Hisia za ukabila za shibuda juu ya chedema haziwakilishi mawazo ya wasukuma.

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Wakuu.
Nimekutana na hoja za huyu bwana anaye onekana amekerwa na hisia za ukabila wa Shibuda juu ya chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) na ameamua kufunguka na kuweka msimamo wake kama jinsi anavyosomeka hapa chini. NImeona si vibaya nika washirikisha na nyinyi mumsome mawazo yake...

Nimesikitishwa na kukasirishwa sana na taarifa iliyo kwenye gazeti moja la leo juu madai ya Shibuda kwamba anasakamwa ndani ya Chadema kwa sababu yeye ni Msukuma. Kwanza sikuamini kama Shibuda (katika akili timamu) anaweza kutamka maneno ya namna hiyo. Pili siamini kama kweli maneno hayo yanaweza kutamkwa na Msukuma halisi kwa maana ya kabila, tabia, na mtazamo. Hata hivyo baada ya kutafakari kauli za nyuma za Mh. Shibuda tangu mwaka 2005 hadi alipohamia Chadema mwaka 2010, nimejiridhisha kuwa maneno yale kweli huenda yametamkwa na yeye. Pengine kitu kigumu kabisa kwangu ni kuishawishi akili yangu ikubaliane na wazo kwamba maneno hayo yanaweza kutamkwa na Msukuma akiwa hajalewa, hana kichaa (kwa kisukuma "lusalo") au ugonjwa mwingine wa akili. Nitafafanua.

Kwanza, kama inavyofahamika kwa wengi, Wasukuma ndiyo kabila kubwa kuliko yote hapa nchini. Jamii ya wasukuma imeenea sehemu kubwa ya kanda ya Ziwa hasa Mwanza, Shinyanga na Tabora. Kwa tabia na aina ya shughuli zao za kiuchumi, wasukuma wamesambaa pia katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Katavi, Tanga, na Pwani. Takwimu za idadi ya watu katika sensa ya mwaka 2002 zinaonesha kuwa kulikuwa na Wasukuma karibia milioni 8 kati ya watanzania milioni 36 wa wakati huo. Kwa kutambua wingi wao hapa nchini, Wasukuma wamejijengea tabia ya kujiamini na kutotishwa na uwepo au mafanikio ya kabila jingine mahali popote.

Haijawahi kutokea Msukuma halisi akalalamika juu kuingiliwa na kabila jingine au kutishiwa na mafanikio ya kabila jingine. Wasukuma ni wapole, wavumilivu, wenye busara, na hawana wivu na mafanikio ya mtu au kabila jingine. Ndiyo maana hata katika ngazi mbalimbali za uongozi, watu wa makabila mengine ni rahisi sana kukubalika na na hata kupigiwa kura kuwa viongozi katika maeneo ya wasukuma bila kujali wanakotoka. Kwa ujumla, linapokja suala la kutohisi au kujali ukabila, wasukuma wamestaarbika muda mrefu sana pengine kuliko kabila jingine lolote hapa nchini. Wengine wanaona huo ni ujinga. Sisi wasukuma tulioenda shule vizuri na kuona yanayotokea kwingine duniani tunaita huu ni ustaarabu. Hili la ustaarabu wa wasukuma hata Shibuda mwenyewe analijua, na kwa bahati mbaya nalo limekuwa likimsumbua. Ndiyo maana napata taabu kuelewa aina ya wasukuma anaowawakilisha Shibuda katika baadhi ya matamshi yake.

Pili, kwa hulka halisi ya Kisukuma (hasa wale wa Mwanza; Shibuda ni Msukuma wa Shinyanga) si rahisi kumkuta baba mzima wa kisukuma akilialia kuonewa au kubaguliwa na mtu au kabila lolote. Wasukuma ni watu wa kujiamini. Wanajiona ni wengi, wenye nguvu, mali nyingi, na kama baba wa 'vikabila' vingine vyote hapa chini (situmii neno 'vikabila" kwa maana ya kudharau makabila mengine bali ni namna tu ya msemo wa kisukuma wenye kuonesha hali ya kutotishwa: kumbuka neno 'vijisenti'?). Ukisikia mwanaume mzima wa kisukuma analalamika; iwe kumlalamikia mtu mwingine au kundi au kabila jingine ujue huyo ni msukuma aliyechanganyikiwa au kushindwa maisha (kwa kisukuma "balemelwa").

Kwa asili na historia yao, wasukuma hawajawahi kulalamika kubaguliwa mahali popote na mtu yoyote nchini. Hata inapotokea kweli wakadhulumiwa, wakanyanyaswa, au kutumiwa (kama ilivyofanya CCM kwa zaidi ya mika 50) wasukuma huvumilia huku wakijipanga. Na muda unapofika huonesha msimamo wao kwa vitendo (rejea yaliyotokea Nyamagana na Ilemela uchaguzi 2010). Ni wasukuma wachache sana (wa aina ya Shibuda) wanaoweza kudekeza vijembe na vijimaneno vya ushwahilini kwa lengo la kutafuta huruma ya watu. Tangu lini kabila kubwa lenye uwezo, mali, na historia ya kujiamini kama wasukuma likaanza kupiga kelele ya kuonewa na watu wa makabila madogo? Hicho ni kilio cha Shibuda na tumbo lake na si kilio cha wasukuma.

