Historia ya wamasai kutokea Israel hadi Africa mashariki

localizer

Senior Member
Jul 25, 2015
121
70
Makabila mengi yaliyopo Tanzania siyo ya asili ya hapa mengi yalihamia miaka ya zamani na kuweka makazi haswa kutokana ardhi hii kuwa na ardhi yenye rutuba kwaajili ya kilimo na malisho ya wanyama.

Sasa ifahamu historia ya Wamasai kutoka Israel hadi Afrika Mashariki.Inasadikika kwamba katika karne za mwanzo kabisa, Safari ya Wamasai (Maasai trek) ilianza kutoka Mashariki ya kati (Israel) kuelekea kusikojulikana (kwa wao). Walianza safari yao kwa kukatiza katika jangwa la Israel kuelekea Misri. Walipofika katika ardhi ya Mesiri (yaani Misiri ya leo) walikuta hali ya hatari kwao na kwa mifugo yao (kumbuka ni safari ya jumla jumla yaani watu na mali zao).

Hali ile iliwafanya wanyama wao kujikondoea na kuanza kufa kwa njaa. Hata maziwa ambayo ni chakula kikuu yalikosekana kabisa. Hii ndio asili ya neno "Mesiri" (ikiwa na maana ya ukosefu wa maziwa) ambaye baadae ilikuja kuoanishwa kuwa "Misri kwa maana ya nchi ya Misri." Waliendelea kusogeasogea (kumbuka hii ni safari isiyo na Mwelekeo bali kutafuta pahala patakapowafaa wao na mali zao yaani wanyama), wakati huo walijikuta hawajui pakuelekea kwaiyo wakawa wanaulizana "Kailo?"

kwa maana ya kwamba unaelekea wapi? Hili neno ndo lilikuja kutoa jina la Mji mkuu wa Misri "Cairo."Waliendelea kusogeasogea kuelekea kusini. Walifika mahali wakaanza kupata matumaini ya uhai wao kwani walikutana na hali nzuri ya hewa na maji. Hali hii ilisababisha pahala pale kuitwa "Isidan"kwa maana ya ardhi yenye matumaini.

Hili neno ndo asili ya jina la "Sudan." Ardhi ile ilizidi kuwapa Matumaini ya Maisha watu hawa na wanyama wao.Kuashiria kwamba walianza kuona cheche za Matumaini tofauti na Mesiri (Misri) walikotoka walipaita pale "Kitum (yaani tutapata)." Neno hili ndo asili ya jina la mji mkuu wa Sudan (Isidan), Khartoum.Wakiwa Isidan (Sudan), walikuta mto mkubwa wenye maji masafi walioita "Nailiil (maana yake maji ya kung'aa). Mto Nailiil (Nile) ilizidi kuwapa matumaini makubwa katika ardhi ya Isidan (Sudan) ambapo walikaa kwa miaka kadhaa kwenye maeneo ya Kitum (Khartoum).

Kama kawaida ya nyakati, mzunguko wa majira uliendelea kuwakanganya watu hawa kwa Maana ya Kiangazi. Kukosekana kwa majani ya malisho katika maeneo hayo kuliwapelekea kuanza safari kuelekea kusini kusikojulikana.Safari yao ilichukua miaka na miaka. Katika safari hii ngumu wamasai walipoteza watu wengi kwa uzee, magonjwa na njaa. Kwaiyo vizazi na vizazi vilitokomea wangali hawajapata makazi ya kudumu.Kila kukicha ni safari, tena, kuelekea kusikojulikana.

Watu hawa walifika mahali tambarare sana. Ardhi hiyo ilikuwa kubwa na usioweza kuona mwisho. Paliwafaa kwa makazi kwa wakati fulani. Ardhi hii waliita "Kinyaa, kwa maana ya tambarare." Neno hilindo asili ya nchi ya "Kenya." Waliendelea kusogeasogea kwenda kusini mpaka walipokuta ardhi yenye baridi kali sana. Walikaa kwa miaka kadhaa katika eneo lile. Hali ya baridi iliwapelekea watu wale kupaita eneo lile "Inairobi, kwa maana ya penye baridi." Hii ndio asili ya jina la mji mkuu wa kenya, Nairobi.Kama kawaida ya wafugaji (Normadic pastoralism) waliendelea kuhamahama. Walianza kusambaa kwenda sehemu mbalimbali.

Walipotoka Inairobi walianza kugawanyika. Kuna walioelekea Inaarook (kwa maana ya vyeusi. Jina hili lina asili ya aina ya miti yenye stamina nyeusi kwa ndani ipatikanayo katika msitu wa Mau, Kenya.). Wakiwa Inaarook (yaani Narok ya sasa) walikupambana na baridi kali kutoka katika msitu Mkubwa wa Mao (Endim e Maondio jina walioita). Kutoka pale wakasambaa kuelekea sehemu mbalimbali kusini mwa Kenya. Wengine walielekea Orkeju oodo (Kajiado), wengineMaasai Mara n.k.

Katika kipindi hichi, baadhi walianza makazi ya kudumu kwaiyo wakati wenginewakihama kuna waliobaki.Kupitia Iloitokitok, Kajiado na Masai Mara watu hawa walianza kuingia Tanzania. Wa Iloitokitok wakaingilia West Kilimanjaro, Wa Kajiado wakaingilia Namanga na wa Masai Mara waliingilia Loliondo (hakukuwa na Uhakika kama majina haya yalikuwepo kipindi hicho ama yalipatikana baadae). Kuanzia hapo WILAYA ya Masai ikapatikana (Baadaya maswala ya Utawala kuanza).

Wilaya hiyo ilijumuisha Ngorongoro ya sasa, Simanjiro, Longido na Monduli ambayo kwa mara ya kwanza nadhani iliongozwa na Hayati Edward Moringe Sokoine. Hiyondo safari ya Wamasai kutoka Afrika ya kati mpaka Afrika mashariki.Historia hii niliipata kwa njia ya simulizi kutoka kwa Mzee mmoja kijiji cha Loiborsiret, kata ya Loiborsiret, Tarafa ya Emborret, wilaya ya Simanjiromkoani Manyara, December 21, 2015 saa mbili asubuhi. Ilikuwa ni moja ya stori zilizonisisimuasana na kunifikirisha kama msomi na mwanajamii wa kimasai.

Nilimuahidi kwamba nitaendelea kuwaambia na wengine kuhusu historia hii. Mzee huyu amefanya kazi chini ya serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne (amestaafu kwa sasa) ambapo alihudumu katika Idara ya Wanyamapori, Afisa mtendaji katika Kata na Tarafa mbalimbali na kwingineko.Shukrani za dhati kwa mzee huyu.

Maarifa yake itaendelea kuishi ndani yetu. Ahsante msomaji wangu.Wako katika Jukwaa laHistoria,

Lokaji Laizer
 
Da! kumbe hiyo ndo asili ya wamasai kwamba wametoka esrail KWELI SHIBE INAKUSUMBUA SIJUI UMEKULA MAKANDE
 
Binafsi sijajua kama hii history ni kweli.lakin kwa uelewa wangu wamasai wamekuwa wakuhama hama saba na majina ya maeneo mengi kwa tanzania na kenya wao waliishi siku nyingi na kupatungia majina
 
Akili ni nywele lakini mleta uzi avatar yako una kipara, kama huna nywele haya usemayo nitaamini vipi?
 
Kama kuna mtu ana ya kwake yenye ukweli, iweke hadharani nayo tuipime. Hongera kijana Laizer umejitahidi. Ila huyo mzee hajakueleza kwa nini wslishindwa kuendelea kusini kwa lengo la kufika ziwa Victoria.
Sasa nakuambia walikwaa kisiki cha Wakurya, ambao walikuwa wamejikita katika maeneo yenye rutuba na malisho mazuri. Kwa miaka mingi Wamaasai lengo lao kuu ilikuwa kutua ziwa Victoria kwa kuambaambaa na mto Mara na hii imewagarimu kupoteza wapiganaji wengi kwa kujaribu kupenya ngome imara ya Wakurya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom