Hisa za NMG sasa kuorodhesha DSE

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Hisa za NMG sasa kuorodhesha DSE Saturday, 18 December 2010 09:15

nation-logo.jpg
Samuel Kamndaya
MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), imetoa ruhusa kwa Kampuni ya Nation Media Group (NMG), inayomiliki Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), kuorodhesha hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Kitendo hicho kinawapa fursa Watanzania kununua hisa, ili kumiliki sehemu ya kampuni hiyo ya kwanza kwa ukubwa kuliko nyingine yoyote, katika nyanja ya vyombo vya habari, katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Gabriel Kitua, aliwaambia waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki hii, kwamba ruhusa imeshatolewa na kwamba kilichobaki ni kwa kampuni kupanga muda wa kuanza rasmi kuuza hisa zake katika soko hilo, lililoanza miaka 12 iliyopita.

“Ingawa leo (Jumatatu) sio siku ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari, lakini ukweli ni kwamba ruhusa imeshatolewa na kilichobaki ni kwa Kampuni ya NMG kuandaa siku ya kuanza rasmi kwa mauzo ya hisa zake pale DSE,” alisema.
Alikuwa akizungumza katika semina iliyoandaliwa na DSE, ili kuwafundisha waandishi kuhusu jinsi soko la hisa linavyofanya kazi zake.

Kuorodheshwa kwa hisa za kampuni hiyo katika DSE, kutawafanya wawekezaji wa sasa na wakakaokuja wa NMG, kupata hisa katika masoko ya hisa za nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Oktoba mwaka huu, NMG iliorodhesha hisa zake katika Soko la Hisa la Uganda na mwezi uliopita, hisa za kampuni hiyo ziliorodheshwa katika Masoko ya Hisa la Rwanda na Burundi, nchi ambazo pia ni wanachama wa jumuiya hiyo.

NMG inakuwa kampuni ya tano kutoka Kenya, kuuza hisa zake katika DSE.
Kampuni nyingine ni ile inayozalisha bia ya Africa Mashariki (EABL), Kampuni ya Ndege ya Kenya, Benki ya Biashara ya Kenya na Diamond Jubilee.

Kampuni hiyo, iliyoorodheshwa katika Soko la Hisa la Nairobi tangu mwaka 1973, itakuwa ya kwanza katika kampuni ya vyombo vya habari kuuza hisa katika DSE.
Katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, NMG ilipata faida ya baada ya kulipa kodi ya Sh597.5 milioni za Kenya ambazo ni sawa na Sh11.352 bilioni za Tanzania.

Ripoti ya kampuni hiyo inaonyesha ukuaji wa mauzo ya magazeti na mapato yatokanayo na matangazo kwa vyombo vyote vya habari inavyovimiliki.

Mauzo ya kampuni ya Mwananchi, inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, Sunday Citizen na Mwanaspoti yalipanda kwa asimilia 32 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, huku mapato yatokanayo na matangazo yakiongezeka kwa asilimia 29.
Hii imetokana na kampuni ya Mwananchi, kupata mtambo wakuchapisha magazeti ambao ni wa kisasa zaidi na ambao ni wa kwanza hapa nchini.
 
Napenda kujua ni gani huu mchakato wa kununua na kuuza hisa unavyofanya kazi.
 
Napenda kujua ni gani huu mchakato wa kununua na kuuza hisa unavyofanya kazi.

Kuhusu mchakato huu wasiiana moja kwa moja na wataalamu waliopewa leseni na mamlaka husika kwa kazi hiyo kupitia: (DSE: Dar es Salaam Stock Exchange).

Kwa maelezo ya jumla tembelea tovuti ya Dar es Salaaam Stock Exchange (DSE), facebook page ya DSE (https://www.facebook.com/dsetanzania), blog ya DSE (http://dsetanzania.blogspot.com), na unaweza kupata program za uelimishaji kupitia DSE twitter na Youtube.
 
Back
Top Bottom