HITS yaaga Tanzania

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
Wakati watanzania hawajasahau jinsi walivyolizwa na great television (GTV), ambayo ilifunga mitambo yao kama wiki mbili zilizopita, tayari mtandao mpya uitwao Excellentcoms au HITS nao unafunga virago kuondoka Tz baada ya mwekezaji kufilisika huko Marekani. Mtandao huo ambao ulikuja kwa kasi ya ajabu, ukiwa umejenga minara karibu kila kona ya nchi na ukitarajia kuanza kutoa huduma zake tangu December 2008, sasa umewapeleka likizo wafanyakazi wake na hatima yake haijulikani.

Pia inasemekana kuwa Barclays Bank nayo inachungulia kaburi wenye mafedha huko kaeni chonjo
 
Mhh..Jamani tunaweza kuwa wazi zaidi hapa kuhusu kuanguka kwa hii company ya simu..na Barclays...au bado habari ni tetesi?
 
Hao barclays Tanzania,ukiacha msukosuko wa kiuchumi,wao siyo watu makini kabisa.kuna malalamiko mengi ya wateja ambao wanalalamikia makato ambayo hayaeleweki. huduma zao ni mbovu,ukienda kupata huduma unazungushwa hawajali muda wa watu, wanafikiri wao peke yao ndiyo wanaofanya kazi.Mbaya zaidi baadhi ya wafanyakazi ni wezi,hii inatokana mfomo wao mbovu kwenye ajira,undugu ukabila,urafiki.unategemea nini kutoka watu wanaojenga matabaka kama hayo.Mkitaka kufanya vizuri pigeni chini idara ya HR,muajiri watu wanaojua kazi.ACHA MKONG'OLIWE SANA,KWANI MLIYAANDAA HAYO MAZINGIRA NINYI WENYEWE.
 
umbea mtupu, hits tanzania bado iko kwenye maandalizi na wafanyakazi wake wote wapo kazini....
 
...mbona inasemekana hii HITS imeuzwa kwa Orange,hata Uganda ilikuwa ianze nasikia wameuza kwa Orange haohao
 
Watanzania wenzangu,

Hili la mabenki kuweni makini kidogo, haya mambo ya mabenki yako so... delicate... kwa rumours tu... mwaweza kufanya benki ifilisike... kuweni makeni....

Kuhusu HITS... kwa kweli huenda Orange wakachukua... kumbukeni Orange, wamewanunua Telecom Kenya... na HITS ya Uganda... huenda wasione shida kuingia Tanzania wakamate EAC.
 
Mwekezaji wa hits anaelekea kufilisika ktokana na global financial crisis na inasemekana kuwa amefunga matawi yote kasoro nigeria, kuna wafanyakazi wa hits tanzania wameahidiwa ajira nigeria hapo bongo ni likizo na kusubiria wafunge ofisi, mlioko hits jueni hili.

Kuhusu barclays, lets keep our finger crossed, mliosoma east african ya wiki hii, huko barclays wamepunguza lending rate!!! Ina maana wanatoa mikopo kwa mahesabu kwa nini? Jiulizeni
 
Hivi ninyi ambao kila kikiwekwa kitu mnahoji source, mnataka kila mmoja aweke source yake hapa? wengine ni source wao wenyewe na kama utabisha kuna siku watu humu wakijitambulisha wengine mtakataa na kuhoji source ya utambulisho wao.
 
Hivi kwani hawa Hits waliashaanza operations zao? Tangu mwanzo walionekana wababaishaji (msiniulize source!).
 
Hivi ninyi ambao kila kikiwekwa kitu mnahoji source, mnataka kila mmoja aweke source yake hapa? wengine ni source wao wenyewe na kama utabisha kuna siku watu humu wakijitambulisha wengine mtakataa na kuhoji source ya utambulisho wao.
ndio maana mleta mada akaita ni tetesi!!! i like that maana inajibu ubishi wote
 
Mwekezaji wa hits anaelekea kufilisika ktokana na global financial crisis na inasemekana kuwa amefunga matawi yote kasoro nigeria, kuna wafanyakazi wa hits tanzania wameahidiwa ajira nigeria hapo bongo ni likizo na kusubiria wafunge ofisi, mlioko hits jueni hili.

Kuhusu barclays, lets keep our finger crossed, mliosoma east african ya wiki hii, huko barclays wamepunguza lending rate!!! Ina maana wanatoa mikopo kwa mahesabu kwa nini? Jiulizeni
ina maana hii crisis imeikumba barclays bongo gafla au ni ile expansion plan yake haikuwa sawa!!!!?

maana jamaa walivyoexpand inaonekana hawakuwa wamejipanga sawa labda.
kwani kama walikuwa ni profit centre haikuwa na haja financial crisis ikawasumbua maana was mass banking to local communities in tz....

naomba mnijuishe zaidi source ya tatizooo
 
Hivi ninyi ambao kila kikiwekwa kitu mnahoji source, mnataka kila mmoja aweke source yake hapa? wengine ni source wao wenyewe na kama utabisha kuna siku watu humu wakijitambulisha wengine mtakataa na kuhoji source ya utambulisho wao.

Baelezee hao akina Tomaso
 
Hits hawaja layoff wafanyakazi wake. Ingawa globally wame kuwa affected lakini uwezekano wa (HITS Tanzania)ni kununuliwa na Orange.

So far wapo kazini wafanyakazi. Nimeongea na mmoja wao.
 
swali ni kwamba tunajuaje kwamba huu haukuwa mpango wao tangu waje?? orange is big competitor wa vodafone outside of africa (mideast, asia , europe etc)...hawajataka kuingia kichwakichwa bongo ambapo vodacom the biggest and most profitable mobile company is fully owned by vodafone. jus a theory? source competition law. lol
 
Back
Top Bottom