? sasa akitokea mwanachama wa chadema akaweka pingamizi mtamuita msaliti?

wakuu naomba nisaidieni na hayo tafadhari

[/FONT][/FONT]

Mkuu heshima mbele, CHADEMA ina weneyewe!

Kama unaulizia demokrasia ndani ya chama hiki, wengi wao hawapendi kufafanua vizuri. Nakumbuka tulijadili ana hapa mizengwe iliyofanyika wakati wa uchaguzi mkuu wa chadema mwaka juzi; hadi sasa najiuliza tutakuwa tunafanya mabadiliko gani kwa kuwabadilisha CCM na Chadema?
 
Utaratibu unaanzia kwenye kifungu hiki: 7.7.16(a) cha Katiba yao. Ambao tayari wameufanya.

Huenda kifungu namba 9.6 kimetumika? Tunamhitaji yule Mwanasheria wao kijana machachari Tundu Lissu atusaidie au Mnyika.

hichi kifungu kinasema;

9.6 Kukasimu Madaraka ya Shughuli za Utendaji
9.6.1 Kamati ya Utendaji ya Wilaya au Kamati Kuu Taifa zinaweza kukasimia baadhi ya
madaraka kwa sekretariat yake kwa azimio la wingi wa kura za wajumbe wa kikao.
9.6.2 Baraza Kuu linaweza kukasimia baadhi ya madaraka yake kwa Kamati Kuu kwa azimio
la uwingi wa kura za wajumbe wa .
9.6.3 Mkutano Mkuu unaweza kukasimu kwa Baraza Kuu baadhi ya madaraka yake, lakini kwa
azimio maalum.

sijaona mahali wanasema mkutano mkuu utakasimu madaraka kwa kamati kuu!! kama ulikasimu kwa baraza kuu, hilo baraza kuu lilikaa lini na azimio maalumu linalohusika linasomekaje?

nafikiri ni vizuri chadema wakafafanua hili manake nahisi pingamizi fulani linanukia...
 
Hili la CHADEMA kuwa na wenyewe siliafiki hata kidogo. Walifanya makosa kama haya kwenye ule uchaguzi mdogo wa Mbeya(V) kama sikosei. Tena mgombea wao alikuwa WAKILI mzoefu kabisa. Hatutaki wakosee kwa Dr Slaa wetu. Watatugharimu sana kama Taifa. Wanajua wasivyopendwa na watu kama Mtikila!
 
Mkuu heshima mbele, CHADEMA ina weneyewe!

Kama unaulizia demokrasia ndani ya chama hiki, wengi wao hawapendi kufafanua vizuri. Nakumbuka tulijadili ana hapa mizengwe iliyofanyika wakati wa uchaguzi mkuu wa chadema mwaka juzi; hadi sasa najiuliza tutakuwa tunafanya mabadiliko gani kwa kuwabadilisha CCM na Chadema?

kweli mkuu, hapa kuna dosari kubwa amabyo watu wazima kwa hiyari yao wameamua kuifumbia macho..... ni mfano mbaya kwa chama kinachotumainiwa na wananchi kama chadema.... achilia mbali lawama za kuanza kampeni kabla ya wakati!!!
 
nionavyo mimi, kicha ya nia njema waliyonayo, chadema wanafanya makosa wanayoona madogo lakini akipatikana mtu wa kuhoji ni makubwa sana.... wasisahau makosa ya wakati wa shitambala katika uchaguzi mdogo wa mbeya vijijini na jinsi yalivyowagharimu hadi kuondolewa kwenye uchaguzi.... siku zote ndege mjanja, hunaswa na tundu bovu....

nawasilisha...
 
Kuna kitu kinaitwa kukasimisha madaraka , mfano mkutano mkuu unaweza kukasimisha madaraka yake kwenye baraza kuu na baraza kuu linaweza kukasimisha madaraka yake kwenye Kamati kuu na kamati kuu inaweza kukaimisha madaraka yake kwa Secretariat ya kamati kuu.

Unapaswa kwanza kuuliza kama kuna jambo la kukasimisha madaraka na mamlaka lililofanyika kwenye mkutano mkuu uliopita na ikizingatiwa kuwa ulifanyika mwaka jana 2009 .

Ila mkutano mkuu utafanyika tarehe 12/08/2010, kwa ajili ya kupitisha ilani na ndio maana mpaka leo hujaweza kuiona ilani kwani mamlaka hayo hayakukasimishwa kwenye chombo kingine.

Kwa kifupi naweza kukupa maelezo hayo , na ni kweli kuwa Dr.Slaa sasa hivi yupo tume ya uchaguzi kwa ajili ya kuchukua fomu za tume, na kumbukeni kuwa anapaswa kutafuta wadhamini mikoa 10 na miwili lazima watoke Zanzibar.
 
Wewe kweli si mwenzetu hata hujui nani kapitisha Slaa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA? But YA "NGOSWE MUACHIE NGOSWE MWENYEWE".
 
Hata mimi mkuu limenisumbua kidogo kichwani nilipojaribu kufuatilia nikakutana na kibao kimeandikwa '' mambo ya ngoswe mwachie ngoswe mwenyewe'' sikuwa na ubishi maana hata hiyo katiba ya CHADEMA siijui, ila naamini wamefuata utaratibu unaokubalika ndiyo maana hatujasikia sauti za mavuvuzela kupinga uteuzi wake. ila umefanya vizuri kuuliza maana naona kale kaugonjwa ka kupenda bado kanasumbua watu:A S 39:
 
If you dont like mushrom soup, whay are you bothered with chumvi ilozidi? kwani wainywa wewe?
 
Back
Top Bottom