Hisia. . .

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,801
59,269
Tumeshazoea kusikia watu wakiambiwa "Usiusemee moyo wa mwenzio" pale hisia za kimapenzi (kupenda) zinapokua zinahusika. Na hiyo kauli kama wengi tunavyojua hua inamaanisha kwamba hakuna anaeweza kujua nini mwingine anahisi ndani ya moyo wake kwa uhakika hata kama matendo yake hayatii shaka kuhusu hilo. Binafsi hua napenda kumwamini mtu mpaka atakaponipa sababu ya kutofanya hivyo, kwahiyo mtu akiniambia anahisi hivi au vile, ziwe hisia nzuri au mbaya ndizo ntazichukulia kama zilivyo.

Nwy leo nataka kuongelea zile ambazo ni hasi kidogo. Kwanini watu hua wanaona wana haki ya kumuamulia/kuona wana uhakika na kile mwingine anachohisi? Kwa mfano unaweza ukasema kitu cha kawaida tu. . .alafu mtu akadakia "mbona unajibu/ongea kwa hasira?"/ "una hasira wewe!!" na kukomalia hayo maneno hata pale mhusika anaposema sio? Au utasikia "fulani hata hakuumia mpenzi/ndugu yake alipofariki" kisa hakutoa machozi. Ina maana mtu hawezi kua hacheki cheki na bado asiwe na hasira? Mtu hawezi akaumia moyoni na bado mnaomuangalia msijue kisa hajatoa chozi? Chozi hili hili ambalo hata kwa vitunguu linatoka? Mtu hawezi akawa kimya labda kwaajili ya mawazo binafsi bila ya kuhisiwa kakasirika ama kaboreka? Mtu hawezi akawa na matatizo binafsi bila ya wewe kulazimisha kwamba ndie mkasirikiwa/mhusika?

Naamini UELEWA ni silaha kubwa sana, yani inaweza ikakulinda na aibu/hasira na hasara wakati wowote ule. .na KUTOKUA muelewa ni hasara inayoweza ikakufanya hata uonekane mjinga wakati mwingine.

Binafsi hua naboreka sana pale mtu anaponilazimishia hisia ambayo sinayo kwa wakati ule. . .hata kama nilikua napanga kumwambia kitu ntaahirisha kama sio kuacha kabisa.

Unapoona mtu yupo tofauti na ambavyo ungependa/ulitarajia uliza kulikoni badala ya kuassume na kulazimisha jibu liwe lile ulilomwandalia. Epuka kulazimisha kua wewe ndio tatizo, maana usipoacha kulazimisha UTAKUA tatizo kwa kukosa uelewa. Penda kuuliza badala ya kuassume. . .
 
mhh afadhali mtu azungumze hisia zako kama mnafahamiana physically na mko mnaona na wakati huo

inafurahisha mtu anapojifanya anakuju kwa post tu za hapa jf.....

eti mbona umekasirika hivyo? lol

au fulani mbona unamfuata fuata kwenye post zake?

mna nini kati yenu?

watu kwa hisia lol
 
mm nieleweshe.unapata wap mda wa kufanya mamb mengne au kuna watu wanalpwa kupost sred nying ww ukia ktk hilo kund?
 
mm nieleweshe.unapata wap mda wa kufanya mamb mengne au kuna watu wanalpwa kupost sred nying ww ukia ktk hilo kund?
Hizi ndio Hisia za kijinga zinazoongelewa kwenye thread hii, The Boss ameelezea vizuri usijifanye unamjuwa sana mtu kwa post zake za JF. KAMA KAZI YAKO NI KUBEBA ZEGE usitake wote tuwe hivyo.
Mimi nafanya kazi mara 2 tu kwa mwaka na ninaingiza kipato cha ku cover life expenses zangu kwa miaka 2.
 
Lizzy hii kitu ipo sana ajabu zaidi ni pale hisia za wengi zinapoamua kuwa negative zaidi kuliko positive!
 
nani kakuulilza kazi yako hapa!! acha uzuzu wewe
 
c ndio mana nikaulza. Mbona unamwaga povu? Bado swal haljajbiwa kama unaweza. Acha kihere here kama hujaelewa!
 
nani kakuulilza kazi yako hapa!! acha uzuzu wewe
Usitake kuharibu thread ya watu, kama ni matusi mimi nina software ya matusi hujalazimishwa kuchangia thread hii heshima ni kitu cha bure, hizi ndio Hisia za kijinga kujifanya mnajuwa watu humu wakati ni mafala tu.
 
unajua unanifurahisha sana wewe, kitu gani kilichokufanya ukamjibu huyo Golden mpolee, nakuona hisia zake ni za kijinga, kila mtu anahisia zake vile vile unavyoona za mwenzio ni za kijinga kwake sio za kijinga.
 
Nadhani hisia huanzia hapa

"kimtokacho mtu kinywani ndicho kiijazacho nafsi yake"

Unaposema neno au kupost kitu, ninakibeba na kutafsiri kwa mtazamo wangu
Then nakimbilia ku-conclude, lakini inawezekana kabisa mwandishi au msemaji aliyesema neno lile ana mtizamo au matumizi yake ya maneno yale ni tofauti kabisa na yangu.

Zaidi naona ni ku-personalize maneno ya mtu mwingine na kujifanya yako
 
Hizi ndio Hisia za kijinga zinazoongelewa kwenye thread hii, The Boss ameelezea vizuri usijifanye unamjuwa sana mtu kwa post zake za JF. KAMA KAZI YAKO NI KUBEBA ZEGE usitake wote tuwe hivyo.
Mimi nafanya kazi mara 2 tu kwa mwaka na ninaingiza kipato cha ku cover life expenses zangu kwa miaka 2.
Mbona ameuliza vizuri, unamjibu kwa jazba? Kama kakosea mueleweshe alipokosea ili kesho asirudie tena.
 
unajua unanifurahisha sana wewe, kitu gani kilichokufanya ukamjibu huyo Golden mpolee, nakuona hisia zake ni za kijinga, kila mtu anahisia zake vile vile unavyoona za mwenzio ni za kijinga kwake sio za kijinga.
Kama kila mtu ana Hisia zake wewe unapata wapi uhalali wa kuongelea Hisia za Golden Mpolee!!??
 
Wee matola, unafanya nini?
Ujue unanyoa ndevu ivoo
utaangusha msuli bure kukimbizana kusiko na sababu.
 
Mie nilishajiambia
Nina maamuzi ya mwisho na masiha yangu
As long as am comfortable, nafanya nitakacho, wakati wowote, kwa staili yeyote

Watu wanajidai weeeema, lakini wana maasi gizani ambayo hata sheitwani huwa anashangaa

Lizzy hii kitu ipo sana ajabu zaidi ni pale hisia za wengi zinapoamua kuwa negative zaidi kuliko positive!
 
Mkuu mimi hapa napata hisia kwamba umekasirika kutokana reaction yako. au nalo hili hisia zimenidanganya?

Usitake kuharibu thread ya watu, kama ni matusi mimi nina software ya matusi hujalazimishwa kuchangia thread hii heshima ni kitu cha bure, hizi ndio Hisia za kijinga kujifanya mnajuwa watu humu wakati ni mafala tu.
 
Mbona ameuliza vizuri, unamjibu kwa jazba? Kama kakosea mueleweshe alipokosea ili kesho asirudie tena.
Ameuliza vizuri kwamba kuna Members wanaolipwa kwa kupost thread? are u serious!! angeuliza kwamba kwa sababu mleta thread ni Premium Member je anaichangia JF pesa kiasi gani kwa mwaka? hili lina logic.
Hivi kwa fikra finyu kama hizi Mtu unaweza kuwa miongoni mwa Great thinker? kweli nimeamini kichuguu ndio nyumba pekee ambamo nguchiro na nyoka wanaishi pamoja.
 
Back
Top Bottom