Hivi CCM walichakachua vipi 2010?

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
Kutokana na Maandamano yanayoendelea sasa inaonekana dhahiri ya kwamba Chadema wanamvuto.Ni chama kinachopendwa na wanachi.Nov 2010 uchaguzi ulifanyika.Kuna malalamiko mengi kuwa CCM wamechakakua.

Kila chama kilikuwa na msimamizi katiko vituo vya kupigia kura...Je nini kilitokea?Je wasimamizi wa vyama vingine mfano Chadema waliruhusu Uchakachuliwaji utokee?au ni mbinu gani amabazo zilifanyika ?

Kwa wale wanaofahamu mbinu zilizotumika naomba waweke wazi...
 
Katika vituo kura zilipigwa na kuhesabiwa vizuri tu.
Kwa kuwa kitabu cha kuandika matokeo kilikuwa na copy nyingi (hadi 13), ni wazi kuna copy ambazo hazikuwa zinasomeka vizuri – any way hilo si tatizo kubwa.
Masanduku kutoka kwenye vituo hadi kata na kata hadi wilayani hayakusindikizwa na vyama; na hata yalipofikishwa wilayani yaliwekwa chini ya ulinzi wa msiamizi wa uchaguzi wa wilaya bila kuwepo ulinzi wa vyama.
Hapa ndipo uchakachuaji ulipofanyika. Yanachukuliwa masanduku ambayo ccm imeshindwa, kura zote zinatolewa na kuwekwa nyingine ambazo nyingi ni za ccm, halafu inaandikwa fomu mpya ya matokeo kwa ushirikiano na msimamizi wa kituo husika, inapigwa muhuri na sahihi za msimamizi na wakala wa ccm (wakati mwingine sahihi za mawakala wa vyama wanazifoji pia ingawa si lazima, kwani msimamizi anasena tu kuwa walikataa kusaini).
Fomu hii mpya ndiyo anakuwa nayo msimamizi wa uchaguzi wa wilaya, wakala wa ccm na nakala ya kwenye kitabu (huwezi kupata nakala iliyobandikwa kituoni kwa kuwa hizo huwa hata asubuhi hazifiki – hubanduliwa mapema sana na kuharibiwa)
Inapofika wakati wa kujumuisha matokeo, utasikia matokeo ya kituo Fulani yanabishaniwa, msimamizi anataja matokeo ambayo chama cha upinzani (tuseme CDM) inayapinga kwa ushahidi wa fomu aliyonayo toka kwa wakala wao ambayo imesainiwa pia na mawakala wa vyama vyote. Utashangaa fomu aliyonayo wa CCM inafanana na ya msimamizi.
Ubishi ukizidi inabidi liletwe box husika ili lihakikiwe! Unachokikuta humo, unajua…
Hivyo ndivyo uchakachuaji mwingi hufanywa. Inapokuwa wamechakachua kwa njia hiyo na bado wakawa hawajashinda, hapo hutumika nguvu za dola tu, fomu ya matokeo ya jimbo inajazwa takwimu ambazo huwezi kupata mlolongo wake toka kwenye vituo. Mshindi anatangazwa, mabox wanayalinda wao, nyinyi mnahangaika na mahakama wao wanaendelea kubadilisha kwenye mabox taratibu etc
Ebu rejea yaliyotokea DSM – fomu na mihuri nk vilivokutwa anatogulo
Rejea pia mabomu yaliyopigwa sehemu mbalimbali.

Hali huwa mbaya sana pale ambapo vyama vya upinzani vimeaminiana na kuweka mawakala kwa kutegemeana (kwa sababu ya uwezo mdogo) lakini vyama vingine vikasaliti chama kingine – hayo yalitokea nadhani karagwe; yaani fomu za matokeo za CDM ndizo zilionekana kuwa tofauti – vyama vingine viwili na ccm na msimamizi matokeo yao yakawa yanafanana!
Kwenye ngazi ya urais hali ni hiyo hiyo, tena unajua watu wengi hufuatilia zaidi kura za ubunge – ina maana wakati mnahangaika na kura hizo huwam hakuna anayekuwa makini na kura za rais. Hata hivyo unakumbuka Dr. Slaa alivyowauliza tume kuwa matokeo mnayotangaza mnayatoa wapi? Mbona fomu alizotumiwa na mawakala wake toka ngazi ya jimbo zinaonyesha matokeo tofauti na wanayotangaza?

Katika sehemu ambazo ccm haikupingwa kwenye ngazi ya ubunge, maana yake mawakala wa vyama vingine huwa wachache tu, hapo kura za urais huchakachuliwa vibaya sana.
Ebu jiulize, inawezekanaje idadi ya watu waliopiga kura za urais ikatofautiana na idadi ya waliopiga kura za ubunge wakati kila mpiga kura hupewa karatasi za kura zote?.

Mkakati wa kudhibiti uchakachuaji huu tulishaujadili kipindi kifupi kabla ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom