Hivi, Ali Mufuruki ulitaka kuiuza Gymkhana kwa wawekezaji?

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Kuna watu wengine unajiuliza hivi tamaa zao zinaisha lini jamani.

Huyu mheshimiwa sana ameshiriki mno kuimaliza ATCL na wenzake, mbaya zaidi ATCL aliondoka kwa aibu kubwa pale, akiwa na wenzake waka-lease ndege kutoka South Africa, mkataba ukaisha wakazirudisha South Afric.

Wakiwa wanajiandaa, wakadai kuna ndege kutoka Ireland nzuri zinamaliziwa kupakwa rangi ya AirTanzania.... Baada ya muda kumbe zile zile zilizochoka zikarudishwa South Africa wakazipeleka Ireland ili zitokee kule.

Ilikuwaje?

Wakati wanaandika mkataba wa ku-lease ndege, mmoja wa watanzania wenye uchungu na nchi hii akachomoa baadhi ya karatasi zikapelekwa kwa wenye shule... Kuanza kuchunguza moja ya registration ya zile ndege zilioandikwa zinakuja ni sawa na ile iliyorudishwa South Africa

...ilimchukua muda kuamini kilichotokea na kuanza kufukuza fukuza mpaka mwisho akaamua kuondoka!

Sasa, pengine wasiomjua kwa hili la kutaka kuuza kiwanja cha Gymkhana si jipya kwake... Anaangalia opportunity bila kujali maslahi...

Kwanza nakupongeza Malinzi kwa kushtuka na wenzako hili, kwa kweli watanzania wachache wanaoweza kutamka tumezungukwa.

Hili la Mufuruki kuleta wawekezaji ati akitaka kuwapa kiwanja wajenge Hotel sidhani hii nchi kama itaendelea kuwa na walafi hivi... kuna wakati unamwona mtu smart kwa nje kwa ndani hatari...

Mwisho, nawapongeza kwa kumwondoa kabisa kwenye maswla ya Gymkhana; naamini angewaharibia maisha yenu na watoto wenu
 
  • Thanks
Reactions: ral
Huwa nawashangaa sana watu wanaomsifia huyu mtu kuwa ni mjasiriamali wa kuigwa Tanzania, khaaa! ufisadi nao ni ujasiriamali?
 
Hatakama angeuza yeye hana hasara kwa kuwa yeye sio Mtanzania. Ni Mganda na wazazi wake wote wako Uganda. Urafiki wake na Mkapa ndio unaleta matatizo mpaka leo. Tusubiri mengine mabaya zaidi toka kwa huyu baba.
 
Huwa nawashangaa sana watu wanaomsifia huyu mtu kuwa ni mjasiriamali wa kuigwa Tanzania, khaaa! ufisadi nao ni ujasiriamali?

Mkuu hujui hapa nchini sasa hv ukiwa fisadi unaheshimika na kusifiwa ? Kuna siku nilikuja ndege moja na Rostam yeye akapita VIP nikachoka kabisa
 
Ninavyofahamu huyu jamaa hana shida hiyo na kilichokuwepo pale gymakhana ni siasa za ugomvi wa madaraka nina uhakika jamaa atashafishwa kwenye hilo.
 
Mfuruki aling'oa makabati ya kuwekea vifaa vya michezo ya wanachama na moja ya chumba akakifanya msikiti akiwa kilabuni huingia humo kwa swala muda wa kuswali unapofika.
 
Ninavyofahamu huyu jamaa hana shida hiyo na kilichokuwepo pale gymakhana ni siasa za ugomvi wa madaraka nina uhakika jamaa atashafishwa kwenye hilo.

Ni kweli amesafishwa kwa uanachama wake kusimamishwa kwa muda wa miezi mitatu.
 
Ninavyofahamu huyu jamaa hana shida hiyo na kilichokuwepo pale gymakhana ni siasa za ugomvi wa madaraka nina uhakika jamaa atashafishwa kwenye hilo.
Ni kweli kabisa. Huyu jamaa anaheshimika sana tu ndani na nje na sidhani kama hayo yaliyoandikwa ni kweli.

Kwa ufahamu wangu ni kuwa Gymkhana ni chombo binafsi na wenye mamlaka nacho ni wale tu wanaohusika nacho. Hivi sisi kujiingiza tu kwa kutumia dhana ya hisia,hearsays, internal politics etc bila kuwa na uhakika ni dhambi kubwa sana.

Huyu bwana mimi binafsi sijawahi kuonana naye ila sifa na heshima yake nimeisikia nchini mwetu pamoja na nje.

JAMANI BILA UTAFITI NI DHAMBI SANA kumpaka mtu tope. Jee baadaye ikigundulika kuwa figisu zote hizo zinatokana na ugomvi wa ukubwa mtasema nini?????
 
Mfuruki aling'oa makabati ya kuwekea vifaa vya michezo ya wanachama na moja ya chumba akakifanya msikiti akiwa kilabuni huingia humo kwa swala muda wa kuswali unapofika.
Sasa hapo tatizo liko wapi. Kenge wewe
 
Sasa hapo tatizo liko wapi. Kenge wewe

Kama aliyoyafanya yalikuwa mazuri, si angedumu kwenye nafasi yake; kwa taarifa Mfuruki ndiye mwenyekiti aliyekalia kiti kwa muda mfupi kuliko wote tangu club ianzishwe mwaka 1916.
 
Back
Top Bottom