Historia Ya KARL MARX

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Ndugu zangu wanaJukwaa La Historia nianze kwa kupongeza juhudi tukufu za mheshimiwa Kichuguu kwa kuanzisha hoja ya kuundwa kwa jukwaa hili na wale wote waliochangia na kuunga mkono hoja (siwezi kutaja wote kwasababu hili sio jukwaa la kutajana majina)

Leo kwa kuanzia au kupasha misuli ningependa nitoe historia fupi ya bwana Karl Marx baba wa Scientific Socialism,

Karl Marx alizaliwa mwaka 1818 huko Trier Prussia ambayo ni Ujerumani kwa sasa (kama nimekosea naomba marekebisho). Baba yake ni Myahudi ambaye alibadiri imani yake na kuamini katika Ukristu,

Marx alisoma katika vyuo vya Bonn na Berlin akiwa ameegemea zaidi kusomea History (historia), Philosophy(falsafa), Jurisprudence (sijajua kiswahili inaitwaje) na Political Economy (siasa ya uchumi).

Baadae Marx alienda Paris Ufaransa huko ndiko alikokutana na mwana Ujamaa mwingine Friedrich Engels ambaye nadhani aliishi tangu mwaka 1820-95 (kama siko sahihi nitaomba maoni).

Mwaka 1847 aliombwa kuandaa Manifesto ya German Communist League In Paris ndipo mwaka 1848 alifanikiwa kuandaa vitabu viwili 1- Communist Manifesto na 2-Das Kapital. Kwa upande wangu nimewahi kusoma kitabu cha Communist Manifesto japo kwa ufupi humo ndani jamaa ametoa theory nyingi sana kuhusu matatizo ya wafanyakazi kupitia hicho kitabu utapata suluhu ya migomo ya madaktari na waalimu hapa nchini, mfano kuna sehemu anasema "Wakulima na wafanyakazi wanauwezo wa kuliondoa tabaka tawala" kama haliwaridhi.

Vitabu hivyo vilisaidia sana kufanikisha mapinduzi ya Urusi 1917 (nitasimulia siku nyingine), mapinduzi ya Ufaransa 1879 (pia nitasimulia muda upo wakuu) na mapinduzi ya mwaka 1848 yaliyotokea sehemu nyingi ulaya.

Nimeshindwa kuelezea kifo chake kwa kuwa sijapata chanzo na mwaka (Kama kuna mdau anajua ni vema akatiririka hapa).
Ndugu zangu wanaJF nimeamua kutoa utangulizi huu kwasababu Karl Marx ni chanzo cha historia nyingi hapa ulimwenguni.

Ahsanteni sana
Source: Kitabu cha "A History Of Modern Times" by C.D.M KETELBEY.
Nilikinunua 1000 kwa wale wanaomwaga chini najua haiwahusu lakini nilitaka kuwasihi msivizarau vile vitabu vina mengi.
 
Last edited by a moderator:
.........................
Mwaka 1847 aliombwa kuandaa Manifesto ya German Communist League In Paris ndipo mwaka 1848 alifanikiwa kuandaa vitabu viwili 1- Communist Manifesto na 2-Das Kapital. Kwa upande wangu nimewahi kusoma kitabu cha Communist Manifesto japo kwa ufupi humo ndani jamaa ametoa theory nyingi sana kuhusu matatizo ya wafanyakazi kupitia hicho kitabu utapata suluhu ya migomo ya madaktari na waalimu hapa nchini, mfano kuna sehemu anasema "Wakulima na wafanyakazi wanauwezo wa kuliondoa tabaka tawala" kama haliwaridhi.

Vitabu vyake hivyo vinapatikana bure Google- books; nimeweka kimoja hapa kwa anayetaka kukipitia. Nitaleta kingine baadaye nikishanikiwa kupunguza ukubwa wa faili. Vitabu hivi vilikuwa ni sehemu ya DS100 UDSM miaka ya themanini.
 

Attachments

  • CommunistManifesto.pdf
    2.1 MB · Views: 328
Pia kama mna picha za zamani za kihistoria mziweke na humu! Enzi hizo posta hakuna lami.
 
Ndio maana hapa JF hukosi kitu..kiukweli moja ya vitu mhimu sana siku hizi mbali na pahala pa kuishi nadhani JF iongezwe kwenye mahitaji mhimu ya binadamu hasa mtz
 
ahsante sana kwa historia hii. kwa sisi wapenda historia umezidi kutukuna
 
Nilisoma sana hiyo philosophy ya communism kwa kina sana wakati wa DS100 tukiianzia kwenye kilichoitwa Hegelian Philosophy na kumalizia na kile kilichotitwa the Crisis of Capitalism.

Kwa maneno, ni kweli Communism ilikuwa inonekana kuwa ni utaratibu mzuri sana na wenye malengo mema kwa watu wote, lakini nadhani kuwa ilikuwa short sighted sana kwa kusahahu laws of nature hasa Survival of the Fittest na The Pyramid of the Human Needs; kwani mfumo huo ulikuwa unaondoa kabisa zile checks and balances zinazotakiwa ili kuneutralize negative effects za hizo laws of nature. Nchi zote zilizofuata Ukomunist kama ulivyohubiriwa na Karl Max, pamoja na rafiki zake Friedrich Engels, na Vladmir Lennin zilishindwa kuendelea hadi pale walipoamua kuingiza capitalism kwa kiasi fulani.

On the other side, nchi zenye mchanganyiko wa mfumo wa ukomunist na mfumo wa ubepari zimekuwa zinafanya vizuri zaidi ya zile za ubepari pure.

Katika maandiko ya Marx, nadhani niliipenda sana ile phrase ya "Dictatorship of the Proletariat"
 

Attachments

  • Kapital.pdf
    18.5 MB · Views: 157
Kichuguu kweli kabisa Communism as the highest stage of socialism ilirudisha nyuma maendeleo ya nchi nyingi hasa kipindi cha cold war kati ya socialism na capitalism, vilevile me naona hakuna tofauti ya Socialism na dictatorship kama mtakumbuka historia ya utawala wa Joseph Stalin kwenye jumuia USSR (nitakuja kumchambua siku nyingine) ulikua ni wa kimabavu sana.
 
Last edited by a moderator:
Kichuguu kweli kabisa Communism as the highest stage of socialism ilirudisha nyuma maendeleo ya nchi nyingi hasa kipindi cha cold war kati ya socialism na capitalism, vilevile me naona hakuna tofauti ya Socialism na dictatorship kama mtakumbuka historia ya utawala wa Joseph Stalin kwenye jumuia USSR (nitakuja kumchambua siku nyingine) ulikua ni wa kimabavu sana.
 
Last edited by a moderator:
mkuu nakupongeza sana kwa kuanzisha thread iliyojaa elimu ya historia ya ulimwengu
 
Mkuu, nimeipenda topic yako, asante kwa kuelimishana. Napongeza Jf kwa kuanzisha jukwaa hili. Big up! Ila naona kama lingejitegemea, au lingekuwa kwenye Elimu maana historia sio siasa.
 
Nakumbuka kidogo theory of surplus value na mambo fulani fulani..long time.. ila mwalimu wangu aliniambia eti alikufa kwa kipindupindu!! Na sikumbuki kama nilimuuliza je wakai huo kilikuwepo?
 
Wakuu hv tofauti ya capitalism na socialism kulingana na mtazamo wa Karl Marx,pia V Lenin alikua na mtazamo sawa na Karl Marx kuhusu ujamaa(socialism)?Je Nyerere alipotangaza azimio la Arusha(1967)alifuata sera ya ujamaa ya Karl Marx au V Lenin? Wakuu mwenye kufahamu zaidi msaada kunielewesha,JF kweli ni kisima cha wanazuoni waliokomaa
 
Alikuwa kichwa mwenye vituko sanaa

1. Check na exile life yake mpaka anakufa..... if my memory sails me correct was due to cholera.
2. Kuna kitendawili kati yake na Engels nani aliandika na nani ali-publish?????
 
Nakumbuka kidogo theory of surplus value na mambo fulani fulani..long time.. ila mwalimu wangu aliniambia eti alikufa kwa kipindupindu!! Na sikumbuki kama nilimuuliza je wakai huo kilikuwepo?

The value theory.......exchange versus use value.....the price tag phenomenon

The misery and poverty are the core sources of devastating diseases like Cholera and Marx lived the poverty at its apex.....he surely died of Cholera

Contextualization; Umewahi kusikia kipindupindu Oysterbay au Masaki????
 
