HIV inanitesa

HIV+

Member
Sep 25, 2012
8
54
Habari zenu wana jamvi.
Naombeni maoni yenu /michango yenu.
Mie ni Mdada wa miaka 30 nima MBA ya UDSM na nimebahatika nimeajiriwa hapa DSM mitaa ya post mpya.Pia nina ishi na Virus visababishavo ukimwi (HIV)

Naisha maisha ya kawaida kabisa nimejenga na nina kiusafiri cha kunifikisha popote napotaka kwenda.Vile vile ni Mrembo nimeumbika haswaa maji ya kunde umbo la kibantu haswaa hakuna mwanaume akutane na mie asigeuke mara mbili mbili kuniangalia.

Niliishi maisha ya kawaida tu hapo awali adi mwaka 2008 mwishoni nilipata mchumba kwenda kupima mie nikangundulika nimeathirika wapendwa.kweli ilikuwa hali ngumu sana kwa upande wangu.Nikakaa kimya adi leo sijawambia mtu ndo naweka wazi hapa Jamii leo hii.Namshukuru Mungu nina afya njema sana sina hapa uwezi kujua hata ukiambiwa uwezi kukubali.

Shida ni hii hapa Unyanyapaa kwa baadhi ya jamaa zetu katika jamii zinazotuzunguka umekuwa mkubwa sana.
Hali hii uwa inanipelekea kutaka kuambuka kwa makusudi wanaume wanaojigonga kwangu.Na wakati mwingine mie kama binadamu uwa najikuta kwenye mahusiano kama mjuavyo mara ya kwanza mtatumia kinga ya pili njema inataka kavu hapo ndo uwa napatwa na ngazi mwili mzima.

Jamani napenda kutoa wito kwa waathirika mwenzangu hapa Jamii forum tujiunge walau tufanye ka network ketu ili tuangalie namna ya kupambamba na Maradhi+Unyanyapaa na kukumbusha jamii UKIMWI upo nna pia hauchagui.Maana sie wagonjwa ndo tunajukumu la kuwalinda hawa wanao tunyanyapaa.

Tukichukulia Hasira unyanyapaa nawaaambia waTanzania wengi watapoteza maisha yao kwa HIV.
Na ninajutia sana Kwa kuwaambukiza wengine kwa taama zao za kimwili.
Asante
HIV+
 
pole sana dada, ila sasa nakushauri uwe mtu wa kusali zaid ili Mungu akue faraja kuepuka unyanyapaa. pia nakuombea usiwe na hasira zaid ili usije ukawaambukiza wengine kama ulivyosea. nimeupenda sana moyo wako wa dhati wa kuwalinda ambao bado hawajaathirika. mungu akubariki
 
I salute you kwa kweli. Penye nia pana njia just keep good faith HIV ya siku hizi is manageable na huna sababu ya kuwambukiza wengine course what goes around comes around. ! Huo unyanyapa utakuwa unatoka wale wasiojitambua, wasamehe bure, a brighter day must be coming to you.
 
oh!sikia mamii
hebu badilisha kwanza hyo user name yako,umeanza kujinyanyapaa mwenyewe!
kuwa ni mwathirika sio kifo,una nafasi ya kufanya mengi sana ambayo wengine(tunaoamini hatuna )hatufanyi
jipende na furahia maisha,kuathirika sio sababu ya kujikataa na kuwapa wengine sababu ya kukukataa au kujustfy kukataliwa na jamii,hiyo jamii inayokunyanyapaa yenyewe haijui hali zao kiafya ziko vipi
jichanganye na marafiki wengine watakaokupa tumaini la kuwa maisha yanaendelea,ukijifunga na kuamini kuwa kwa kuwa ur HIV+ basi marafiki unaowastahili ni wa aina hiyo tu hujitendei haki my dear!
wewe ni wa thamani sana na wa pekee!
thamani yako kama mwanadamu inabaki palepale haijalishi jamii inakuchukulia vipi!ulianguka hapo umefanikiwa kusimama ishi maisha yako unayodhani ni salama kwako na kwa wenzio!
 
Huwezi kujua kama upo wala kuugopa mpaka ukute umeathirika, jamani this disease is very real, ipo, ipo kabisaaaaaaaa! Ahsante mdada kwa kutukumbusha, usiwaambukize wengine, utapata neema na thawabu zako kutoka kwa MUNGU! MUNGU akuongoze na kukufariji katika kipindi chote cha ugonjwa wako, na sisi wengine jamani tuache kucheat, ambao hawajao/olewa wafanye hivyo na wastick to one man/woman marriage, sio mzaha hali ni mbayaaaaaa!
 
They call me King Kong, copy?
They call me King Kong, copy?
They call me King Kong, copy, copy, copy?
They call me King Kong, copy?
Big ballin’ is my hobby
So much so they think I’m down with the
illuminati
My watch do illuminate
My pockets are tottie
But I’m God body, ya’ll better ask
somebody
I was born a God
I made myself a king
Which means I down graded to a human
being
You was born a Goddess
I made you my queen
Which means we upgraded to Louis the
thirteen
Hot tottie, her body like cognac
Her momma likes herb tea
We birthed a couple of sacks
And after she sleeped, I creeped in to
her tee-pee
We did it Indian style, had the girls
speaking
In tongue she like young, you hung,
what you done, done
Stop it fore you wake up my momma
might (ahhhh)
Now that I’ve arrived it’s time that I go...
I’m so cold, I’m so cold...
I’m like oh Kimosabe
Your body is my hobby
We’re freakin’
This ain’t cheatin’ as long as we tell
nobody
Tell your girls you’re leaving
I’ll meet you in the lobby
I’m so cold, yeah I need that hot tottie
Hot tottie (hot tottie)
Hot tottie (thought I’d never fall in love,
thought I’d never fall in love)
I’m so cold, I’m so cold (ho)
I’m so cold, I’m so cold (ho)
I’m so cold, I’m so cold (ho)
I’m so cold, I’m so cold (ho)
I need a hot tottie
Will you be my hot tottie?
She said she wanna make me better
She wanna make me better
 
HIV ilikuwa ni death sentence maika iliyopita, siku hizi ukichanganya lifestyle na dawa uanweza kuishi vizuri na kutimiza maana ya ule wimbo wa zamani katika kipindi cha kusalimia wagonjwa cha "Pole" "Ajuaye bwana mola kwa mzima kuwa mfu, mgonjwa kuwa salamaaaa, leo tunawapa poleee".

Nakusihi sana usifanye maambukizo ya makusidi kwa maana hilo ndilo linamtenganisha binadamu na mnyama.
 
Baada ya kuusambaza ndio umepata busara sio?

Mkuu Safari_ni_Safari hautakiwi kumjibu hivyo. Yeye ameshasema anajutia kwa kuwaambukiza wengine. Inatosha maana ameshajutia na hivyo kutubu. Tunachotakiwa kufanya ni kumpa moyo aendelee kijilinda na kuwalinda wengine. Tuache unyanyapaa maana unyanyapaa ndio kiama chetu pale wanao nyanyapaliwa wanapoamua kuambukiza makusudi ili kulipa kisasi. Tuache unyanyapaa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom