Hivi daktari ana thamani kuliko binadamu wengine???

Madakatari wa Tanzania kwani kulikuwa hakuna njia ingine ya kuigomea serikali iwasikiliza madai yao kuliko kutumia mbinu za kigaidi watu wasiokuwa na hatia wapoteze maisha ili maslahi yao yatimizwe.

Kisa wao ni watu wenye akili sana kuzidi wengine.
Hapo mie ndio pananikera. hawa jamaa wanajiona wao ni kama Miungu fulani hivi, hawajui udaktari ni kazi kama nyingine kama polisi, mwanajeshi, wahasibu, walimu nk. si waondoke tuu wenzao watakuja kupiga kazi. malalamiko kuhusu wao kusoma masomo magumu hiyo siyo tija walichagua wenyewe, kwa nini wasisomee accounts masomo rahisi ili nao wawe na mihela. mbona kozi ya kusomea hali ya hewa ni ngumu sana na hawalalamiki, ma engineer? achitekchas, wategua ,mabomu????
 
...Hivi unajua kuwa ''CHILISOSI inatoka kwenye CHILI NA SOSI'' vitu ambavyo ni ''HUWEKWA JUU YA CHIPS,NYAMA,etc'' ili kuongeza ladha wakati wa ''KUTAFUNA'',mi ningeomba watu wasipoteze muda kuongea na mtu ambaye ''ANATAFUNWA!!''

Madaktari wamegoma,kwanini msiweke hizo substitutes za ''WAALIMU'' waliowafundisha Madaktari badala ya kuendelea kupiga makelele!!??

Mnakubali kuwa Udaktari ni kazi kama kazi zingine,ila hamtaki kukubali kuwa na wao wana haki ya kuacha kazi mda na wakati wowote ule wanapoona maslahi hakuna kama ambavyo watu wa kazi zingine wanavyoweza kuacha kazi any time wakijiskia au kupata maslahi mazuri zaidi...!

Naomba mnijibu jamani, kwa nini hawa madaktari wantumia uhai wetu kuomba nyongeza ya mshahara
Kwani wao ni bora kukliko hawa wafuatao
POLISI
WANAJESHI
WALIMU Nk
Daktari alipwe shs 10,000,000 halafu mwalimu aliyemfundisha alipwe laki nne??
Halafu wanatumia kisingizio cha huduma bora kudai mihela.
Hebu nisaidieni mawazo yenu

Kuwa mkweli; Tanzania siyo nchi ya kijamaa tena, kwa hiyo kila kazi inalipwa kulingana na thamani yake. Iwapo unajua kuwa uhai wako unategema hao madakatari, basi walipe vizuri kwani kwa tamko hilo ni kukiri kuwa taaluma yao ni ya muhimu. Iwapo unaamni taaluma ya daktari siyo ya muhimu, na hivyo uhai wako hauhitaji taaluma yao basi usillamike wanapogoma. Hebu fikiria tena iwapo wabunge watagoma hata kwa mwaka mzima, je utaathirika vipi?
 
Watatu watatu kwenye vitanda, wamelala mpaka chini, kuambukizana magonjwa nje nje. Sasa hapo kama wewe ni daktari na ofisi yako ndo hiyo day in day out, si unakuwa katika risk kubwa ya wewe mwenyewe kuambukizwa maradhi na kuyapeleka majumbani kwao? Au wao wana kinga fulani kutoka mbinguni hatuijui.........Ahhhhh gomeni tu hayo mazingira ya kazi siyo kabisa....

Tusiwe mambumbumbu kwa hali hii (jumlisha na mziki wa shule yao ya miaka umri wa mtoto kuzaliwa hadi kufika darasa la pili), risk allowance haki yao, sindano za kinga haki yao, posho ya mazingira magumu haki yao, ongezeko la mshahara haki yao, tena hata hayo madai ya maboresho ya huduma ya afya wala msingepigia kelele, mngetuacha wavunja miwa wenyewe tupigike mpaka tutakapoona haja ya kuiwajibisha serikali dhaifu!!

Halafu baadhi ya hawa hawa kinamama wakipewa kanga, ubwabwa na 5000 wanasahau shida zote hizi kweli maskini mpe pombe asahau shida kwa muda
 
Yote nayakubali lakini kama kweli wana huruma basi wasiombe mshahara wa kutisha ili hizo hela zitumike kuboresha afya

Na ikulu isitenge kila siku 1000000/= kwa chai kumbuka twaweza pata vitanda viwili hospitalini au madawati 3
 
Naomba mnijibu jamani, kwa nini hawa madaktari wantumia uhai wetu kuomba nyongeza ya mshahara
Kwani wao ni bora kukliko hawa wafuatao
POLISI
WANAJESHI
WALIMU Nk
Daktari alipwe shs 10,000,000 halafu mwalimu aliyemfundisha alipwe laki nne??
Halafu wanatumia kisingizio cha huduma bora kudai mihela.
Hebu nisaidieni mawazo yenu

Daktari si bora kuliko wengine, ila tatizo serikali ya CCM haikutoa hilo somo kwa madaktari mapema likaeleweka. Muda mrefu serikali ya CCM imekuwa party na wamekua mfano mbaya kwa Madaktari na raia wengine - labda tusubiri hang-over ya Serikali ya CCM iishe.
 
Back
Top Bottom