Wakuu hv tofauti ya capitalism na socialism kulingana na mtazamo wa Karl Marx,pia V Lenin alikua na mtazamo sawa na Karl Marx kuhusu ujamaa(socialism)?Je Nyerere alipotangaza azimio la Arusha(1967)alifuata sera ya ujamaa ya Karl Marx au V Lenin? Wakuu mwenye kufahamu zaidi msaada kunielewesha,JF kweli ni kisima cha
wanazuoni waliokomaa

1. I see them as two sides of the same coin only with a major difference when it comes to sharing the product of labour; it is widely shared in socialism...there is a clear trickle down effect when it comes to sharing of the benefits among the majority....N.B; A lot of philosophical acrobats are employed here

2. WHILE in the Capitalism just few appropriates the product from the majority laborious production in return of a wedge......now a days called salary

But; In all systems classes are there with a far less contradictions and conflicts in the Socialism side of the coin........

3. Class, conflicts and contradictions are inherent features of any society being capitalistic or socialistic



AZIMIO; I can say it was more of a copy and paste of strategies from the Socialistic countries than the mastering of PHILOSOPHICAL background guiding the system.....we lacked this compass....together with a hesitant will among the technocrats. Same goes with MKUKUTA....MKURABITA and the likes....with the same system but a big difference in context expect a halt.... I think Azimio neither was sort of Stalinist nor Marxism

Ukipata muda soma the Consciencism; By Kwame Nkrumah tunaweza kupata muono kwa nini falsafa ya Ujamaa haiwezi kuwa copy and paste story......falsafa itasimama daima ila ili kuwa na mafanikio historia, siasa na uchumi wa sehemu husika ni lazima kuangaliwa kwa upekee na sio kama ilivyofanyika somewhere else...... were these adressed in the pre-umble of Ujamaa na Kujitegemea under the label ya AZIMIO????? It was reified before its existence


I stand to be corrected
 
Wakuu hv tofauti ya capitalism na socialism kulingana na mtazamo wa Karl Marx,pia V Lenin alikua na mtazamo sawa na Karl Marx kuhusu ujamaa(socialism)?Je Nyerere alipotangaza azimio la Arusha(1967)alifuata sera ya ujamaa ya Karl Marx au V Lenin? Wakuu mwenye kufahamu zaidi msaada kunielewesha,JF kweli ni kisima cha wanazuoni waliokomaa
sina uhakika sana lakini niliwahi kusikia mtu mmoja akisema kuwa Karl Marks alipata PhD katika umri wa miaka 21!
Nimewahi kusoma vitabu vyake lakini wakati huo sikuwa naelewa vizuri juu ya ubepari (capitalism) maana tulishafundishwa kuwa ni mfumo usiotakiwa hata kusikiliza habari zake kutokana na 'udhalimu' wake. Sema tu madogo walipoteza vitabu vyangu lakini itabidi kuvitafuta upya. Kulikuwa na kitabu kingine cha Renee Dumont kinaitwa 'Afrika Inakwenda Kombo' nacho kilitoa facts nyingi za juu ya mifumo ya utawala Afrika na Mwalimu jinsi alivyoamua kubalance kati ya uchumi wa Ubepari (Magharibi) na Ukomunisti (Mashariki).

Lakini hoja yako hapo wanasema kuwa (bila shaka tutapata jibu hapa jf) Karl Marks alidevelop hizo theory na kuziandika vizuri sana kama mleta uzi alivyosema. Lakini kuhusu implementations hakuweka sawa ni muda gani bali alisema mazingira ndiyo yange-determine. Sasa Lenin ndio akaja na hoja kuwa wasingeweza kuendelea kusubiri wakati 'ukweli' juu ya mfumo wa utawala umeshawekwa wazi na hapo ndipo wakaamua kufanya 'force implementation' yaani MAPINDUZI!
Sasa matokeo yake baadhi yetu tunaweza kupima. Ulaya Mashariki walirukia hizo theory na leo tunawaona; Russia tunaiona; Cuba tunawaona; CHINA 'wali-customize' zile theory nao tunawaona ...na Tanzania je???. ...Azimio la Zanzibar nalo halijatoa mwelekeo!!

Lakini justification ya theories za Marks ni kinachotokea leo kwenye nchi kama Ureno, Spain, Greece na zitakazofuatia.
Nasubiri kusoma zaidi juu ya hili hapa jf
 
Kama kuna kitu wanajf tulikikosa kwa muda sasa basi ni jukwaa hii adhimu. Hakika hapa ni mahali pa muafaka pa kupakua na kujitaalamisha ktk mambo mbalimbali ya kale, kwa niaba ya uongozi wa jf. Shukrani za dhati kwako Invisible! Hakika sasa tutafaidika na mengi ktk historia kwani tumepata mahali pa marejeleo! Shukrani pia mkuu Kichuguu, Ipycalypse na wengineo!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom