Historia ya kweli ya maisha ya Sheik Ponda na Fareed ni muhimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LINCOLINMTZA, Oct 21, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wana JFs,
  Hawa watu wameleta gumzo katika nchi yetu kwa siku za hivi karibuni. Naomba mwenye taarifa za hawa watu azirushe hapa ili tuyajue maisha yao. Mahali alipozaliwa, aliposoma, na mafunzo yoyote aliyopata.

  Nawakilisha
   
 2. mgomba101

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 38
  Ponda alikuwa muuza kahawa pale magomeni mwembechai kabla ya kuwa mwanaharakati wa kiislam.
   
 3. morenja

  morenja JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,443
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 38
  nikweli ni muhimu sana kuwajua .
   
 4. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi hata kutafuta historia yao naona kichefuchefu
   
 5. m

  mukandarasi JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 648
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 18
  Kuna haja ya kujua katokea wapi au upande gani wa Jamhuri yetu,sababu kumekuwa na uvumi tuu kuwa si raia!Hii imekuwa kawida yetu siku hizi mtu akikuudhi basi siyo raia.Japo kwa muda mrefu umekuwa unakunywa nae kahawa.Mfano Kinana aliwahi kukutana na kadhia hiyo alipotaka kugombea ubunge na Makongoro jimbo la arusha wakati alikwisha kuwa waziri wa ulinzi nchi hii,pia usisahau Ulimwengu kilichompata wakati alikwisha kuwa DC.Sasa kwanini Wasomali wamekuwa wakikamatwa na Sh'Ponda kutokamatwa siku zote wakati Uvumi ulikuwepo kuwa jamaa si raia? Kwakusisitiza hilo sina maana ya kumtetea Ponda kwani hata mimi naona mambo anayofanya hayapo katika sifa za watanzania,bali na washangaa jamaa tuliowakasimu madaraka!! Kujifanya mabingwa wa kutibu na kuponya kuliko kutafuta kinga.
   
 6. Kyenju

  Kyenju JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 4,280
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 38
  Chanzo cha chabari hizi kinaanza kwa kueleza kuwa, imebainika kuwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Issa Ponda si raia wa Tanzania.

  Uchunguzi uliofanywa na chanzo hiki nchini Burundi, Kigoma na taarifa za uhakika kutoka idara ya Uhamiaji na vyombo mbali mbali vya dola umebaini kuwababa yake Ponda mzee Issa Ponda alizaliwa mwaka 1921, na kuishi eneo la Rumonge barabara ya 6, nyumba namba 31, Bujumbura nchini Burundi, na kuhamia nchini mwaka 1957.

  Mzee Issa Ponda alifikia ujiji, kwenye mji wa Ball (hivi sasa Kawawa) na kupokewa na mtanzania abaye baadaye alikuja kuwa mjomba wake Ponda anayeitwa Iddy Matata. Mara baada ya kahamia kwenye mji huo na kupewa kiwanja na mzee Matata mzee Issa ndipo alipomuoa Mariam Ally Kassa (huyu ndiye mama wa Shehe Issa Ponda) na alimzaa Shehe Ponda Mwaka 1958.
  Taarifa za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa, mzee Ponda baada ya kuoa na kupata mtoto, alianza kutafuta namna ya kuzoeleka kwenye eneo alilokuwa anaishi ili aonekane ni mzaliwa wa Tanzania na alifanikiwa kwa hilo hadi akagombea udiwani uliodumu kuanzia mwaka 1964 hadi 1965.
  Taarifa za uhamiaji zinaonyesha kuwa, Ponda ambaye alipata elimu yake ya msingi Kigoma na kuishia darasa la saba, hakuwai kuukana uraia wake kama sheria ya uhamiaji inavyoelekeza, kwa hiyo bado anatambulika kama raia wa Burundi.
  Hata hivyo Sheikh Ponda kwa kutumia njia anazozijua (njia za panya), mwaka 1995 alpohamia njini Dar es salaam akitokea Kigoma alikuwa anafanya biashara, alaipata hati ya kusafiria namba A0143978 (nakala chanzo cha habari kinayo) iliyotolewa Juni mwaka 1995 kwa jina la Pondamali Issa Pondamali ambayo ilitakiwa kuisha 21, June mwaka 2000, ingawa aliongezewa muda hadi 2005, na inaonyesha anuani yake ya posta ni 21842 Kigoma namba ya simu ni 21842.

