Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,496
19,332
Wiki chache zilizopita niliwaletea historia ya fedha ya sarafu hapa nchini kwetu nikaahidi kumalizia na historia ya noti. Kwa bahati mbaya majukumu yamenizidi nikashindwa kupata nafasi ya kuiandika ingawa nilikuwa nimeshaifanyia utafiti wa kutosha. Leo hii nimeamua kulivalia njuga ili niikamilishe, samahani sana kwa wanachama kwa vile historia hii ni ndefu kidogo kuliko ile ya sarafu kwa vile noti zilipitia mabadiliko mengi sana kuliko sarafu.

Kwa muda mrefu fedha zilizotumia katika nchi hii zilikuwa ni sarafu. Noti za karatasi zilianza kutumika mwaka 1905 wakati wa utawala wa mjerumani kwa upande wa bara. Noti hizo zilitolewa katika thamani ya Rupie 5, 10, 50, 100 na rupie 500 kama ionekanavyo hapa chini. Noti za rupie 500 zilikuwa chache sana na sikufanikiwa kupata picha yake

Rupie 5
doa_5rupien.jpg

Rupie 10
doa_10rupien.jpg

Rupie 50
doa_50rupien.jpg

Rupie 100
doa_100rupien.jpg

Kwa upande wa zanzibar, mwaka huo huo wa 1905, noti za Rupee za kizanzibari zilitolewa katika thamani za Rupee 5, 10, 20, 50, 100 na rupee 500 pia. Kwa bahati mbaya sikuweza kupata picha zake zote, naonyesha mfano wa noti za rupee 5 tano tu niliyofanikiwa kupata.

5 Zanzibari rupee


zz10.jpg


Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, serikali ya kijerumani ilitoa noti za dharura ambazo zilikuwa ni za karatasi ya kawaida kabisa. Noti hizi zilikuwa katika thamani za Rupie 1, 5, 10, 20, 50 and Rupie 200 ingawa hizi za Rupie 200 zilikuwa adimu sana na sikufanikiwa kupata picha yake

1 Rupie
doa_1rupiene_1.jpg

5 Rupien
doa_5rupiene.jpg

10 Rupien
doa_10rupiene.jpg

20 Rupien

doa_20rupiene.jpg

50 Rupien

doa_50rupiene.jpg

Noti hizi za dharura zilikuwa hafifu sana na wakati mwingine zilikuwa zinafyatuliwa kwa muhuri tu kama hii hapa chini ya Rupie 1.

doa_1rupiene_3.jpg


Inaelekea kuwa mji wa Tabora ulikuwa na umuhimu wa pili kwa dar es salaama wakati wa serikali ya kijerumani kwa vile unaonyeshwa katika Noti zote. Kama mtakumbuka, ile sarafu ya dhahabu ya Rupie 15 ilikuwa inaitwa "Tabora Pound."


.....INAENDELEA
 
Baada ya utawala wa kijerumani kuanguka na nchi kuchukuliwa na waingereza, kwanza nchi ilitumia noti za Rupee za Afrika ya Mashariki na Rupee za Zanzibar ingawa Rupie za kijerumani pia ziliendelea kutumika. Kwa upande wa Zanzibar noti ya rupee 1 ilianzishwa mwaka 1920. baadhi ya noti hizo ni hizi hapa


1 Zanzibari Rupee

zz1.jpg

1 EA Rupee

ea_1rupee.jpg

5 EA Rupee

ea_5rupee.jpg

10 EA Rupee

ea_10rupeeef.jpg

Katikati ya mwaka 1920, serikali ya uingereza ilianzishwa sarafu ya pamoja kwa nchi zote za Afrika ya Mashariki iliyojuliakana kama Florin ya Afrika ya Mashariki. Noti za Florini zilikuwa katika thamani za Florin 1, 5, 10, 20, 50, 100 na Florin 500, ambapo noti za kuanzia Florin 10 na kuendelea juu zilikuwa pia na thamani ya Pound (1, 2, 5, 10 na 50). Kwa vile sarafu hii haikudumu zaidi ya miezi sita, ni noti chache sana zilizotolewa, mifano ya noti hizo ni kama ifuatavyo

1 EA Florin
ea_1florin.jpg

5 EA Florin
ea_5florin.jpg


Mwanzoni mwa mwak 1921, serikali ya kiingereza ilianzisha sarafu ya pamoja afrika mashariki iliyojulikana kama Shillingi ya Afrika ya Mashariki na hivyo kuondokana na Florin ya Afrika Mashariki. Shilingi ya Afrika Mashariki (baadaye nitakuwa naandika kwa kifupi tu kama Shilling) ilikuwa na thamani ya Shillingi 20 kwa pound moja na ilikuwa imeegeshwa kwenye pound kiasi kuwa thamani ya Shilling 20 kwa pound haikubadilika. Noti za Shillingi zilizotolewa wakati huo zilikuwa za thamani za Shillingi 5, 10, 20, 100, 1000, na Shillingi 10,000. Noti za Shillingi ishirini na kuendelea juu zilikuwa pia na thamani ya pound (1, 5, 50). Noti hizi zilikuwa zimeandikwa kwa kiingereza, kiarabu na kiamhara kinachotumika Ethiopia. Katika utawala wote wa kiingereza, kulitolewa mitindo miwili tu ya noti hizo. Mtindo wa kwanza ulidumu kuanzia mwaka 1921 hadi mwaka 1958, ma mtindo wa pili ulidumu kuanzia mwaka 1958 hadi baada ya uhuru mwaka 1964. Sura ya mbele ya noti zote ilikuwa ikionyesha mtawala wa himaya ya uingereza. Sura ya nyuma kwa upande wa noti za mtindo wa kwanza ilikuwa na simba mmoja wa kiume katika eneo la mlima Kenya. Noti zilizotolewa mara ya kwanza wakati wa utawala wa Mfalme George wa tano (1910-1936) ni kama ifuatavyo:

5 EA Shilling
ea_5shsgeorge5.jpg

10 EA Shilling
ea-10shsgeorge5.jpg

20 EA Shilling
ea_20shsgeorge5.jpg


100 EA Shilling
ea_100shsgeorge5.jpg

1000 EA Shilling
ea_1000shsgeorge5.jpg
(Picha hii ilipingwa wakati pesa imeshafutwa rasmi kwa kutobolewa matundu; noti halisi haikuwa na matundu hayo)

Kwa thamani ya shillingi na uchumi wa watu wakati huo, ni noti chache sana zenye thamani ya Shilling 1000 na Shillingi 10,000 ziliingia kwenye mzunguko, na sikufanikiwa kupata noti ya Shilingi 10,000. Kwa hiyo ilipofika mwaka 1933, serikali ikaamua kusimaisha matumiz ya noti za shillingi 1000 ingawa zile za shillingi 10,00 ziliendelea. Wakati wa utawala mfupi wa Mfalme Edward wa nane mwaka 1936, hazikutolewa noti zozote. Noti nyingine zilitolewa wakati wa utawala wa mfame George wa sita (1936-1952), ambapo noti ya Shillingi 1 ilianzishwa. Noti hizo zilikuwa kama ifuatavyo.

1 EA Shilling
ea_1shsgeorge6.jpg

5 EA Shilling
ea_5shsgeorge6.jpg

10 EA Shilling
ea_10shsgeorge6.jpg
[/​

20 EA Shilling
ea_20shsgeorge6.jpg
[/​

100 EA Shilling
ea_100shsgeorge6.jpg
[/​

Kutokana na uhadimu wake, sikuweza kupata noti za Shillingi 10,000. Hata hivyo miaka 11 ndani ya utawala wa mfalme George wa sita, iliamuliwa kufuta noti hizi za Shillingi 10,000 ambazo zilikuwa hazitumiki sana.

Baada ya kifo cha Mfalme George wa sita mwaka 1952 na binti yake Malkia Elizabeth wa pili kuchukua usukani noti zilizotolewa zilikuwa zinafanana na zile zilizokuwapo mwazoni isipokuwa aliondoa noti ya Shillingi 1 kwenye mzunguko.

5 EA Shilling
ea_5shselizabeth2_1.jpg

10 EA Shilling
ea_10shselizabeth2_1.jpg

20 EA Shilling
ea_20shselizabeth2_1.jpg

100 EA Shilling
ea_100shselizabeth2_1.jpg


.... INAENDELEA
 
Hata hivyo mwaka 1958, noti hizo zilitengezwa upya katika mtindo tofauti na zile zilizokuwapo mwanzo. Noti mpya zilikuwa na rangi nyingi huku zikionyesha mazao mbali mbali ya uchumi yaliyokuwapo Afrika ya Mashariki. Noti ya shillingi 5 ilionyesha pamba na karafuu; noti ya shillingi 10 ilionyesha mkonge na chai; noti ya shillingi 20 ilionyesha kahawa na alizeti, na mwisho noti ya shillingi 100 ilionyesha minazi, miwese na pareto. Inaelekea kuwa kuanzia hapo, shillingi ya Afrika mashariki iliacha kubebeshwa kwenye pound kwa vile noti mpya hazikuwa na thamani ya pound tena.


5 EA Shilling
ea_5shselizabeth2_2.jpg

10 EA Shilling
ea_10shselizabeth2_2.jpg

20 EA Shilling
ea_20shselizabeth2_2.jpg

100 EA Shilling
ea_100shselizabeth2_2.jpg


Noti hizi ziliendelea hadi baada ya uhuru ingawa mwaka 1961 zilifanyiwa marekebsihao madogo kwenye sura ya mbele ili kuweza kuonyesha sahihi sita za wajumbe wa bodi ya fedha ya afrika mashariki ambapo wakati huo walikuwa wameongezeka na kuwa sita kutoka watano waliokuwapo mwaka 1958. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo


5 EA Shilling
ea_5shselizabeth_2_3.jpg

10 EA Shilling
ea_10shselizabeth2_3.jpg

20 EA Shilling
ea_20shselizabeth2_3.jpg


100 EA Shilling
ea_100shselizabeth2_3.jpg



Baada ya nchi zote za Afrika ya Mashariki kuwa huru, noti za kwanza zilizotolewa mwaka 1964 zilifanyiwa mabadiliko makubwa sana. Kwanza, noti hizi zilikuwa zimeandikwa katika kiingereza, kiarabu na kishwahili; halafu sura ya mtawala wa uingereza iliondolewa na badala yake kuwekwa mashua. Sikuweza kufahamu mara moja kwa nini waliamua kutumia mashua. Sura za nyuma za noti ziliendelea kuonyesha mazao mbalimbali ya Afrika ya Mashariki ingawa kwa mpangilio tofauti kama inonekanavyo katika picha hizi.


5 EA Shilling
ea_5shs.jpg

10 EA Shilling
ea_10shs.jpg

20 EA Shilling
ea_20shs.jpg

100 EA Shilling
ea_100shs.jpg


..... INAENDELEA
 
Mwishoni mwa mwaka 1985 Nyerere alirudi kijijini kwake Butiama na kuiacha Ikulu mikononi mwa Mwinyi. Noti mpya zilizotolewa mwishoni mwa mwaka 1986 zilikuwa sawa kabisa na zile zilizoacha na Nyerere isipokuwa zilikuwa na sura ya Mwinyi isipokuwa noti zile za Shillingi 100 ambazo ziliendelea kuwa na sura ya Nyerere kama Baba wa Taifa. Vile vile noti mpya ya shillingi 200 ilianzishwa ikiwa inajulika wakati huo kama "double cabin." Nyuma ya noti hizi za Shillingi 200 kulikuwa na wavuvi wanaodhaniwa kuwa walikuwa wa Zanzibar kwa vile kuna karafuu inayoonekana kwa pembeni.

20 Tz Shilling
tz_20shs_mwinyi_1.jpg

50 Tz Shilling
tz_50shs_mwinyi1.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere_3.jpg

200 Tz Shilling
tz_200shs_mwinyi_1.jpg


Ilipofika mwaka 1988, kufuatia kushuka kwa thamani ya shilingi, ilikuwa ni muhimu kuwepo kwa noti zenye thamani kubwa zaidi ili kuwapunguzia watu mzigo wa pesa. Hivyo benki kuu ikaanzisha noti mpya za shillingi 500, ambao zilijulikana kama "Pajero." Noti hizi za shillingi 500 zilikuwa na sura tofauti kabisa na zile nyingine. Nembo ya Taifa ilikuwa ya rangi, halafu zilikuwa na nembo ya waziwazi ya Benki Kuu ya Tanzania. Nyuma yake zilionyesha akina mama wakivuna zao la kahawa au karafuu, sikumbuki tafsri ya picha hiyo vizuri.


500 Tz Shilling
tz_500shs_mwinyi_1.jpg

Kasi ya kupungua kwa thamani ya shilingi ilikuwa kali sana kiasi kuwa miaka miwili baadaye, Benki Kuu ililazimika kuingiza noti mpya ya Shillingi 1000 ambayo ilikuwa na sura kama ile ya Shillingi 500 isipokuwa ngao ya taifa haikuwa ya rangi. Vile vile ilikuwa na maandishi ya ndani kwa ndani kuonyesha 1000. Nyuma yake kulikuwa kiwanda cha nyama cha Tanganyika packers cha pale Kawe.

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mwinyi_1.jpg

Noti zetu wakati huo zilikuwa pana sana na zilikuwa zinaongezeka upana kadiri thamani yake inavyopanda. Ilipofika mwaka 1992, Benki kuu ilifanya mabadiliko makubwa katika noti zetu. Kwanza zilipunguzwa sana upana halafu zote zikatengezwa upya kuwa na sura inayofanana. Noti ya shillingi 20 iliachisHwa na badala yake zikaongezwa noti mbili za Shillingi 5,000 na Shillingi 10,000 kama ifuatavyo:


50 Tz Shilling

tz_50shs_mwinyi2.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_mwinyi_2.jpg

200 Tz Shilling
tz_200shs_mwinyi_2.jpg

500 Tz Shilling
tz_500shs_mwinyi_2.jpg

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mwinyi_2.jpg

5000 Tz Shilling
tz_5000shs_mwinyi_2.jpg

10000 Tz Shilling
tz_10000shs_mwinyi_2.jpg


Noti hizi ziliendelea kutumiwa hadi mwisho wa utawala wa Mwinyi mwaka 1995.

......INAENDELEA
 
Baada ya kuvunjwa kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika ya Mashariki na kuundwa kwa benki kuu za Tanzania, Kenya na Uganda mwaka 1966, Benki Kuu ya Tanzania ilitoa noti za kwanza zenye thamani hizo hizo za Shillingi 5, 10, 20 and Shillingi 100. Upande wa mbele wa noti hizi kulikuwa na sura ya Mwalimu Nyerere wakati wa kupata uhuru, na upende wa nyuma ulionyesha mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania. Noti ya Shillingi 5 ilikuwa na mlima Kilimanjaro, noti ya shilingi 10 ilikuwa na shamba la mkonge, wakati noti ya shilingi 20 ilikuwa inaonyesha mgodi wa almasi wa Mwadui. Noti ya shillingi mia moja ilikuwa inaonyesha morani wa kimasai akichunga ng'ombe wake.

5 Tz Shilling
tz_5shs_nyerere1.jpg

10 Tz Shilling
tz_10shs_nyerere1.jpg


20 Tz Shilling
tz_20shs_nyerere1.jpg


100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere1_v1.jpg

Kwa waliotumia noti hizo wanakumbuka kuwa noti ya shilingi kumi ilikuwa inajulikana pia kama jani la katani, wakati ile ya 100 ilikuwa inajulikana pia kama Masai au Pink kutokana na rangi yake. Kwa muda mrefu noti ya shilingi ishirini imeendelea kujulikana kama paund au "mbao" kutokana na historia kuwa mwanzoni ilikuwa ina thamani ya Pound 1.

Hata hivyo sura ya masai kwenye noti ilileta mjadala kidogo kiasi kuwa benki kuu iliamua kuzibadilisha. Ilipofika mwaka 1969, wakatoA noti za shillingi 100 ambazo zilikuwa na wanyama katika mbuga ya serengeti kama ionekanavyo hapa chini

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere1_v2.jpg


Noti hizi ziliendelea kutumika hadi mwaka 1978 zilipofanyiwa mabadiliko makubwa hasa ili kuondoa sura ya kitoto ya Nyerere na kuweka picha ya Nyerere akiwa mtu mzima. Noti mpya zote zilikuwa zimendikwa kwa kishwahili tu, na vile vile noti ya shillingi tano ilisimamishwa. Upande wa nyuma wa noti zote kulikuwa na ramani ya Tanzania pamoja na sura mbalimbali zihusuzo Tanzania. Noti ya shillingi 10 ulikuwa na mlima Kilimanjaro, kinyago cha kimakonde na mnara wa Azimio la Arusha; noti ya shillingi ishirini 20 ilikuwa na kiwanda cha nguo kuashiria kuwa nchi ilikuwa inasonga mbele kiviwanda, na ile noti ya shillingi 100 ilikuwa tasisi za elimu kuanzia shule za msingi na vyuo vikuu kuashiria juhudi za nchi kupambana na adui ujinga. Vile vile shughuli za elimu ya kujitegemea zimeonyeshwa kwa wanafunzi kulima kwa jembe la mkono!!

10 Tz Shilling
tz_10shs_nyerere_2.jpg

20 Tz Shilling
tz_20shs_nyerere2.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere_2.jpg

Miaka saba baadaye, mwaka 1985 (muda mfupi sana kabla Nyerere hajastaafu) noti zilifanyiwa mabadiliko tena kwa kuondoa noti ya shillingi 10 na kuwekwa kwa noti ya shillingi 50. Noti hizi zilikuwa na sura ya Nyerere akiwa ameanza kuzeeka, na zilitumia rangi nyingi sana kuliko zilizotangulia. Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958, noti ya shillingi mia moja ilibadilishwa rangi kutoka "pink" na kuwa ya bluu. Noti ya shilingi ishirini ilionyesha shughuli mbalimbali za baadhi ya viwanda vyetu, wakati shilingi 50 ilionyesha shughuli za kujitolea kujenga mashule. Noti ya shillingi 100 ilionyesha wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaama na baadhi ya majengo ya chuo hico. Nadhani ilikuwa pia kuonyesha kuwa nchi imepiga hatua katika upande wa elimu ya juu.


20 Tz Shilling
tz_20shs_nyerere3.jpg

50 Tz Shilling
tz_50shs_nyerere.jpg

100 Tz Shilling
tz_100shs_nyerere_3.jpg



.... INAENDELEA
 
Wakati Mkapa alipochukua usukani wa kuongoza nchi, aliamua kusitisha matumizi ya sura za viongozi kwenye noti. Kwa hiyo noti zote zilizotolewa mwaka 1997 chini ya utawala wake hazikuwa na sura ya kiongozi yeyote. Badala yake zilikuwa na kichwa cha Twiga ambaye ni kihistoria ndiye mnyama wa taifa. Wakati huo pia, noti za shillingi 50, 100 na shillingi 200 zilisimamishwa.

500 Tz Shilling
tz_500shs_mkapa_1.jpg

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mkapa_1.jpg

5000 Tz Shilling
tz_5000shs_mkapa_1.jpg

10000 Tz Shilling
tz_10000shs_mkapa_1.jpg

Hata hivyo baada ya kifo cha Mwalimu Nyerere mwaka 1999, iliamuliwa kuwa sura yake iwe ya kudumu kwenye noti ya Shillingi 1000, hivyo noti hiyo ilisanifiwa upya na kuwa kama ifuatavyo

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mkapa_1_-v2.jpg


Noti hizi ziliendelea kutumika hadi mwaka 2003 zilipofanyiwa mabadiliko ya kuongeza usalama zaidi. Vile vile kutokana na manunguniko ya kichinichini kutokea zanzibar kuhusiana na mtumizi ya Twiga ambaye alikuwa mnyama wa Tanganyika, iliamuliwa kutotumia twiga tena. Badala yake sura za wanyama wakubwa mbalimbali wa Tanzania zilitumika ingawa sura ya Nyerere iliendelea kubaki kwenye noti za Shillingi 1000. Vile vile noti mpya ya Shillingi 2000 ilianzishwa. Upande wa nyuma wa noti hizi ulionyesha shughuli mbalimbali za uchumi, sehemu za kihistoria na harakati za kukuza elimu . Kwa mara nyingine tena kuanzia mwaka 1978, noti hizi ziliandikwa kwa Kiingereza na Kishwahili tena. Noti hizi ndizo zinazotumika hadi leo, sura zake ni kama ifuatavyo

500 Tz Shilling
tz_500shs_mkapa_2.jpg

1000 Tz Shilling
tz_1000shs_mkapa_2.jpg

2000 Tz Shilling
tz_2000shs_mkapa.jpg

5000 Tz Shilling
tz_5000shs_mkapa_2.jpg

10000 Tz Shilling
tz_10000shs_mkapa_2.jpg



TAMATI
 
Kichuguu tutajie umri wako maana haya mambo unayotupa ni zamani za kale ambapo wengi wetu tulikuwa bado matumboni mwa bibi zetu i mean kabla mama zetu hawajazaliwa... lol


Huoni hilo jina amekula chumvi nyingi. (Kichuguu kinavyoonekana)
 
Kichuguu

Unakumbuka nilikuuliza kuhusu hizi noti hata Benki kuu hawana takwimu sahihi inabidi waje hapa kuchota kumbukumbu. Nchi yetu inatia kinyaa.

Dua,

Nilipokuwa nafanya utafiti wangu huu, niligundua kuwa Benki kuu hatunzi rekodi za sarafu yetu vizuri, hasa kwenye internet. Inawezekana wana rekodi nzuri kwenye mafaili lakini hawajazieweka kwenye internet kwa faida ya watu wote.
 
mzee kichuguu nashukuru sana kwa darasa hili. umenifanya kujua sehemu ya historia ambayo sikufikiri ningeijua. nilikuwa nadhani kufahamu fedha is not that important but now i find it very interesting.mzee umenifanya nitake kujua karibu mengi ya wakati wanyuma. zingine zimenikumbusha utoto wangu!lol! ila one thing for sure kipindi hicho pesa yetu ilikuwa inanguvu sana sio kama leo inapo itwa madafu.chukua tano kaka
 
Sio madafu tu hata wachuuzi wanaona taabu kutrade nayo...
nenda maduka ya wahindi town utakuwa mijidola ktk price lists... hata majibu ya magembe bungeni anapotaja fedha... anaona aibu kutumia shilingi yetu kama kigezo....

Nimechokoza...
 
Back
Top Bottom