Hisa za Zanzibar katika Benki Kuu: Je, SMZ imewahi kuipa ruzuku BoT?

Hii nchi ya madudu tu , hesabu zao nchi wanazifanya Dodoma na kutuambia walitakalo , sio lile la kweli !! Kila upande wa muungano unalalamika dhidi ya mwengine , je bado hatujajua tu kuwa huu ni muungano wa viongozi na usio wazi kwa raia ? mi binafsi yangu siufahamu huu muungano !!
 
jokaKuu,
Kama Gavana Ndullu amesema kuwa benki kuu imepata faida kwa mara ya kwanza tangu iundwe basi ama hajui anachosema au anapotosha ukweli makusudi. Nakumbuka mwaka 1977 kabla ya vita vya Uganda kulikuwa na mjadala mkubwa pale Benki kuu wakati Gavana akiwa Nyirabu. Wakati huo benki kuu ilikuwa imepata faida na Gavana Nyirabu alikuwa amependekeza wafanyikazi wapewe bonus. Kuna baadhi ya wasocialist pale waliokuwa wanapinga wazo hilo eti kuwapa wafanyikazi bonus ni kinyume cha maadili ya ujamaa. Kwa hiyo hii si mara ya kwanza kwa benki kuu kupata faida.

....Imepata faida na kutoa gawio la......
Inawezekana kabisa ilipata faida katinka nyakati hizo ulizozitaja, lakini tofauti na kipindi hiki ni namba na kutoa gawio.
 
JokaKuu,

Kuhusina na kuwepo kwa taarifa kwamba ZNZ ilitoa 11% ya mtaji wa kuanzisha BOT, sio taarifa bali hata serikali imekubali hili. In fact, kuna mgogoro wa muda mrefu tuu kati ya serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusiana na shares za Zanzibar BOT. Hili suala lilibbuka bungeni hivi karibuni ambapo kama sijakosea Mh. Hamad Ali Hamad (CUF) aliuliza swali la nyongeza kutaka ufafanuzi kuhusiana na asilimia 11.5 ya shares za Zanzibar BOT. Swali lake la nyongeza lilitokana na kutoridhika na majibu ya Naibu Waziri wa Fedha kwa swali la msingi lililoulizwa na Rashid Omar (CUF).

Katika swali lake la msingi Rashid Omar alisema kulikuwa na taarifa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni shareholder wa kwanza kabisa wa BOT. Then, akataka kujua kama Zanzibar ilishawahi kufaidika na matunda ya shares zake BOT. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha wakati huo Pereira Ame Silima (sasa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani) alimjibu kuwa BOT ilianzishwa na Bank of Tanzania Act 1965 kama chombo kilichokuwa chini ya Serikali ya Muungano wa Tanzania.

Ni kweli kabisa BOT ilianzishwa na Bank of Tanzania Act 1965 to take over the functions and operations of the then East African Currency Board (EACB) founded in 1919 to manage currency supply and exchange in the then British colonies of East Africa and neighbouring countries. Kuna maandishi yanasema kuwa baada ya kufa kwa EACB, pounds 950,000 as dividend of Zanzibar and 668,884 Pounds BOT capital from EACB were taken by Union Republic to establish the BOT.

Kwa mujibu wa swali la nyongeza la Hamad Ali Hamad (CUF), records zinaonyesha kuwa Zanzibar ilikuwa na asilimia 11.5 ya shares kwenye EACB. Wakati BOT inaanzishwa, shares hizo zilihamishiwa BOT. Katika swali lake, Hamad Ali Hamad (CUF), alitaka kujua zilipo hizi shares ambazo zilihamishiwa kutoka EACB kwenda BOT.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Fedha alikubali kuwa asilimia 11.5 ya shares za Zanzibar EACB zilihamishiwa BOT wakati wa kuanzishwa kwa benki hiyo. Kuhusu zilipo shares hizo, Naibu Waziri huyo alisema it is still unclear na kwamba ni moja ya controversial issues za muungano ambazo zinafanyiwa kazi kwa sasa na serikali za pande zote mbili.