  Sheikh Ponda aliamia Dar es salaam baada ya tukio la kupigwa risasi mguuni na polisi wakati akisafirisha magendo ziwa Tanganyika kati ya Tanzania na Burundi, ambapo duru za kiusalama zinaonyesha kuwa, alipelekwa kwa gari hadi Mwanza na kisha kwa ndege mpaka jijini Dar es salaam na kuojiwa na aliyekuwa afisa upelelezi pamoja na aliyekuwa mkuu wa usalama wa taifa wakati huo Haidery Zuberi kabla ya kuachiwa (Ponda).
  Sheikh Ponda pia amewahi kuhusishwa na uuzaji wa madawa yaliyokwisha muda wake na mara kadhaa amekamatwa akijaribu kuyavusha kuelekea nchi jirani.

  Sheikh na kundi lake ni wanasadikika kutumiwa na vyama fulani vya kisiasa ili kuanzisha vurugu na uvunjifu wa amani nchini, Sheikh Ponda pamoja na wenzake walikutana 7, Septemba kwenye msikiti wa kichangani (TIC), Magomeni Mpipa jijini Dar es salaam na 8, septemba kwenye msikiti wa Mtambani Kinondoni na kupanga namna ya kufanikisha vurugu hizo, pamoja na mkakati wa kumung'oa Mufti wa Tanzania Sheikh mkuu Shabani Bin Simba.
  Wanaomfahamu vizuri Ponda wameishauri idara ya uhamiaji kumrudisha kwao Burundi kwa kuwa ni kinara wa vurugu na uvunjifu wa amani hapa nchini.


  Chanzo cha habari ni gazeti la Afrika leo la Jumatano Septemba 12-18, 2012 Toleo namba 60.


  Katika gazeti la Kiislamu la safina la tarehe 7, Septemba 2012 toleo namba 25, lineeleza kuwa Ponda analo genge linalomfadhili limempa ponda hadhi ya usheikh licha ya kujua kuwa hastihili kuwa sheikh.

  Nanukuu: Gazeti moja linalojiweka mbele katika kudai haki za waislamu limekuwa likiandika habari zake si kwa kuwasilina naye bali kwa kupitia kumbukumbu za zamani tu.
  Katika kuhakikisha malengo yao yanafanikiwa genge hili limempa Ponda, hadhi ya Sheikh wa kiislamu licha ya kujua fika kwamba Ponda si sheikh hana elimu ya dini inayompa hadhi hiyo. Baadhi ya watu wanadai sheikh huyu hajamaliza hata juzuu 30 zinzzokamilisha msahafu wa qu'raan licha ya kutojua masomo mengine yanayomfanya mtu afikie kiwango cha usheikh, kama Figh na kadhalika.

  Mwisho wa kunukuu.

  Tuangalie kwa ufupi mtu anayeitwa Farid Had

  Farid Had ni kiongozi wa kikundi cha uhamsho au genge la vurugu na machafuko Zanzibar ambalo wengi wa wafuasi wake ni watu kutoka Pemba wenye kuutukuza uarabu. Ni mtu anayemwataka Wazanzibar wjiondoe kwenye muungano. Lakini wazanzibar wanafikiri ni mwenzao kumbe sivyo. Farid Had ana uraia wa mchi mbili, kinyume na katiba ya nchi yetu.
  Yupo mtu aliyesema aliwahi kukutana na Farid kwenye mkusanyiko mmoja wa wanadini wa kiislamu nchini Mauritania akiwa anawakilisha si Zanzibar wala Tanzania, bali aliwakilisha nchi ya Oman. Hakuna anayejua mtanzania aliwezaje kupata nafasi ya kuwakilisha Oman nje ya nchi yake lakini hayo yanasemwa na sina shaka kama hayapo yanakuja, maana pafukapo moshi usikanyage moto upo.

  Huyo ndiye bwana Farid Had.
   
 7. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,466
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  duuuuuh
   
 8. j

  jakamoyo JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 240
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  viwanda vya uongo vinafanya kazi, kwanini wasipeleke taarifa uhamiaji?
  Hayo ni magazeti uchwara, habari haziko balanced, hazijawahoji wahusika wakiri au kukanusha wanayo tuhumiwa nayo.
   
 9. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uzushi kila siku uzushi tu, hivi unafahamu Historia ya
  Raisi wako wa awamu ya Tatu? Je yule Mzanaki!
   
 10. Porsha

  Porsha New Member

  #10
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 1
  Scary!! Everything is so obvious though
   
 11. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Narudia tena kauli yangu ya hapo nyuma kwamba ingawa vurugu za mbagala na kwingineko zilifanywa na waislam, lakini ieleweke kwamba hizi hazikua vurugu za kidini, bado naamini kwamba watanzania tunapendana bila kujali dini zetu.

  Kuhusu mambo za Zanzibar kwakweli sina uhakika wa nini kinaendelea ila hiyo point ya waislam kutoka Pemba ndio nina mashaka nayo, hivi inawezekana kweli hayo yatokee unguja tu pemba ibaki tulivu, wakati wengi wa wahusika ni kutoka pemba! may be I do not know!! kila kundi hapo lina lengo lake, wengine wanafuata upepo tu!!
   
 12. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 7,494
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 63
  Subiri kuche huku tanzania uone wadau watakavyo changia kwa jazba
   
 13. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama mpaka mtu akane uraia wake tutajikuta out of 46 million people 10 million only are TZns !!! jifanye tu myanja oune teh teh.....
   
 14. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 3,095
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 38
  ndio manaaaa???
   
 15. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 826
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa taarifa.
   
 16. Kocha

  Kocha JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 2, 2008
  Messages: 356
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 18
  Duh! Kumbe Ponda ni darasa la saba!!Ndio maana ufahamu wake ni mdogo
   
 17. k

  kigoda JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2012
  Messages: 1,785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hilo gaidi hilo ukute nalo lilihusika kuchoma baloz za Tanzania na Kenya.
   
 18. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,490
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 48
  Farid anataka babu zake warudi, na watarudi tu kwa jinsi nilivyoaona washikaji wanashangaa kasri vile, watamuita aje AWEKEZE kwenye makasri!
   
 19. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 18
  Japo kwa sasa wengi wa wafuasi wake wanaweza wasielewe sana, ila ni vema hawa "mafilauni"siri zao na njama zao juu ya Tanzania zikawekwa wazi naamin watanzania ni waelewa sana wataelewa kuwa hawana lolote jema juu ya Tanzania yetu na kuwapuuza!
   
 20. Black Bat

  Black Bat JF-Expert Member

  #20
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,916
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 38
  huyu katumwa na suktan wa Oman
   
 21. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #21
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 38
  Msumari huo unachoma,utawataja mbaka wakoroni!
   
 22. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #22
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 7,248
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 48
  Dawa yao ndogo, ni km yule Sheikh wa Mombasa anapewa k2 chenye ncha kali au sindano maana hizi Elimu za kuishia Std7 na kung'ang'ania Elimu ahera kz kwelikweli
   
 23. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #23
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suala la uraia sio tija kabisa.Kuna raia wengi wageni Tanzania na wanafanyakazi na wengine wanaishi kinyemela.Hata wewe mtoa mada ukichunguzwa sana utakuta unatokea nje ya mipaka ya Tanzania.HOJA kubwa hapo ni kuwadhibiti wahuni na wavunja amani wote na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria bila kujali umetumwa na wanasiasa, unauraia wa nje, una elilimu au la , una ushehe au uchungaji.Serikali ionyeshe makucha yake kwa kutumia vyombo vyake vyote bila kujali historia ya mtu.
   
 24. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #24
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,964
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 48
  ....Ooh, Ok.

  Ndio kusema 1958 alizaliwa Tanganyika ......tena kabla ya uhuru wa 1961, na kabla ya muungano wa 1964 uliozaa nchi ya Tanzania?
   
 25. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #25
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,781
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kyenju huna lolote fitina mkubwa wewe mpandikaza chuki unaesukumwa na udini.

  Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 26. Mr.mzumbe

  Mr.mzumbe JF-Expert Member

  #26
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 16
  Hiimijitu inakuw kama miskule fulani hivi....!!!!kama ponda ndio chanzo cha vurugu,sasa kawanini wanpiga kelele pale watu wanaposema chadema ifutwe????ponda anadai haki za waislam kama inavyojitambulisha chadema.Waislam na wenyewe wameona kweli kuna haja ya kuwa karibu na ponda na kushirikiana nao kwenye kudai haki zao...ndio maana watu mamia kwa maelfu wanamkubali ponda.Haya majitu yanayoitwa wa kristo ni watu waahajabu sana...mbona hata siku moja hawajawahi kukemea maandamano ya cdm,ndio kwanza wanawapa support!!!!
  MAPINDUZI AU UKOMBOZI si lazima kiongozi ni muhusika wa taifa uhusika,ndio maana hata znz J.OKELLO aliongoza mapinduzi,hata nyerere alisababisha watu wetu wengi sana kufa kwa ajili ya kujitolewa tolea hovyo kwenye mapinduzi ya nchi za kiafrika.ISHU siyo ponda ishu ni madai ya ponda.
   
 27. isambe

  isambe JF-Expert Member

  #27
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 1,109
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 63
  tukienda deep tutakuta hakuna aliye mtanzania halisi,kuanzia wewe mleta mada na sisi wachangiaji,hilo la uraia wa mtu tusliulize hapa ,hoja hapa huyu mtu ni menace to society,hatufai.kuhusu Farid naona umeme ulikatika wakati mleta mada alipo kuwa akikariri data zake,namshauri asiogope avuke bahari aende Zenji Mitaani akahoji watu wampe data za Farid,hapo ndipo tutaona ukomavu wake wa habari.
   
 28. Revolution

  Revolution JF-Expert Member

  #28
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe wakati tukiwa ziarani Oman kujikomba na kuchungulia akaunti zetu kuna waoman wengine waliojivalisha utanzania wanaleta vurugu huku nyumbani....salaaaleh!!!!
   
 29. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #29
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,011
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 38
  tusitafute njia rahisi ya kutatua matatizo kwa kutafuta nani ni raia na nani si raia,tuna historia ya watu kutuhumiwa kuwa si raia na mwisho wa siku tuhuma hizo zikaonekana zilikuwa na malengo furani
  tutatue matizo yetu pasi ya kupandikiza chuki za nani si raia na nani si raia,sheria ifuate mkondo wake kwa kupambana na raia wenye makosa na si kutafuta visingizio vya aina yeyote ile
  kwa jinsi nilivyosoma hapo juu,bado shehe ponda ni raia wa tanzania tena wakuzaliwa na wala si kuomba,maana kama mwandishi alivyosema kuwa alizaliwa tanzania wakati mama yake na baba yake wakiwa tanzania na tena mmoja wa mzazi wake ni mtanzania,bado sifa ya yeye kuwa ni mtanzania ipo palepale labda kama iwe alizaliwa burundi na baadae kukulia tanzania hapo ni story nyingine tena.
   
 30. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #30
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,774
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Lisemwalo lipo na kama halipo baaasi bilashaka laja!!- Ila mkuu hapo kwenye red vipi??? mbona pamekaa kimashaka mashaka ( hizo figure ni za anuani au number ya simu??)

   
Thread Status:
Not open for further replies.

Share This Page