Elections 2010 Hivi CHADEMA haina wataalamu, au viongozi wake ndiyo wasioambilika?

Mkuu MF
Kama umeshindwa kuisoma yote, nini sababu ya msingi ya kukoti jamvi lote hilo? Si ungeandika tu kwamba umeshindwa kusoma? Kajamvi haka kanakutia uvivu wa kusoma? Vipi umeshamaliza kusoma sera na ilani ya Chadema?
Alafu mbali na kumaliza kusoma ilani nimeirudia mara nyingi tu. Hii imeandikwa kama ya sisi m vile, nimeshindwa kuisoma vizuri ingawa naendelea kuisoma kwa shida. Sijui aliiandika Makamba?
 
Mwenye uvumilivu wa kuusoma mpaka mwisho huo upupu na kukubaliana nao, ampigie kura Kikwete. Sisi tulio na kiu ya maendeleo tutampigia kura Dr. Slaa.
Ule umakini wenu umeishia wapi? Kweli mnaweza ama mnaota tu?
 
Alafu mbali na kumaliza kusoma ilani nimeirudia mara nyingi tu. Hii imeandikwa kama ya sisi m vile, nimeshindwa kuisoma vizuri ingawa naendelea kuisoma kwa shida. Sijui aliiandika Makamba?
Inaonekana Makamba anawakosesha wengi usingizi...!
 
Daboman punguza hasira, Unakuwa na hasira hadi unasahau kuweka paragraph duh pole
 
This discussion reminds me of a guy who said "Iliposemwa Yesu akirudi kila jicho litamuona some hundreds years ago ilionekana ni impossible, but wait - What if it will be thru TV??'' Can someone imagine how a TV of 2095 will b?
 
sorry, your thread is very short i think u didnt have enough time to prepare the long one. tehe tehe tehe tehe,,,,,,
 
This discussion reminds me of a guy who said "Iliposemwa Yesu akirudi kila jicho litamuona some hundreds years ago ilionekana ni impossible, but wait - What if it will be thru TV??'' Can someone imagine how a TV of 2095 will b?

Nyambala, kwa hiyo matumaini ya Dr Slaa kushika usukani ni sawa na yale ya Yesu kurudi? Kama ndio hivyo basi nitakufa kabla yake, mana mamia ya miaka imepita tangu tuambiwe kwamba Yesu atarudi!!!
 
May be slaa he can....! na treni yake ya angani
Mkuu Kibunango, kwa sasa unajishushia hadhi kwani unajibu kihuni. Najua unaumia rohoni na Dr. Slaa anakunyima usingizi lakini hebu punguza munkari kidogo. Kama hukuwa moja wapo wa waliolitafuna taifa hili bila huruma, huna cha kuogopa - bado wiki tatu tu, historia iandikkwe upya.
 
Nyambala, kwa hiyo matumaini ya Dr Slaa kushika usukani ni sawa na yale ya Yesu kurudi? Kama ndio hivyo basi nitakufa kabla yake, mana mamia ya miaka imepita tangu tuambiwe kwamba Yesu atarudi!!!

Shape both ur head and ur ass up!
 
Mkuu Kibunango, kwa sasa unajishushia hadhi kwani unajibu kihuni. Najua unaumia rohoni na Dr. Slaa anakunyima usingizi lakini hebu punguza munkari kidogo. Kama hukuwa moja wapo wa waliolitafuna taifa hili bila huruma, huna cha kuogopa - bado wiki tatu tu, historia iandikkwe upya.

huyo toka kitambo hana hadhi. Kule kwa wakubwa kumemtibua akili. Alikuwa kapten kule
 
Hivi sasa tunaishi katika kipindi ambacho wataalamu na wanahistoria ya maendeleo ya kitekinolojia katika ulimwengu wanakiita 'information age', yaani kipindi cha 'habari na mawasiliano'. Kwa mujibu wa wataalamu na wanahistoria hawa, kipindi hiki kimeanza mwanzoni mwa miaka ya 1990, na kuchukua nafasi ya kipindi kilichotangulia ambacho wenyewe walikiita 'industrial age', yaani kipindi cha 'mapinduzi ya viwanda'.
Tofauti na huko nyuma, hiki ni kipindi ambacho taarifa na habari zinatembea kwa kasi kubwa sana na kuwafikia watu wengi zaidi kuliko muda mwingine wowote ule katika historia ya mwanaadamu. Aidha ni kipindi ambacho taarifa na habari mpya zinazoingia na kusambaa ulimwenguni kila siku ni nyingi mno, kiasi kwamba mtu anayetaka kwenda sambamba na wakati, analazimika awe ni mwanafunzi wa kudumu.
Wataalamu wa tekinolojia ya habari na mawasiliano wanakisia kuwa kila baada ya miezi kumi na nane habari zinazohusu nyanja mbalimbali zinazoingia na kusambaa ulimwenguni zinaongezeka mara dufu!
Maendeleo katika tekinolojia ya computer yaliyopelekea kuvumbuliwa kwa computer ndogo za mezani na mapajani; uvumbuzi wa mtandao wa kidunia wa internet (world wide web) unaowawezesha wamiliki wa computer duniani kote kujiunga na kisha kupokea, kutuma, kubadilishana, na kupashana habari; na ujio wa mawasiliano ya simu za kiganjani, kwa pamoja ndiyo yaliyozaa kipindi hiki.
Kipindi hiki kimezaa mabadiliko makubwa sana katika nyanja zote za maisha. Mifano ni mingi sana inayoweza kutumika kulidhihirisha hili.
Hebu tutazame mifano michache: Kiasili, serikali ni taasisi ambayo ina umbile la piramidi. Juu zaidi kuna raisi, au waziri mkuu, au mfalme, nakadhalika. Chini ya huyu kunaweza kuwa na makamu wa raisi na waziri mkuu, ambao chini yao nao kuna baraza la mawaziri. Mtiririko huu unakwenda mpaka tunampata mtendaji wa mtaa au kijiji, nakadhalika.
Katika umbile la namna hii tunapata kitu kinachoitwa URASIMU. Jambo zito na lenye uwezekano wa kutikisa Taifa zima linaweza kutokea katika ngazi ya kijiji, lakini hadi raisi apate taarifa za jambo hilo, inaweza kuchukua muda mrefu na pengine asipate taarifa hizo kabisa. Kinachotokea ni kwamba mmoja au baadhi ya viongozi walioko kwenye ngazi za kati, kwa ajili tu ya kulinda maslahi yao, au kwa hofu wanaamua kuacha kuendelea kutoa taarifa katika ngazi zinazofuatia juu yao.
Hapa nchini miaka ya nyuma kuna maeneo yalikuwa yanakumbwa na njaa hadi baadhi ya Wananchi wanapoteza maisha yao, lakini viongozi wa juu wa serikali wanaishia kupata taarifa hizo kupitia vyombo vya habari. Hali hii ilijitokeza kwa sababu tu viongozi wa ngazi za chini au waliogopa kutoa taarifa, au kuna ambao katika mnyororo huo wa kupeana taarifa walizembea; na mawasiliano na ngazi za juu yakakatika.
Katika kipindi hiki cha habari na mawasiliano, urasimu wa namna hii unapaswa kuwa historia tu. Pamoja na kwamba umbo la serikali linabaki ni lile lile la piramidi, lakini iwapo kila ofisi ya serikali kuanzia juu hadi chini imeunganishwa kimawasiliano na mtandao wa internet, upashanaji wa habari unabadilika na kuchukua umbo kama la uso wa maji.
Ukidondosha kijiwe katikati ya uso wa maji yaliyotuama, mawimbi yanasafiri kutoka hapo kijiwe kilipodondokea na kuelekea pande zote juu ya uso huo wa maji, tena kwa wakati huo huo. Kama ilivyo kwa mawimbi katika uso wa maji, barua pepe moja iliyoanzia kwa mtendaji wa kijiji kimoja, mathalani kule Rukwa, inaweza kumfikia katibu tarafa, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, waziri mkuu, na raisi kwa wakati huo huo mmoja. Hii ina maana kwamba kama serikali haikuchukua hatua zinazotakiwa kwa wakati muafaka, tatizo halitakuwa tena ni la urasimu katika kupeana taarifa, ila litakuwa ni kutokana na sababu nyingine, kama uzembe, nakadhalika.
Hebu sasa tuangalie ulimwengu wa kibiashara. Kwa wafanyabiashara walioridhia kuwekeza muda na kujifunza, kipindi hiki cha habari na mawasiliano ni kipindi ambacho kimezaa fursa zisizo na kifani.
Kwa mfano: Kama una bidhaa unauza, na hujui soko liko wapi, unachotakiwa kufanya ni kujisajili tu katika moja ya masoko makubwa ya kwenye mtandao, mathalani Alibaba.com, na kuorodhesha bidhaa ulizonazo nazo. Kwa uhakika kabisa, kabla ya masaa ishirini na nne kupita, utaletewa orodha ndefu ya wafanyabiashara duniani kote na anuani zao, ambao wanatafuta bidhaa unazouza.
Au mathalani, umebuni mradi mzuri lakini kikwazo chako ni mtaji. Kuna mitandao kadhaa ya wawekezaji ambayo ukishajisajili – kuna gharama kidogo unalipia – unaruhusiwa kuwasilisha muhtasari wa business plan yako, yaani muhtasari wa andiko la mradi wako. Wanachama wa mtandao husika watapata fursa ya kupitia muhtasari huo, na wale watakaovutiwa watawasiliana na wasimamizi wa mtandao, ambao nao watakupatia orodha na anuani za wawekezaji hao ili muweze kuwasiliana na kujadiliana. Mwisho wa yote wawekezaji hao watataka walione andiko lote la mradi wako, na kama umeandika kitu cha uhakika, usishangae kukuta unapata watu kutoka Ulaya, Australia, India, Marekani nakadhalika; ambao wako tayari kutoa fedha zao wawekeze kwenye mradi wako kabla hata hamjaonana uso kwa uso!
Hali iko hivyo hivyo kwa wanaotafuta elimu mbalimbali, mafundi wanaokarabati mashine mbalimbali, madaktari wanaohangaika na magonjwa yanayotatiza, watafiti katika fani mbalimbali, nakadhalika.
Kwa mfano: Mwanafunzi anayesomea shahada ya uzamifu hapa kwetu Tanzania anaweza akapata tabu sana kufanya utafiti wa maandiko (literature search) juu ya fani husika, iwapo tegemeo lake pekee ni hizi maktaba zetu. Hii inatokana na ukweli kwamba maktaba zetu zina upungufu mkubwa wa vitabu na majarida ya kitaaluma, kutokana na gharama kubwa ya kuagizia vitu hivyo. Hata hivyo tatizo la mwanafunzi huyu linaweza likamalizika ndani ya muda mfupi sana kwa kutumia mtandao. Kuna maktaba nyingi katika mtandao zilizosheheni kila aina ya vitabu na majarida ya kitaalamu; unachotakiwa tu ni kujisajili na kufumba na kufumbua, nyaraka katika fani unayotafiti zitakuwa mbele yako kwa mamilioni.
Uzuri wa kipindi hiki ni kwamba siyo rahisi tena kudanganya na kuzuia habari kama ilivyokuwa siku za nyuma. Habari inaweza kutokea katika jiji la Mbeya leo asubuhi, na kwa ajili maslahi fulani fulani, ikamuuliwa kwamba taarifa zile zisifikishwe kwa Wananchi kupitia vyombo vya habari vya kawaida yaani Radio, TV na magazeti. Wakati miaka kumi iliyopita uamuzi huu ungekuwa ni wa busara kwa hao wenye kuutoa, leo hii utakuwa ni uamuzi wa kuchekesha. Utaachaje kuwa ni uamuzi wa kuchekesha wakati huenda hata kabla ya kikao kinachotarajiwa kutoa maamuzi ya kuzuia habari husika isitangazwe kuketi, habari hiyo itakuwa tayari imeshasambaa nchi nzima kwa njia ya SMS na barua pepe?
Hivi sasa tuko katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31, 2010. Wagombea mbalimbali wa nafasi za udiwani, ubunge na uraisi wameendelea na kujinadi, na katika kujinadi kwao tumesikia mengi. Uzuri wa kipindi hiki cha habari na mawasiliano ni kwamba, ni rahisi kujua yapi kati ya yanayonadiwa na wagombea yanawezekana; na yapi hayawezekani.
Naomba nisieleweke vibaya. Kila kinachonadiwa kinawezekana, lakini kuwezekana kwenyewe kunategemea na mazingira ya eneo husika na wakati unaohusika. Kuna mambo mengi ambayo yanawezekana Ulaya, Marekani, Japan, na katika nchi nyingine zilizoendelea lakini hayawezekani katika mazingira ya Tanzania ya leo. Kwa mfano mgombea akijinadi kuwa mkimchagua ataweka treni ya chini ya ardhi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, moja kwa moja unajua kuwa kwa mazingira ya Tanzania ya sasa mgombea huyu ana walakini. Lakini ahadi hiyo hiyo ikitolewa na mgombea aliyeko Ujerumani, Kanada, au nchi nyingine yoyote iliyoendelea, wala watu wa huko hawatapoteza muda wao kujadili; kwa mazingira ya kwao hilo ni jambo la kawaida kabisa; linawezekana.
Miongoni mwa wagombea uraisi ambao wamekuwa wakitoa ahadi ambazo kwa mtizamo wangu zina walakini mkubwa, ni Dr. Slaa wa CHADEMA. Miongoni mwa ahadi hizo ni ile ya kuweka treni ya masaa matatu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam, na ile ya kushusha bei ya saruji hadi shilingi 5,000.00 kwa mfuko wa saruji wa kilo 50.
Tuanze kwanza kuangalia hii ahadi ya treni. Umbali kutokaMwanza hadi Dar es Salaam ni kilometa 1,229. Ili kuwa na treni ya kuweza kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa masaa matatu, itailazimu treni hiyo iwe na mwendo kasi wa kilometa 410 kwa saa moja! Hivi sasa treni inayoshikilia rekodi kwa mwendo wa kasi ni ile ya Maglev inayofanya safari zake kati majiji ya Shanghai na Beijing, kule China. Treni hii ina mwendo kasi wa kilometa 431 kwa saa. Treni nyingine maarufu duniani kwa mwendo kasi ni Shinkasen ya Japan, kilometa 260 kwa saa na Eurostar ya Ulaya, kilometa 250 kwa saa!
Katika Tanzania ya leo ahadi ya Dr. Slaa ni kiini macho kwa sababu nchi hii kwa sasa hata uwezo wa kuwapatia Wananchi wake wote milo mitatu kwa siku haina; achilia mbali ukweli kwamba zaidi ya asilimia 40 ya bajeti ya nchi inategemea zaidi wahisani. Sasa kama hao wanaotufadhili wenyewe bado treni hiyo ya mwendo kasi wa kilometa 410 kwa saa hawajawa nayo, sisi tunategemea treni hiyo tuitoe wapi?
Tukija kwenye ahadi ya kuuza mfuko wa saruji kwa shilingi 5,000/- tu, hapa napo inabidi tujiulize: Hivi CHADEMA haina wataalamu wa uchumi, au mgombea wao ndiye asiyeambilika? Katika uzalishaji wa saruji, kuna malighafi muhimu inayoitwa CLINKER. Hivi sasa Tanzania ina uwezo mdogo sana wa kutengeneza malighafi hii; na viwanda vyote vya saruji nchini inabidi kuiagiza kutoka nje ya nchi.
Nchi maarufu kwa uzalishaji na ambayo inaiuza malighafi hii kwa bei rahisi kuliko nchi zote ni China. Katika masoko ya China, kilo 50 ya Clinker inauzwa kiasi cha shilingi 3,902/- kwa sasa. Hii ina maana kuwa pamoja na gharama za usafirishaji hadi katika bandari ya Dar es Salaam, gharama za kuipakua, kuihifadhi, kuitoa, na hatimaye kuisafirisha hadi kiwandani, malighafi hiyo inaweza kufikia gharama ya shilingi 4,500/-; bila hata kulipiwa ushuru wa forodha.
Malighafi hii ikishafika kiwandani inatakiwa sasa ichanganywe na malighafi nyingine zinazopatikana nchini, mathalani 5% - 8% jasi (gypsum), kabla ya kutiwa kwenye mtambo wa kusagia ili kupata saruji yenye ulaini unaotakiwa. Iwapo kilo 50 ya malighafi hizi inafikia shilingi 500/- tu kwa mfano, hii ina maana kuwa hata kabla ya kuinjikwa kwenye mtambo wa kusagia, tayari saruji ghafi yetu imeshatugharimu shingi 5,000/-.
Katika gharama hii ongezea gharama ya nishati inayotumiwa katika mtambo, gharama za kuiweka saruji iliyo tayari kwenye vifungio, gharama za upakiaji na usafirishaji hadi kwa mawakala, na gharama za utawala; ambazo kwa mfano tu, tuseme ni shilingi 500/-. Sasa hata kabla kiwanda hakijaweka faida yake na kulipa kodi yoyote ile ya serikali, tunaona kuwa tayari gharama ya mfuko mmoja ishafika shilingi 5,500/-. Ukiweka faida ya kiwanda ambayo ni asilimia kati ya 7 na 9, utagundua kuwa mfuko mmoja wa saruji kwa mahesabu ya chini kabisa ambayo hayajumuishi kodi yoyote ya serikali ni shilingi 5,940/- kwa bei ya kiwanda. Ongeza na bei ya mawakala wasambazaji wa kiwanda na wauzaji wa jumla na rejareja, utagundua kuwa hata bila kulipiwa kodi yoyote ile, haiwezekani saruji ikauzwa chini shilingi 6,500/- kwa mfuko wa kilo hamsini.
Njia pekee ambayo Dr. Slaa ataweza kutuuzia mfuko wa saruji kwa shilingi 5,000/- ni iwapo tu serikali yake itakuwa inatoa ruzuku kwa wazalishaji wa saruji. Swali linakuja:Ruzuku hiyo itatoka wapi?
Narudia tena: Hiki ni kipindi cha habari na mawasiliano. Ni kipindi kigumu sana kudanganya, na hasa lengo linapokuwa ni kuudanganya umma. Inawezekana CHADEMA haikuwa na nia ya kutudanganya, lakini wanawezaje wakajitetea kuwa wamekuja na ahadi nzito kiasi hicho bila kufanya utafiti? Tangu kampeni hizi zimeanza chama hiki kimefanya makosa mengi mno ya kiufundi na ya wazi, kiasi kwamba mtu unabaki ukiwa umepigwa na bumbuwazi. Ni vipi chama kichanga kiasi hicho kiwe na matumaini ya kupewa ridhaa ya kuongoza nchi? Ushauri wangu kwa CHADEMA ni kwamba viongozi na wagombea wake wawe wanatoa ahadi baada ya kuzifanyia kazi; vinginevo watagundua kuwa Watanzania wanaowadhania ni wajinga, kumbe ni wajanja kuliko wao.

Maneno mengi sana. Ungeandika paras nne tu badala ya kutuwekea background ya ICTs. Mimi nilifikiri ambayo yangefuata yangeendana na ICTs kumbe hamna!!!

Jaribu kulinganisha ahadi za wagombea wote wa Urais.

Wewe ni sababu mojawapo ya Tanzania kuwa maskini!!!!!!!
 
Unaweza kuwa ni miongoni mwa walimbukeni wengi huko chadema kwa kutetea upupu huu pasipo udhibitisho rasmi. Umbali toka Dsm mpaka Mza kwa treni ni km 1260 hivi. Tena kumbuka vizuri ni kwa treni! Kwa barabara umbali huo unaweza kupungua kwa asilimia kadhaa, na kwa usafiri wa anga unapungua kwa asilimia kubwa.

Ukipima umbali huo moja kwa moja toka kwenye ramani, utapata kilometa 850.20 hivi. Na sijawahi kuona reli iliyoonyoka toka pointi A hadi B kama ambavyo wewe unavyotaka kutuambia hapa!

Reli ya kati imepita katika mikoa zaidi ya minne(Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, na Mwanza), sasa wewe na slaa wako mnataka kutuambia kuwa mtajenga reli mpya bila kupita katika mikoa hiyo? Mtaipitisha angani nini? Je wananchi wa mikoa iliyobaki wasahau huduma hiyo muhimu kwao kwa usafiri?

Treni ya sasa yenye kutumia diseli inakwenda kilomita 65 kwa saa, na ina vituo vingi, ndio maana inachukua karibu masaa 39 kufika Mwanza ilhali ndege yenye kutumia injini za jet inachukuwa sio zaidi ya saa moja. Usafiri kwa barabara sasa upunguza umbali, kwani asilimia 90 ya barabara hiyo ipo katika kiwango cha lami, hivyo kuruhusu magari madogo kusafiri zaidi ya kilomita 100 kwa saa, mabasi kilomita 80 kwa saa (ingawa madereva wengi wa mabasi hayo uendesha km 100-120 kwa saa) na malori ya mizigo km 80 kwa saa.


Nafikiri tatizo ni katika vision. Tatizo kubwa la CCM hawajawahi kuwa na Vision ya Tanzania kama nchi kujiendeleza Kisayansi (Shule za kata) na hawana mpango wa kushindana na taifa lolote duniani (hata shirika la ndege hatuna). Hivyo basi, sisi katika CHADEMA tunaamini katika ushindani wa kisayansi na uwezo wa kuwa na treni yenye kasi hiyo ya 410 km/hr.

Nani kakwambia lengo la treni ya Slaa (PhD) ni kuwa kumbakumba na hivyo kulazimika kupitia Dodoma na nani kakwambia hatuwezi kuwa na reli ambayo ni almost straight line (Approx. 900 km). Hata ahadi ya masaa mawili na nusu ni feasible. Mwandishi anakili technolojia ya speed 410 km/hr siyo ndoto (Ipo China)...Sasa hapo kuna geni chini ya Jua?
 
Maneno mengi sana. Ungeandika paras nne tu badala ya kutuwekea background ya ICTs. Mimi nilifikiri ambayo yangefuata yangeendana na ICTs kumbe hamna!!!

Jaribu kulinganisha ahadi za wagombea wote wa Urais.

Wewe ni sababu mojawapo ya Tanzania kuwa maskini!!!!!!!

Huyo huenda akawa ni sababu mojawapo ya Tanzania kuwa masikini lakini WEWE ni sababu kubwa ya Tanzania kuendelea kuwa masikini! :tonguez:
 
Nikisema nawe ni mhuni nitakuwa nimekosea? Soma mara mbili bandiko lako na utajua kwa nini nimediriki kukuita mhuni.
Kwa mujibu wa KAMUSI ya kiswahili sanifu neno mhuni maana yake ni mseja yaani mtu asiye na mke au mume, pili mtu asiye na makazi maalum, tatu mtu asiye na tabia nzuri na nne mtuasiye chungia wengine heshima
Neno kiherehere maana yake ni mpapatiko wa moyo au wahaka au wasiwasi au machugachuga
Machugachuga ni hali ya kutotulia mahali pamoja au wasiwasi au wahaka
wahaka ni hali ya wasiwasi na kupapatika kwa moyo, kiherehere,wasiwasi
Neno ***** maana yake ni mtu mjinga, mpumbavu, bozi au ****
Neno mahaba maana yake ni mapenzi
Neno MAGAZIJUTO (MA=mabano GA=gawanya ZI=zidisha JU=jumlisha TO=toa) hesabu za darasa la tatu enzi za elimu ya mwalimu

Nimetumia kiswahili sanifu katika kukutaka wewe mwana CCM na wana CHADEMA kutoa mchanganganuo wa kimahesabu wa ahadi za wagombea wenu DKT JK na DKT SLAA naomba nipe mchanganuo huo na si kukwepa hoja na kuniita mhuni, eti mimi ni CHADEMA.
MIMI nina mke hivyo mimi si mhuni, MIMI ninamakazi yangu ya kudumu hivyo sitegemei DKT SLAA ashushe bei ya cement na bati ndio nijenge hivyo mi si mhuni kwa tafsiri ya kiswahili sanifu, pia sijakuvunzia heshima wewe au wana CCM na wana CHADEMA au wagombea wenu hivyo tafsiri ya neno mhuni hainihusu, kwa hiyo mimi si mhuni.

Napenda kukuambia kuwa mwanachama wa chama chochote cha kisias ambacho kimesajiliwa kisheria si kosa la jinai, hivyo siwezi kuona aibu kuwa mwanachama wa chama chochote kama mimi ni mwanachama. Hivyo kuwa CUF,CCM,CHADEMA,NRA.NLD,UPDP,APPT nk sio kosa na mtu inapaswa ajivunie chama chake. Narudia tena kujitangaza humu JF kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa. mimi ni mwanaharakati wa mazingira na uchumi (mjasiriamali) hila ndoto zangu naona zina zimwa na CCM ndio maana naonekana mpinzani wao. Kiukweli nawa support wagombea wanaopigania nchi hii kuitoa katika kongwa la utumwa wa kiakili, na katika makucha ya mafisadi bila kujali chama wanachotoka.

Turudi kwenye MADA naomba ufafanuzi wa kimahesabu ukizingatia kanuni za MAGAZIJUTO kutoa mchanganuo wa uhalisia wa AHADI za mgombea wako wa chama cha jembe na nyundo, je AHADI hizo zinatekelezeka ndani ya miaka mitano? nakukumbusha zingatia utendaji wake ndani ya miaka mitano iliyopita bila kusahau ufisadi uliotamalaki nchini
 
Unaweza kuwa ni miongoni mwa walimbukeni wengi huko chadema kwa kutetea upupu huu pasipo udhibitisho rasmi. Umbali toka Dsm mpaka Mza kwa treni ni km 1260 hivi. Tena kumbuka vizuri ni kwa treni! Kwa barabara umbali huo unaweza kupungua kwa asilimia kadhaa, na kwa usafiri wa anga unapungua kwa asilimia kubwa.

Ukipima umbali huo moja kwa moja toka kwenye ramani, utapata kilometa 850.20 hivi. Na sijawahi kuona reli iliyoonyoka toka pointi A hadi B kama ambavyo wewe unavyotaka kutuambia hapa!

Reli ya kati imepita katika mikoa zaidi ya minne(Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, na Mwanza), sasa wewe na slaa wako mnataka kutuambia kuwa mtajenga reli mpya bila kupita katika mikoa hiyo? Mtaipitisha angani nini? Je wananchi wa mikoa iliyobaki wasahau huduma hiyo muhimu kwao kwa usafiri?


Wala si ulimbukeni, ni kukosa kwako kuelewa zaidi ya mambo yaliyozoeleka. Kwani kufikiri nje ya mazoea (boksi) kunahitaji ubunifu na uthubutu. Vinginevyo kwako hakuna kinachowezekana. Maelezo ya msingi ni kuwa masuala ya reli zilizopo, barabara, shule, maji, nakadhalika hayastahili kuwa kwenye ajenda ya mgombea uraisi kwani ni ya kawaida. Haina maana kuzungumzia vitu ambavyo raisi yeyote atakayechaguliwa atavitendea kazi. Mgombea anatakiwa kuzungumza vile ambavyo vitamuwezesha kujipambanua na wagombea wengine. Anatakiwa atoe maono ambayo yatatufanya tujue kuwa asipochaguliwa tutakosa 1,2,3 … Si kuwa na rais ambaye akiwepo au asipokuwepo yote sawa tu. Wala haina maana kuwa ukianzisha mradi mpya wa reli basi ya zamani lazima ife. Reli inayozungumziwa, hakika ni mpya na ya moja kwa moja kutoka Dar hadi Mwanza. Huwezi ukawa na vituo lukuki njiani kwa treni ya kasi inayozungumzwa.
Wala si lazima reli hiyo ipitie mikoa uliyoitaja, kwani mikoa hiyo nayo inaweza kuwa na miradi kama hiyo. Mradi huo hauzuii kuigwa sehemu nyingine. Unapokuwa na jambo jipya lazima uwe na pa kuanzia. Kwa maelezo yako unakiri kwa limbukeni kuwa kitekinolojia inawezekana na imeshafanyika kwingine duniani kwa mafanikio. Ila kwa mawazo yako pia unaamini kuwa kwa vile hapa ni Tanzania hiyo haiwezekani. Hiyo ndiyo tofauti kubwa iliyopo kati ya wanaoamini kuwa wanaweza na wa aina yako ambao mnaamini kuwa haiwezekani kufanya chochote. Utawala huu kama ungekuwa ndio unaongoza enzi za kujenga reli ya TAZARA basi akina Kibunango wangeshauri iachwe kwani haiwezekani na inapita porini bila kujua kwamba porini kwa leo (2010) ndiko mjini ifikapo 2030.
[Ukipima umbali huo moja kwa moja toka kwenye ramani, utapata kilometa 850.20 hivi. Na sijawahi kuona reli iliyoonyoka toka pointi A hadi B kama ambavyo wewe unavyotaka kutuambia hapa!]
Umbali kutoka Mwanza hadi Dar usikupe shida. Kwa treni za moja kwa moja (ambazo ziko duniani) kama alivyoainisha mtoa kiroja ni kati ya 250 hadi 400 km kwa saa. Kwa hiyo hakuna ubishi kuwa hizo km 1,000 (kwa njia mpya ya mkato na kona za lazima) zinawezekana kabisa kwa saa tatu. Tukubaliane mpaka hapo. Kama nilivyoeleza hapo awali huu ni mpango wa miaka 15. Katika kipindi hicho teknolojia inayoongezeka kila uchao itakuwa na majibu mazuri zaidi.
[Reli ya kati imepita katika mikoa zaidi ya minne(Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, na Mwanza), sasa wewe na slaa wako mnataka kutuambia kuwa mtajenga reli mpya bila kupita katika mikoa hiyo? Mtaipitisha angani nini? Je wananchi wa mikoa iliyobaki wasahau huduma hiyo muhimu kwao kwa usafiri?]

Treni ya sasa itaendelea na shughuli zake kwani huo ni mpango ambao tayari unafanya kazi. Cha muhimu kufahamu ni kuwa tunahitaji kusogea mbele ya hapo. Huwezi kusogea bila kuwa na mipango. Kwa maneno mengine wakati akina Kibunango mnaamini kuwa miaka kumi na tano ijayo Watanzania
waendelee kuwa na treni na reli ya mwaka 47 (kilomita 65 kwa saa) wenzenu wanathubutu kubuni mpango mpya. Huu ni uthibitisho kuwa hakuna ubunifu wala uthubutu upane wa Kibunango. Kila kisichokuwepo, hakiwezekani kana kwamba sisi si binadamu kama binadamu wengine duniani.

Kibunango, ukitaka kuwaua wanao hali wakiwa hai waimbie tu huo wimbo wako mtamu kuwa hawawezi. Kama hamu yako ni kuidhoofisha jamii iaminishe kuwa haiwezi kuthubutu kufanya lolote. Ukitaka kulifuta taifa katika ramani ya dunia huna haja ya kutumia nyuklia, wewe lilishe tu sumu kuwa taifa hilo haliwezi, utakuwa umefanikiwa “kupita maelezo”.
Tuliambiwa na akina Kibunango hatuwezi kuongoza TANESCO wakaletwa Net Group Solution, nini kilichotokea? Haikutosha tukaelezwa hatuwezi kuendesha hata kampuni ya maji ya Dar es Salaam, wakaletwa. Benki eti tumezishindwa, wakaletwa. Hawakuishia hapo, hata reli waliyojenga wakoloni na ambayo imeendeshwa kwa miaka mingi kwa ufanisi mzuri tu, ghafla tukawa hatuwezi, imekodishwa kwa kampuni ya Kihindi. Kweli hatuna tunachoweza? Hatujui hata kulima na hivyo ili kuokoa kilimo kwanza, wako mbioni kuleta walowezi. Mambo haya yakiachwa kuendelea bila kukemewa na kusitishwa, Watanzania tunaweza kujikuta kuwa kivutio tu cha watalii, kama walivyo wahindi wekundu Amerika na Australia.
Kwa maana: Dawa ya Mjinga ni kuumia
 
Tatizo ni chadema na ahadi za kihuni! Hata wafuasi wake wengi ni wahuni na mfano mojawapo ni wewe mwenyewe! Hebu angalia lugha uliyotumia katika posti yako hapo!

Zaidi nimeona uchambuzi wako yakinifu!

UUNGWANA ni vitendo inawezekana nimekukwaza wewe na wana JF wengine kwa maneno(uliyopigia mstari) niliyotumia katika POSTs zangu naomba RADHI kwako na kama kuna yeyote ambaye maneno niliyotumia yamemkwaza. Lakini FAMI na KUGA ni majina ya wagombea wetu wa urais hapa TZ. Nitatoa tafsiri ya maneno haya ktk post nyingine ili mhakiki kama nimeyatumia kimakosa au la.

Lakini kibunango naomba mchanganuo wa kimahesabu kuhusu kutekelezeka au kutotekelezeka kwa AHADI za mgombea wenu
 
Hili li-article halina urafiki na wasomaji. Weka walau aya basi tuweze kusoma hii post yako. Dah!

Malengo ya article siyo kutengeneza urafiki na wasomaji. Malengo yake ni kutoa changamoto kwa wachangiaji waongeze matumizi ya akili zao badala 'KU-COMFORM' tu, hata pale Walalahoi wa nchi yetu wanapodanganywa mchana kweupee!
Wabunifu wa forum hii wameiita kuwa ni 'HOME OF GREAT THINKERS', tafadhali msiwaangushe!
Una haki ya kwenda kumpigia kura Dr. Slaa siku ya tarehe 31/10/2010, lakini haki ya kuzuia tusichambue ahadi zake huna!
Tunaochambua ahadi za Dr. Slaa hatuna makosa kwa sababu timu yake ya PR na marketing inafanya kazi kubwa kuwashawishi Watanzania kuwa Slaa ni 'Mkombozi' wetu. Unataka tukubali tu? Hiyo siyo sifa ya kisomi hata kidogo!
 
Back
Top Bottom