Mwisho, nataka Mh Shibuda aweke wazi kuwa matatizo yake na Chadema si matatizo ya wasukuma na Chadema. Kama anahisi kubaguliwa na Chadema kwa sababu ya 'aina ya usukuma wake' basi atambue pia kuwa anabaguliwa hata na wasukuma wenzake ambao sasa wamejaa ndani ya Chadema. Na mimi nataka kusisitiza kuwa kama anafanya vurugu zote hizi kwa lengo la kuitisha Chadema au kuvuta hisia za wasukuma na huruma zao ili wampe urais kwa kigezo cha ukubwa wa kabila lake basi ajue ameaumia. Wasukuma hawako tayari kuwakilishwa na mtu wa aina ya Shibuda (labda wale wa jimboni kwake tu). Kuna wasukuma wengi wasomi, waelewa, wastaarabu, na wenye hekima mara elfu kumi ya Shibuda. Kwa ujumla, karata ya ukabila haichezeki uskumani. Hata kama itatokea waaamue kuicheza, hawatakuwa tayari kuunga mkono mtu wa kuwaharirisha mbele ya makabila mengine (madogo) nchini kama Shibuda. Ndani ya wasukuma kuna majembe ya ukweli yanayoweza kugombea urais na kufanikiwa lakini si jembe butu na lililochoka kama Shibuda.

Kama Msukuma mwenzake na mwelewa wa tabia na mtazamo wa kabila langu, namwomba kaka yangu Shibuda asizidi kutuaibisha na kututengenezea taswira tusiyokuwa nayo miongoni mwa watanzania. Asitulazimishe kukubaliana na hisia zake za kipuuzi zinazotokana na msukumo wa wake wa kimaslahi na kutafuta sifa za kijinga na pengine huruma ya wapiga kura wake atakaporudi kugombea tena kwa tiketi ya chama chake halisi yaani CCM. Na kama anataka kweli kutumia karata ya ukabila kulazimisha kugombea urais kupitia Chadema basi akaanzie jimboni kwakwe alikotokea ili tuone kama kweli anaweza kuwazidi akili wasukuma wote wa huko hata kuwafanya waingiwe na hisia potofu zisizotokana na hulka halisi za Kisukuma.

Imeandikwa na Ikwalal M. Ikwalala
Wa Mwanza.
 
Ukimfuatilia Shibuda utaumiza kichwa bure kaka. Maana shibuda hajielewi anataka nini... :der: Mimi nashauri ni bora apige keleleee kisha atanyamaza tu.
 
Ni kweli mkuu, wasukuma siyo watu wa kulialia. Nadhani Shibuda anasumbuliwa na uswahili wa pwani baada ya kuishi Tanzania visiwani kwa muda mrefu. Kwa hiyo naye ameathirika na kuwa mliajiliaji kama wazenji.
 
Sijui Shibula ana uwezo wa kuelewe hii uzi. Uzi hii inakata kweli kweli. Big up
 
Kumfukuza shibuda ni woga na woga ni kosa kubwa, aachwe tu abwabwaje tanzania hakuna mtu asiyemfahamu; system itamtema yenyewe wakati ukifika, wananchi watamkataa saa ikiwadia; asifukuzwe na asijibiwe ili tuoneshe namna nyingine ya kushughulika na ccm karne hii
 
wasukuma, watu wa kujiamini mahala popote, kuongea kisuma mahala popote ndo sifa za kuwa msukuma kwelikweli
 
Ni kweli mkuu, wasukuma siyo watu wa kulialia. Nadhani Shibuda anasumbuliwa na uswahili wa pwani baada ya kuishi Tanzania visiwani kwa muda mrefu. Kwa hiyo naye ameathirika na kuwa mliajiliaji kama wazenji.

Kwa wale mliokaribu na Shibuda, hivi hata kisukuma anakijua kweli au anacho cha kuombea maji tu? Nasema hivyo kwani sijawahi kumsikia bungeni akimwaga nahau/misemo ya kisukuma tofauti na vijembe uchwara vya ki-Zenj,

Kwa kifupi Shibuda ni wa kumdharau, kwani hata mtaani ukikutana na kichaa fulani na akaanza kukutukana basi salama yako ni heri ukae kimya kwani ukianza kujibizana naye kweli anaweza kukudhuru na yeye hana hasara
 
Hivi huyu ndiye Shibuda aliyewahi kuteremshwa kwenye train Tabora, wakati akienda Dodoma kugombea Uenyekiti wa wazazi wa CCM na Idd Simba?

Kama ndiye the guy is very controversial!
 
Wala siyo controversial, he is a stupid oppotunisit.
 
Back
Top Bottom