Hivi 'audience' ya Clouds Fm ni nani?

Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,831
1,164
Jana kwenye taarifa ya habari ya saa 12 jioni nilisikia mtangazaji wao akisema '' mademu wawili wamefikishwa mahakamani mkoani Shinyanga kwa kosa la shambulio.........''. Hii lugha ya kihuni huwa inamlenga msikilizaji wa aina gani hasa? Hivi hii Radio ina mkuu wa vipindi kweli au kanyaga twende tu.
 
Hio ni Radio ya vijana Mwita25 hio Radio mara nyingi inaendeshwa very informal for ndo their style... Watu wazima wengi wanaosiia ndo wale vijana wa miaka la late 90s na early 2000; ambao they don't mind hio lugha...
 
Biashara yoyote unapoanzisha ni lazima ujue target audience yako ni ipi,kwa kuangalia umri,eneo na jinsia. Sasa ukitazama Radio kama Clouds utaona kuwa audience ambayo wamelenga kwa asilimia zaidi ya 80 ni vijana. Na vijana awa ni wale ambao ni kuanzia miaka 16-35. Kwa hiyo lugha kama hiyo kutumika sio ajabu.
Na nadhani sio wao tu,vipo vituo vingi vya Radio vyenye lugha kama hizo. Nilimsikia Waziri anayehusika na mambo ya habari akisema kuwa Tz ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na vyombo vingi vya habari. Sasa hivi Tz kuna vituo vya Redio zaidi ya 70.
 
iyo redio kiukweli haina hata maadili hata kidogo, japo wanasema ni redio ya vijana ila wapo vijana ambao hawapendi hiyo lugha ya kichenzi sasa unadhani itaheshimika vipi!
 
iyo redio kiukweli haina hata maadili hata kidogo, japo wanasema ni redio ya vijana ila wapo vijana ambao hawapendi hiyo lugha ya kichenzi sasa unadhani itaheshimika vipi!
Shida iko wapi...??? Si waache kusikiliza tu...!!! Unajuwa kuna watu wanataka asichokipenda yeye basi dunia nzima isipende................aaahmxxiiii
 
Me huwa nasikiliza sports extra na kile kipindi cha njia panda kila jumapili. Programe zingine zinaboa kinoma.!
 
No tukubaliane na huu mshangao; ni wapotoshaji audience or not kama hiyo ilikuwa ni taarifa lazima kuwa makini
 
Hio ni Radio ya vijana Mwita25 hio Radio mara nyingi inaendeshwa very informal for ndo their style... Watu wazima wengi wanaosiia ndo wale vijana wa miaka la late 90s na early 2000; ambao they don't mind hio lugha...

sidhani! radio hii ni kwa ajili ya vijana ambao hata maishani hawajielewi, i mean hawana agenda! vijana wa kawaida huwa tunaskiza muziki wao tu, lakini sio ile mijadala ya kina asalamaleko!
 
kundi kubwa la watanzania ni vjana na asilimia kubwa ni wale ambao hawajaelimika hao ndiyo wasikilizaji wakubwa wa haka karedio ka mashoga. nimejaribu kufatilia nimegundua kuwa waskilizaji wake wengi ni mabeki3 na wa mama wa nyumbani. ukiangalia sana washabiki wa haka karedio ndio washabiki wa movie za kibongo hahahaaaaaa. nimefuatilia sana hasa vyuoni mara chache sana kukuta wanaskiliza hii redio au kutazama movie za kibongo, movie zao wasomi wanaita tutorial ambazo huangalia sana wawapo campus.
 
kwa kifupi wasikilizaji wa redio hii ni vijana kuanzia form 1-6,wafanyakazi wa saluni za kike na kiume,wapenda bongo fleva, na kuna vipindi vya asubuhi na taarabu ambavyo walengwa ni mama wa nyumbani na mahausigeli.

Lakini kuna hichi kitoto Shadee nadhani hivi karibuni itabidi nichague watu 2-3 hapa JF mkapeleke barua ya posa kwao nimetokea kumpenda sana.
 
naomba niwe kwenye ujumbe wako wa posa mkuu.
 
Jana kwenye taarifa ya habari ya saa 12 jioni nilisikia mtangazaji wao akisema '' mademu wawili wamefikishwa mahakamani mkoani Shinyanga kwa kosa la shambulio.........''. Hii lugha ya kihuni huwa inamlenga msikilizaji wa aina gani hasa? Hivi hii Radio ina mkuu wa vipindi kweli au kanyaga twende tu.
arrrg wewe nawe thread zako zimekaa ki saluni saluni mambo ya leo tena na umbea umbea acha hizo wewe.Acha thread zako za kike kike
 
arrrg wewe nawe thread zako zimekaa ki saluni saluni mambo ya leo tena na umbea umbea acha hizo wewe.Acha thread zako za kike kike

thread za kike zikoje na za kiume zikoje? I hate mwanaume anaedharau wanawake. Bila uwepo wa u-kike wewe ungekuwepo vipi duniani? Watu wengine mnakera sana...tpuuu
 
Back
Top Bottom