Noti niliyopenda kuliko zote... Nakumbuka nilikuta Kibunda Chumbani kwa Mdingi wangu nikazihesabu zote zilikuwa mpya Hesabu yenyewe iliishia elfu tatu first time kushika pesa Nyingi nilishangazwa... nakumbuka ndio nilikuwa naongoza class kwa Hesabu so nilizihesabu twice nijue sijakosea...10 Tz Shilling
Umeona eeh? Katukumbusha mbali sanaKichuguu wewe ni jembe aisee!
Wiki chache zilizopita niliwaletea historia ya fedha ya sarafu hapa nchini kwetu nikaahidi kumalizia na historia ya noti. Kwa bahati mbaya majukumu yamenizidi nikashindwa kupata nafasi ya kuiandika ingawa nilikuwa nimeshaifanyia utafiti wa kutosha. Leo hii nimeamua kulivalia njuga ili niikamilishe, samahani sana kwa wanachama kwa vile historia hii ni ndefu kidogo kuliko ile ya sarafu kwa vile noti zilipitia mabadiliko mengi sana kuliko sarafu.
Kwa muda mrefu fedha zilizotumia katika nchi hii zilikuwa ni sarafu. Noti za karatsi zilianza kutumiaka mwaka 1905 wakati wa utawala wa mjerumani kwa upande wa bara. Noti hizo zilitolweka katika thamani ya Rupie 5, 10, 50, 100 na rupie 500 kama ionekanavyo hapa chini. Noti za rupie 500 zilikuwa chache sana na sikufanikiwa kupata picha yake
Rupie 5
Rupie 10
Rupie 50
Rupie 100
Kwa upande wa zanzibar, mwaka huo huo wa 1905, noti za Rupee za kizanzibari zilitolewa katika thamani za Rupee 5, 10, 20, 50, 100 na rupee 500 pia. Kwa bahati mbaya sikuweza kupata picha zake zote, naonyesha mfano wa noti za rupee 5 tano tu niliyofanikiwa kupata.
5 Zanzibari rupee
Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, serikali ya kijerumani ilitoa noti za dharura ambazo zilikuwa ni za karatasi ya kawaida kabisa. Noti hizi zilikuwa katika thamani za Rupie 1, 5, 10, 20, 50 and Rupie 200 ingawa hizi za Rupie 200 zilikuwa adimu sana na sikufanikiwa kupata picha yake
1 Rupie
5 Rupien
10 Rupien
20 Rupien
50 Rupien
Noti hizi za dharura zilikuwa hafifu sana na wakati mwingine zilikuwa zinafyatuliwa kwa muhuri tu kama hii hapa chini ya Rupie 1.
Inaelekea kuwa mji wa Tabora ulikuwa na umuhimu wa pili kwa dar es salaama wakati wa serikali ya kijerumani kwa vile unaonyeshwa katika Noti zote. Kama mtakumbuka, ile sarafu ya dhahabu ya Rupie 15 ilikuwa inaitwa "Tabora Pound."
.....INAENDELEA
uko vizuri Mkuukweli hata mimi nimependa
Asante kwa kurekebisha rekodi, hata hivyo jambo hilo lilijibiwa zamani kidogo na mchangiaji mwingine, nadhani ilikuwa kipindi hicho hicho nilipopost thread hii, yaani mwaka 2007 (karibu miaka kumi iliyopita!)Kichuguu nyuma ya noti ya shilingi 1000 haikuwa kiwanda cha nyama cha Kawe bali mgodi wa makaa ya mawe Kiwira
Nimegundua mimi mwenyewe nililijibu jambo hili mwaka 2011 ndipo tukapigia debe uwepo wa jukwaa la Historia.Asante kwa kurekebisha rekodi, hata hivyo jambo hilo lilijibiwa zamani kidogo na mchangiaji mwingine, nadhani ilikuwa kipindi hicho hicho nilipopost thread hii, yaani mwaka 2007 (karibu miaka kumi iliyopita!)
Eti nyie Wanzibar wenzangu mbona mwajitoa ufahamu, mnadai haki kwa kichuguu, yeye alichofanya Ni kuleta historia hapa. Hizo fedha zingine hazitumiki sasa hivi alaah mbona mwatuabisha, si mfungue mada muelezee jinsi mlivyonyimwa haki Kama ipo.Lakini Alikuwa Rais Wa Kwanza Wa Zanzibar
Na Ni Muhimu Sana Kwa Wananchi Wa Zanzibar Nao Kuona Kuwa Viongozi Wao Wanathaminiwa
Pesa Zimejaa Mijinyati Na Mijingombe Tuuu Halafu Watu Wa Zanzibar Wanachorewa Kijimlango Au Kijitawi Cha Rafuuu
Where Is The Fairness?
Nyie Mambo Haya Mnaona Mambo Haya Ni Madogo Lakini Yanasemwa
Tujikumbushe tulikotoka. Hizi ni baadhi ya noti zilizowahi kutumika kwa malipo halali hapa Tanzania.
Unakumbuka nini wakati wa matumizi ya noti hizi?View attachment 353754View attachment 353755View attachment 353756View attachment 353757View attachment 353758View attachment 353759View attachment 353760View attachment 353761View attachment 353762