Kuhusiana na kuwepo kwa People's Bank of Zanzibar ambayo ilikuwa ikifanya kazi kama "benki kuu" ya ZNZ kwa kipindi kirefu mpaka miaka ya 80 au 90, ni kweli kuna benki inaitwa the Peoples Bank of Zanzibar (PEOPLE'S BANK OF ZANZIBAR ) ambayo ilianzishwa mwaka 1966 na serikali ya Zanzibar under Cap. 153 of the Zanzibar Companies Decree. Hii benki ilikuwa imejikita zaidi Zanzibar hadi mwaka 2011 ilipofungua tawi Dar Es Salaam na ilikuwa na mpango wa kufungua matawi Mwanza, Mtwara na Arusha.

Benki hii bado inamilikiwa na serikali ya Zanzibar kwa asilimia 100. Ni moja ya benki za zamani sana Tanzania. Ni kweli ilikuwa ina-function kama commercial bank na central bank ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi mwaka 2001 ambapo kazi zake ki-central bank zilihamishiwa BOT.

Whether Zanzibar imekuwa ikipata mgao kutokana na faida inayopata BOT kulingana na kiwango cha shares zake za mwaka 1966 au kutoa ruzuku wakati BOT ikipata hasara ni ngumu kujua. Lakini kwa mujibu wa majibu ya Naibu Waziri kwa wabunge hao, hisa zote za BOT zilimilikuwa na Serikali ya Muungano. Hata Bank of Tanzania Act 2006 bado inasema hivyo.

Kifungu cha 2 cha sheria hiyo ya mwaka 1965 kilisema kuwa the "Act shall extend to Zanzibar as well as to Tanganyika citation shall bind the United Republic." Section 14(1) of the 1965 Act provided that "the authorized capital of the Bank shall be twenty million shillings". Section 14 (2) provided that "the capital of the bank shall be subscribed and held only by the United Republic. Kama kweli start-up capital ya BOT i.e. twenty million shillings ilitokea Treasury ya Serikali ya Muungano na kuwa custodian wa shares za BOT alikuwa Treasury Registrar, interests and liabilities za Zanzibar to BOT as an individual zinatokea wapi tena?

Lakini kuna article moja inajaribu kuelezea kuanzishwa kwa BOT na kuhamishiwa rasilimali za Zanzibar kwa nguvu hasa zile zilizokuwa EACB kwenda BOT kinyume na makaubaliano ya Muungano ya mwaka 1964. Labda ndio maana katika majibu yake, Naibu Waziri alipoulizwa kuhusu zilipo asilimia 11.5 ya shares hizo alisema bado haieleweki na kwamba ni controversial issue ya muungano ambayo inayofanyiwa kazi na serikali za pande zote mbili. Nina hard copy ya hiyo article, nitajaribu kutafuta soft copy niiweke extract husika hapa.
 
Mkuu EMT nakumbuka waziri wa fedha wa ZNZ aliulizwa swali kuhusu mgao wa share na alisema wazi kuwa wamekuwa wanapokea tangu mwaka (1995 au 97 sina uhakika) lakini ni katika kipindi cha miaka niliyoitaja hadi sasa.
Hapo swali likawa limejibiwa. Nitajaribu kutafuta Hansard za BLW. Nina uhakika na hicho.

PBZ ilihamishiwa BoT wakati wa Ali Hassan Mwinyi. Kumbuka huyu alikuwa Rais wa ZNZ kabla ya kupewa jukumu la muungano. Kwahiyo madai ya kuwa Nyerere aliua PBZ si ya kweli na ni uzushi wa kawaida wa WZNZ.
Nasor Moyo kawaambia BLW mchana kweupe kuwa aliyehamisha PBZ ni A.H.Mwinyi.

Kuhusu ZNZ inachangia nini, nashindwa kuelewa kwanini watu hawaitambui SMZ. Hii si mkoa au Wilaya, ni serikali.
Kinachopaswa kuonekana ni wao kama SMZ wanachangia kitu gani katika muungano?

Ni ukosefu wa fikra na ujuha pale mtu atakaposema eti Tanganyika inachangia nini. Ikumbukwe kuwa ulinzi na usalama wa ZNZ pamoja na Rais na mashekha wao unachangiwa na muungano. Mbona hapo Tanganyika haitajwi.
Pesa bilioni 32 alizopokea Bilal ni za muungano mbona ZNZ inazikubali kama za muungano.

Hoja hii ni kama ile ya Maalimu Seif aliyoitoa leo. Baada ya kumbana kuwa anauma maneno leo kauma zaidi. Kasema anataka ZNZ huru lakini yenye mkataba na Tanganyika. Ni kwasababu hizo za kujificha nyuma ya Tanganyika ni ngumu kuelewa mchango wa ZNZ ni upi, ingawa ukweli ni kuwa hakuna. Hakuna kwasababu ni Zero.
Lakini ZNZ inachukua nusu ya bajeti yake kutoka Muungano. Fuatilia hesabu za mapato na matumizi utaona nakisi ya bajeti ya bilioni 250 kati ya bilioni 660 zinatoka muungano.

Swali linalobaki ni kuwa kwanini wao wadai share wasidai share ya madeni?
 
Nguruvi3,

..mimi nadhani tuwaunge mkono na juhudi zao za muungano wa mkataba.

..nina hakika hakuna Mtanganyika atakayekubali huu upuuzi wa kuendelea kuwapakata wa-Zanzibari.

..nadhani muungano wa sasa hivi ni vigumu kuuvunja kuliko muungano wa serikali 3, au hata huo wa mkataba wanaouzungumzia.
 
Joka Kuu,

................
Moja, Zanzibar ilipata uhuru wake mwaka 1964, na ndani ya mitano na nusu, ikaungana na Tanganyika, na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Originally, kwa ufahamu wangu, suala la FEDHA halikuwa sehemu ya mkataba wa muungano, suala hili liliingizwa baadae kwenye katiba ya Muda ya mwaka 1965, na likaendelea kuwa treated KIMUDA MUDA mpaka 1977 katiba ya kudumu ilipozaliwa. Sasa iwapo Zanzibar ilichangia 11% towards uanzishwaji wa BOT in 1966, ningependa kwa wale waelewa zaidi wanisaidie kunielimisha kwamba mchango huu ulifanyika chini ya makubaliano yepi - mazingira haya yalihalalishwa na nguvu gani;

............
Mzee Mtei angetusaidia sana angefunguka kuhusu hili suala. Si mara moja mada kama hii imeletwa lakini Mzee Mtei ambaye alikuwa Gavana na waziri wa fedha kwa vipindi tofauti ameamua kukaa kimya.

Tukusanye sahihi za wanajf za kumbembeleza Mzee Mtei aje atoe ufafanuzi wa haya mambo. Hapa bila data ni kupiga mayowe tu.

Pia Jussa aliwahi kutoa kauli kuwa kuna ripoti ya mshauri mwelekezi ambayo inasema kuwa shughuli za muungano(mambo ya muungano) yanajiendesha kimapato na linabakia salio. Kama Jussa ni member hapa pia anaweza kutuanikia hiyo ripoti ili mjadala unoge.

Data iliyopo ni bilioni 32 tu alizopewa Bilali ili atetee muungano wa serikali mbili kuelekea moja.

Mimi napata tabu kidogo na usiri mkubwa juu ya mapato na matumizi ya mambo ya/shughuli za Muungano. Kwa nini hata wabunge hawahoji juu ya hili na wananchi wakaelewa kifedha nini kinaingia na nini kinatumiwa kwa mambo ya muungano.
Nini kinaingia cha Tanganyika(mambo yasiyo ya muungano kwa bara) na kinatumika vipi.

Kama haya yangewekwa wazi nafikiri dhana/kauli za kubeba viroba vya misumari, tunaonewa zingeweza kuthibitishwa kwa mahesabu na maelezo yaliyo wazi.

Mzee Mtei na Jussa karibuni mtusaidie hapa kwa maelezo na ufafanuzi juu ya jambo hili linalotutafuna mawazo na fikra.
 
1995- 2000: Sio siri kwamba Zanzibar ilikuwa katika kipindi kigumu hadi kushindwa kulipa misharaha ya wafanyakazi wake.

1993- 2000: EPZ ilianzishwa, hata hivyo kutokana na kubanwa kimisaada, mpango mzima ulishindwa kuendelea.

1995- 2000: Ni miaka ambayo Zanzibar ilidai kwa nguvu zote gawio lake la 4.5% katika kipindi chochote kile cha muungano.
 
Hii hoja ya leo imejaa ushabiki ningeomba Mzee Mwanakijiji na wote waliotajwa wafanye utafiti wa kina kuhusu kuanzishwa kwa BOT maelezo yako wazi na hiyo asilimia 4 imefikiwa vipi.

Pia SMZ kama wanapewa pesa na BoT kulipa mishara huo utakuwa ni mkopo kama wanaopatiwa SMT. Kama ukweli haujulikani tusizungumze tufanye utafiti.

Kuhusu umeme ninavyoelewa ni kwamba SMZ wakati wa rais Abood jumbe waliulipia kwa pesa zao.

Mwisho; hebu fanyeni utafiti kuna tetesi kuwa SMT ilikaribia kuwa insolvent kwa lugha yao na ikabidi rais Jumbe atoe mahela kwa magunia kuisaidia nchi kaka wasitangaziwe wamefilisika (hiyo ni miaka ya 70); sababu mnazijua hebu tupeni ukweli.

Kaka/dada zangu msisimuliane nani kafanya nini na ana uwezo gani, yapo mengi ya kila upande kumfanyia mwenziwe na hiyo ndio spirit ya muungano. Mkiendelea na lugha hizi zinawa panguvu muamsho na kundi lao. Miaka 50 hatujauana; naomba miaka mingine 50 ya kuishi kwa usalama ndani ya jamhuri.

Znz na bara zikitengana, tutajuta! Fuatilieni visa vya mara kwa mara baina ya Urusi ile ya muungano na wenzake waliotengana; hakuna maisha ya raha wanatiliana wasiwasi mpaka wanafikia karibu na kuanzisha vita kwa chokochoko za kila upandee
 
Last edited by a moderator:
Naona kuna masuala mengi sana kuhusu kadhia hii. Mimi nawashauri pitieni taarifa ya JOINT FINANCE COMMISSION ambayo ni moja ya taasisi tanzu za BOT inayoshughulikia mambo hayyo ya mgao wa kila nchi na kuangalia maslahi ya kila upande.

kama mtapitia taarifa zao kiundani basi mtaona ukweli upo wapi.

Kwani nimewasome wengi mpa katika kubuni na kuandika kile kisicho sahihi.
Afisi zao zipo Sukari house, Posta dar es salaam.
 
@ Nguruvi3

Si kweli kwamba Pesa za waya ni mkopo kutoka Serikali ya Muungano. Huu umetoka mkopa kutoka Marekani katika Milleneum project
 
Joka kuu, pia kuna asilimia 7 ZNZ inapata kutoka pato la taifa.


Jana nimeona Shein anapokea nyaya za umeme, kumbuka hizo zimelipiwa na JMT, kama ni mkopo huo ni wa Mtanganyika.

Mambo kama hayo ndiyo yanawafanya WZNZ wang'ang'anie mkataba. Wanajua wanachokipata ndani ya huu muungano wasiotaka kuuvunja lakini kelele nyingi.

Hivi mkuu upo ushahidi kuwa hizo nyaya za umeme zimelipiwa na JMT??? Au tunasema tu ili tuwe tumesema???
 
Joka Kuu,

Hii habari ya BOT kupata faida kwa mara ya kwanza ni sawa na hoja kuwa Mshahara wa Rais ni siri! As Joe Biden would say it is a bunch of marlakey!

Then it means Serikali has never made any economic progress on its balance sheet!
 
Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Jasusi, Mchambuzi, Nonda, Mdondoaji, Barubaru, Ritz, Jasusi, Taso,

..hebu tuendelee kuuchunguza huu muungano wetu zaidi.

..kuna taarifa kwamba ZNZ ilitoa 11% ya mtaji wa kuanzisha BOT.

..pia AG wa ZNZ aliwahi kunukuliwa akisema kwamba pamoja na kutoa hisa hizo, SMZ ilianzisha PBZ[People's Bank of Zanzibar] ambayo ilikuwa ikifanya kazi kama "benki kuu" ya ZNZ kwa kipindi kirefu mpaka miaka ya 80 au 90.

..katika gazeti la raia mwema, gavana wa BOT, Prof.Ndulu, amenukuliwa akisema kwamba kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa BOT, benki hiyo imepata faida na kutoa gawio la $ 173 million kwa serikali.

..kwa msingi huo huenda basi ZNZ na SMZ wamepewa mgao stahiki kutokana na faida iliyopatikana BOT.

..hapa nitapenda kuhakikishiwa kwamba ZNZ imepata stahiki yake kutokana na kiwango cha hisa ilichotoa mwaka 1966.

..kitu kingine ambacho amekieleza Prof.Ndulu ni kwamba kwa muda wote tangu kuanzishwa kwake BOT ilikuwa ikiendeshwa kwa RUZUKU kutoka serikalini.

..sasa mimi napenda kuuliza: Katika miaka yote ambayo BOT ilikuwa ikiendeshwa kwa HASARA na kutegemea RUZUKU toka serikalini, ZNZ au SMZ ilikuwa ikitoa kiasi gani??

Nakala:
takashi, Zitto, Edwin Mtei, Mkandara, EMT, Kitila Mkumbo, Masanja, Rev. Kishoka, Kasheshe, Nnauye Jr, Maxence Melo, Kiranga, Geza Ulole, Kubwajinga, Nonda, Malila, Kichuguu, Nyani Ngabu, Selemani, Mohamed Said, maggid

NB:

..nawaomba wote mchangie hoja hii. hata wale ambao sikuwa-tag mjisikie huru kabisa kuchangia hapa. kila mmoja wenu achangie tafadhali.

Mkuu,

Joka Kuu usinione kimya nimekumbwa na kazi nyingi ila nategemea weekend hii inshallah nitakuwa free nitaisoma na kujaribu kudondoa mawili matatu kwa mujibu wa kumbukumbu zangu. Niwie radhi kwa kutokurespond .

Nilikuwapo!!!!
 
Governor Ndulu must have been talking about something which the reporter mistook for profit.

As the Founder Governor of the Bank of Tanzania, I can confirm that even in the first year of operations, 1966/67, the Bank of Tanzania made a profit which under the then Bank of Tanzania Act, was credited into the Consolidated Fund of the Government of the United Republic of Tanzania, as sole shareholder, under the then legislation.

I can also confirm that during my governorship, the Bank never received a subsidy from Government after the utilization of the capital of TSh. 20,000,000 paid up by the Government.
 
Benki kuu imekuwa ikipata faida kila mwaka na haipati ruzuku, sema mwaka huu imepata faida sana kupita shirika lolote la umma.
Hili ni tatizo ni la mwandishi
 
Leo nilikuwa najikumbusha makala za huko nyuma. Mtunzi wa makala hii aidha hakumuelewa Prof Ndulu au ameamua tu kuvuta attention ya Wana Jamii. Ukweli ni kuwa:
1. Bot HAIJAWAHI KUPATA RUKUZU hata mara moja!
2. Mgao huo mkubwa ni RECORD kwa BOT na si wa kwanza.
3. Hupata faida mara kwa mara na mgao hutolewa sambamba na faida hiyo.
4. Ukitaka kujua haya soma BOT ANNUAL OPERATIONS REPORT ambazo hupatikana www.bot.go.tz au www.bot-tz.org

Kwa taarifa yenu mali za BOT ni 10trn sawa na makusanyo yote ya TRA ya mwaka mzima hivyo ruzuku ingekuwq kubwa sana. Ingekuwa ngumu sana.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom