Historia ya Wimbo wa Taifa wa Tanzania na mtunzi wake

Melody za wimbo huo ambao kwa Tanzania unaitwaMungu Ibariki Afrika, zimetoka kwenye wimbo uitwao Nkosi Sikelel iAfrika, neno la lugha ya Xhosa lenye maana hiyo hiyo pia). Wimbo huo ulitungwa mwaka 1897 na Enoch Sontonga, aliyekuwa mwalimu kwenye shule ya misheni ya jijini Johannesburg.

Wimbo huo ulianza kutumika kama wimbo maalum wa hekaheka za ukombozi wa Afrika na baadaye kuanza kutumiwa kama nyimbo za taifa za nchi tano barani Afrika, zikiwemo Zambia, Tanzania, Namibia na Zimbabwe baada ya kupata uhuru.

Mwalimu Santonga aliwaza afrika akaitungia na wimbo wakati wengine waliwaza nchi zao na makabila yao na vyama vyao.

Hakuwa mwanasiasa lakini legacy yake iko hadi leo.Hakuwa mwalimu wa nyimbo lakini alitunga wimbo uliogusa Afrika unaoishi hadi leo.

Hakuwaza kulipwa wala kuuwekea hati miliki kama waimba nyimbo uchwara wa leo ambao nyimbo zao huishia hewani au katika makaburi ya sahau baada ya kuchuja baada ya muda mfupi.

I Salute you.Teacher SANTONGA.
 
Safi sana hiyo elimu kwa wasioijua.
Huyu Enoch Sontonga amezikwa makaburi karibu na jiji la Johannesburg, nimepita eneo hilo.
Hata hivyo kaburi lake halisi halijulikani.
 
wabongo wengine vichaa mtu anaandika vitu vya maana wengine wanalete vitu vya upumbavu. Wamekuwa kama watoto wa chekechea
 
Safi sana hiyo elimu kwa wasioijua.
Huyu Enoch Sontonga amezikwa makaburi karibu na jiji la Johannesburg.
Hata hivyo kaburi lske halisi halijulikani.

kama wa-South wangelikua wanaljua kabur lake wangekua wana li praise sana,wako deep sana kwenye kuwakumbuka ma Legends kwny taifa lao...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom