Hivi Chadema ni WATAKATIFU..?

leroy

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
1,589
2,140
  • Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa siasa za Tanzania katika miaka ya hivi karibuni.
  • Nakubali kabisa kuwa hali ya siasa ilivyo hivi sasa imechangiwa na mapungufu ya serikali ya chama tawala, ccm.
  • Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kwa nini mtu ukibainisha mapungufu ya chama cha CHADEMA unaonekana mbaya na kuishia kushambuliwa kwa matusi na lugha za kejeli. Hii ni matokeo ya ukereketwa ama nini...
  • Je, ubaya upo ccm pekee? Chadema ni watakatifu? siasa hizi za kuangalia kibanzi kilichopo kwenye jicho la mwenzio na kusahau boriti lililopo jichoni mwako itatufikisha popote?
  • Mi naamini kila taasisi ina mapungufu yake, kwa hiyo utamaduni wa kukosoa ulioibuka hivi sasa miongoni mwa watanzania nashauri ulenge pande zote la sivyo tutakuwa hatutendi haki.
  • Kukosolewa ni sehemu muhimu ili uweze kusonga mbele......

nawasilisha.
 
Kuna kutaja mapungufu lakini pia kuna kupiga propaganda.
 
Ukisikia kelele inatoka katikati ya watu mahali paliporushiwa jiwe ujue limempata huyo anayepiga kelele. Wape watu uhuru watende waonacho ni halali ikiwa hawakuvunja sheria.
 
Unajua maana ya mtakatifu kweli embu rudi kwenye vitabu halafu uje tena.Tena unazungumzia hawa binadamu wa kizazi kilichopo mhh
 
Hakuna mkamilifu,na naamini CDM pia wanatambua kuwa wao sio miungu,ni watu waelewa na wana upeo mzuri tu,wanajua kutofautisha mpunga na magugu na naamini ni kutokana na umakini huo ndo wameweza kufika walipo leo,hivyo ni lazima wanakubali "CONSTRUCTIVE CRITICISM" na sio kejeli,kebehi na derogatory propaganda kwa malengo ya watu flani!
 
Maswali yaleyale, yanaulizwa na watu walewale. Leta maswali ya msingi, sio eti "kwanini Mbowe analipia mtoto mil 15".
 
Hakuna mkamilifu,na naamini CDM pia wanatambua kuwa wao sio miungu,ni watu waelewa na wana upeo mzuri tu,wanajua kutofautisha mpunga na magugu na naamini ni kutokana na umakini huo ndo wameweza kufika walipo leo,hivyo ni lazima wanakubali "CONSTRUCTIVE CRITICISM" na sio kejeli,kebehi na derogatory propaganda kwa malengo ya watu flani!

Umesema vema. Thanks!
 
Tatizo CCM hawataki kutubu. Dhambi (Gamba) limeng'ang'ania.

Rom 3:23 For all have sinned. This has been already shown.
And come short of the glory of God. Wycliffe says, Have need of the glory of God. I believe this suggests the idea. Man was made originally in the image of God. He was then sinless. No sinner is in the Divine image. All have sinned, and to have the divine likeness restored, need to have their sins blotted out. Until this is done they come short of the glory of God.
 
  • Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa siasa za Tanzania katika miaka ya hivi karibuni.
  • Nakubali kabisa kuwa hali ya siasa ilivyo hivi sasa imechangiwa na mapungufu ya serikali ya chama tawala, ccm.
  • Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kwa nini mtu ukibainisha mapungufu ya chama cha CHADEMA unaonekana mbaya na kuishia kushambuliwa kwa matusi na lugha za kejeli. Hii ni matokeo ya ukereketwa ama nini...
  • Je, ubaya upo ccm pekee? Chadema ni watakatifu? siasa hizi za kuangalia kibanzi kilichopo kwenye jicho la mwenzio na kusahau boriti lililopo jichoni mwako itatufikisha popote?
  • Mi naamini kila taasisi ina mapungufu yake, kwa hiyo utamaduni wa kukosoa ulioibuka hivi sasa miongoni mwa watanzania nashauri ulenge pande zote la sivyo tutakuwa hatutendi haki.
  • Kukosolewa ni sehemu muhimu ili uweze kusonga mbele......

nawasilisha.

Nimefurahishwa na bango lako la wino wa kijani ni rangi ya CCM
 
Unajua maana ya mtakatifu kweli embu rudi kwenye vitabu halafu uje tena.Tena unazungumzia hawa binadamu wa kizazi kilichopo mhh

well said,

kufuru kubwa kusema chadema ni watakatifu kwani kimekuwa ni chama cha kidini? hadi unatumia neno watakatifu?
 
  • Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa siasa za Tanzania katika miaka ya hivi karibuni.
  • Nakubali kabisa kuwa hali ya siasa ilivyo hivi sasa imechangiwa na mapungufu ya serikali ya chama tawala, ccm.
  • Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kwa nini mtu ukibainisha mapungufu ya chama cha CHADEMA unaonekana mbaya na kuishia kushambuliwa kwa matusi na lugha za kejeli. Hii ni matokeo ya ukereketwa ama nini...
  • Je, ubaya upo ccm pekee? Chadema ni watakatifu? siasa hizi za kuangalia kibanzi kilichopo kwenye jicho la mwenzio na kusahau boriti lililopo jichoni mwako itatufikisha popote?
  • Mi naamini kila taasisi ina mapungufu yake, kwa hiyo utamaduni wa kukosoa ulioibuka hivi sasa miongoni mwa watanzania nashauri ulenge pande zote la sivyo tutakuwa hatutendi haki.
  • Kukosolewa ni sehemu muhimu ili uweze kusonga mbele......

nawasilisha.

Natafuta mchumba awe na sifa na mahaba ya kimagamba.
 
dereva mzuri au mbaya ni yule anayeendesha chombo.
ccm ni wabaya kwa sababu wanakusanya tril 8 na matumizi yao ni 10 tri hizo 2 nani analipa?

chadema wanaweza kuwa wazuri au wabaya ila huwezi kuwahukumu kwa vile aliyeko madarakani kashindwa na kuasume kuwa na wao watashindwa.
 
CHADEMA si watakatifu ila wana uhusiano wa karibu na baba mtakatifu wa VATICAN! Unganisha dots mwenyewe!
 
  • Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa siasa za Tanzania katika miaka ya hivi karibuni.
  • Nakubali kabisa kuwa hali ya siasa ilivyo hivi sasa imechangiwa na mapungufu ya serikali ya chama tawala, ccm.
  • Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kwa nini mtu ukibainisha mapungufu ya chama cha CHADEMA unaonekana mbaya na kuishia kushambuliwa kwa matusi na lugha za kejeli. Hii ni matokeo ya ukereketwa ama nini...
  • Je, ubaya upo ccm pekee? Chadema ni watakatifu? siasa hizi za kuangalia kibanzi kilichopo kwenye jicho la mwenzio na kusahau boriti lililopo jichoni mwako itatufikisha popote?
  • Mi naamini kila taasisi ina mapungufu yake, kwa hiyo utamaduni wa kukosoa ulioibuka hivi sasa miongoni mwa watanzania nashauri ulenge pande zote la sivyo tutakuwa hatutendi haki.
  • Kukosolewa ni sehemu muhimu ili uweze kusonga mbele......

nawasilisha.

wewe jamaangu utakuwa una matatizo ccm imeshachokwa miaka 50 inatosha tumevumilia vya kutosha...ukitukanwa ujue unataka kutumia mapungufu kidogo tena yasiyo ya msingi kuhalalisha CCM ni safi...sasa nakushauri ukitaka usitukanwe na kushambuliwa na jamii jikite zaidi kwenye ushauri na siyo umbea wa kutaka kuonesha cdm wana makosa na wao pia hawafai kuongoza..tumechoka sana yaani ccm hata marafiki wenye mrengo wa ccm sasa nimewapunguza...tunahitaji damu mpya hata kama haitakuwa na mabadiliko makubwa ili kufungue njia ya mabadiliko kwanza
 
Back
Top Bottom