Hivi CUF itasimamisha Mgombea Urais Zanzibar 2015?

Maishamapya

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,279
375
Nimekuwa nifuatilia sana mijadala ya baadhi ya wanaJF kuhusu hatima ya Chadema na upinzani kwa ujumla. Wako ambao wamekuwa wakiona kuwa CDM itaanguka na hasa baada ya kukataa kuwashirikisha Cuf na vyama vingine.

Kwa kutafakari yote haya imebidi nijiulize: Hivi sasa hivi Znz kuna kambi ya upinzani? Si cuf ni sehemu ya serikali ya sasa? Watawezaje kuinyooshea kidole CCM juu ya mapooza yake wakati wao pia ni sehemu ya serikali hiyo? Hivi mwaka 2015, Cuf watasimamisha mgombea huko visiwani? Je, atakuwa mgombea wa cuf au ...? Ni lipi jipya ambalo mgomea wa cuf atawaambia wanzanzibari kuwa atalifanya ambalo serikali aliyoshiriki haikulifanya? Je, atathubutu kusema ni kwa vile haikuwa cuf?

Nionavyo mimi Cuf si chama cha upinzani kwa sasa bali ni sehemu ya utawala wa CCM. Tunachosubiri sasa ni kuona muunganiko wa sera za vyama hivi viwili. Na ninapata shida sana kufikiri namna gani wanaweza kusimamisha mgombea 2015. Chama pekee cha upinzani kilichobaki Tanzania ni CHADEMA.

Nipeni hoja zenu wanaJF
 
'Aaah, mmmh! Tutasimamisha mgombea wetu makini, tutasema wenzetu walituburuza na hawakutaka kusikiliza mipango yetu. Sawa sawa!?
Pili tulipokuwa ndani ya serikali tumegundua uzembe mwingi mno, Sawa sawa?
Tupeni nafasi ya kuwa juu yao tuwaonyesheni kazi, ila mkipenda warudisheni hao hao, twatawala wote na..........
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom