Hip hop Facts Thread

WATU NA VYANZO MBALIMBALI VILIVYOWAHI KUFAFANUA HIPHOP

Baadhi ya watu na vyanzo mbalimbali vya habari vimewahi kufafanua Hip Hop kwa nyakati tofauti tofauti kulingana na mapokeo. Wafuatao/vifuatavyo ni vyanzo na watu mbalimbali waliowahi kufafanua maana ya hip hop:-

AFRICA BAMBATAA

“Hip hop ni harakati za utamaduni mzima. Unapoongelea kughani (rap), kughani ni sehemu ya utamaduni wa hip hop. Ughanaji (emceeing), umanju (deejaying), uvaaji, lugha vyote hivi ni sehemu ya utamaduni. Wavunjaji (break dance), namna unavyotenda, unavyokwenda, unavyotazama (mambo) ni sehemu ya utamaduni na muziki wake hauna ubaguzi rangi. Muziki wa hip hop umetokana na weusi, udhulungi, njano, nyekundu, nyeupe……. ni sehemu za hip hop”.

DJ KOOL HERC

“Hip hop ni kemia (chemistry) ambayo imetoka Jamaika.. nilizaliwa Jamaika na nilikuwa nasikiliza muziki wa kiamerika nikiwa huko huko. Msanii niliyekuwa nikimpenda ni James Brown. Ndiye aliyenivutia mimi, nilikuwa nikicheza vibao vingi vya James Brown. Nilipokuja hapa (Bronx) nilijiweka katika mtindo wa kiamerika ili kuendana na mazingira. Niliweza kukata midundo na kuicheza kwa muda mrefu na watu wakaipenda, niliwapa ladha waliyoipenda……’’

DAVEY D

“Hip hop ni utamaduni ambamo ughanaji (rap) ndimo umeasisiwa. Mwanzoni ulikuwa na nguzo nne ambazo ni sanaa ya machata (graffiti art), mavunjanji (break dancing), umanju (dj) na emceeing (ughanaji). Hip hop ni mtindo wa maisha ambao una lugha yake, mtindo wa kuvaa, muziki wake na fikra zake hukua kila siku. Siku hizi machata pamoja mavunjaji havitiliwi maanani sana ndio maana neno “rap” na “hip hop” yanatumika kwa pamoja kumaanisha kitu kimoja lakini ikumbukwe kila nguzo zina umuhimu na zinaendelea kuwepo katika utamaduni”
Anaendelea kusema “tatizo ni kuelewa maana ya hip hop, mara nyingi huwa inatolewa na wazungu (whites) wenye vyombo vya habari au wale ambao huwa wanapata nafasi ya kuhojiwa katika vyombo hivyo. Huwa wanaelezea maana ya hip hop kwa manufaa yao na sio kwa manufaa ya uma na wale waliouasisi utamaduni huu wa hip hop”

COMMON
“Hip hop ni njia yetu ya kujieleza (expression). Niliipenda mapema zaidi pindi tu ilipotambulishwa (hip hop) kwangu. Nilisikia “the message” ya Melle Mel… nilipenda namna alivyowasilisha na nilipenda pia alichokuwa akikisema
 
SAMIA X

Samia X ni mmoja kati ya waasisi na waanzilishi wa kundi la KWANZA UNITY amewahi kusema

“ Hip Hop ni sayansi ya upangaji vina katika midundo kuelezea maisha yanavyoendelea katika jamii, Maisha….. ni msigishano na mpambano unaoendelea kati ya miundo miwili tofauti kutafuta uwiano sahihi kama giza na mwanga, starehe na shida,
protini na wanga, majani na miiba ”.

Maneno hayo aliyatoa wakati akifanya utangulizi katika santuri ya “vina mwanzo, kati na mwisho” ya mwanamuziki Farid Kubanda maarufu kama Fid Q.

WIKIPEDIA

Katika mtandao huu, Hip Hop imeelezewa kama mfumo wa kuwasilisha mawazo kwa kutumia sanaa ya muziki ambao utamaduni wake umeasisiwa kutoka katika jamii za wamarekani weusi na walatino katika miaka ya 1970 jijini New York hususani katika South Bronx. Kwa mujibu wa mtandao huu, Hip Hop imeorodheshewa misingi mitano ambayo ni Ughanaji(mceeng), mavunjaji (break dancing), machata (graffiti) ambayo imenukuliwa toka kwa Afrika Bambaataa. Msingi wa tano unatajwa kuwa ni Mdundo kinywa (beat boxing).
 
WISEGEEK

Tovuti hii inaelezea Hip Hop ni harakati za utamaduni ambao mara nyingi huwa katika mfumo wa muziki. Utamaduni huu ulianzia Bronx katika jiji la New York katika miaka ya 1970. Utamaduni huu ulianza katika jumuiya za wamarekani weusi ukapewa mchango mkubwa na jamii za walatino katika ukuaji wake.

Utamaduni wa Hip Hop ulianza kama mtindo wa maisha uliokuwa handakini kabla ya kuibuka na kuwa moja kati ya mikondo mikuu ya maisha duniani. Mfumo huu umejipatia umaarufu mkubwa kwa kuwa umekua ukifanywa kibiashara hususani katika taifa la marekani. Hip Hop inaelezewa kama ni aina ya muziki ambayo inayohusisha vitu vingi katika uwasilishwaji wake lakini mara nyingi huwahusisha zaidi manju na mghanaji.

Katika tovuti hii imetaja nguzo za Hip Hop ni Djing, Emceeing, break dancing na sanaa ya Graffiti. Inaelezewa pia wakati mwingine Hip Hop Fashion, mdundo kinywa (beat boxing), Hip Hop Slang, Street Knowledge na Street Enterpreneurship zimekua zikiongezwa kama nguzo ya tano.

Kwa ujumla

Naweza kusema, “Hip Hop ni utamaduni ambao huegemea katika kuwianisha kwa usahihi mambo kwa kutumia zaidi kanuni za kisanaa kurahisisha milinganyo halisi inayoikumba jamii husika kwa kutoa taarifa, maarifa na njia katika kusaidia harakati za ukombozi wa tabaka fulani linalogandamizwa”.

Muasisi wa utamaduni huu anafahamika kama Clive Campbell au kwa jina maarufu kama Dj Kool Herc. Alikuwa ni manju(dj) mwenye asili ya Kijamaika aliyehamia nchini marekani katika Bronx mwishoni mwa miaka ya 1960. Asili ya utamaduni huu wa Hip Hop, unatoka kwa vijana weusi wa kimarekani pamoja na walatino walioishi Bronx katika miaka ya 1970. Kwa wengi unatambulika kuwa unatokana na wamarekani weusi kutokana na mchango mkubwa walioutoa katika jitihada za kuikuza hip hop. Licha ya kuanzishwa na watu weusi utamaduni huu wa Hip Hop unaweza kufanywa na mtu yeyote yule bila kujali itikadi za kidini, kikabila, rangi, lugha au utaifa wa mtu.

Jina la Hip Hop lilikuja miaka michache baadaye utamaduni huu ulipokomaa na kuwa mtindo rasmi wa maisha. Katika miaka ya sabini utamaduni huu uliweza kupata kufafanuliwa nguzo zake nne za mwanzo kabla ya tano kuongezeka. Kwa mara ya kwanza ziliorodheshwa na Afrika Bambaataa. Nguzo hizo zilikuwa ni Uchenguaji/ughanaji (mceing), Umanju(deejaying), mavunjanji (break dance) na machata (graffiti).

Maneno yaliyo katika maana ya Hip Hop hapo juu ukitumia mawanda mapana utagundua yana maana kubwa kama ambavyo yanavyoelezewa katika aya zinazofuata.
 
Billboard ni source makini ukitaka kupresent data za music, na hakika wamefanya research kabla ya kuja na hiyo list man.[/QUOTE]

Yeah billboard ni source makini ila bila PAC kwangu wamepoteza umakini.... Ukiichunguza hii list imekaa ki east east cost.

Sorry kwa ku qoute vibaya
 
CanXXqvUsAEmiZ_.jpg


RIP Big Pun1971 - 2000

We still remember CAPITAL PUNISHMENT
 
CTVa8H3WsAASdzr.jpg



Mama yake JCole alikuwa actress..she acted in a few local plays and shows
 
Kwa mtazamo wangu hii ndio best freestyle ever, Eminem na mwanae Proof.. Kila kitu ni freestyle kuanzia michano, body language mpaka location. Ni freestyle fupi ila ya kiufundi sana.

 
No hip hop bila PAC binafsi nimeanza sikia neno hip hop from 2pac
Mkuu ebu ona kigezo walichotumia kuipanga hiyo. List yao... Na mwaka huu nahisi watawaweka hadi Rae sraemmurd
 

Attachments

  • 1454874552984.jpg
    1454874552984.jpg
    67.6 KB · Views: 320
Tupac Amaru Shakuru.. Alibatizwa kwa jina La Lassane Parish Crooks.

Ukiongelea Hip Hop bila kutaja neno "2Pac" Ni sawa na Maisha Bila Maji... Sio kwamba utakufa ghalfa La hasha.. Utakufa, ila Baada ya Siku Chache.

Twende Mbele na Kurudi Nyuma, Pac Alikua moto nyoko balaa.. Big alikaa, Rakim and the Rest Wanakaa..

1.Tupac
2.B.I.G
3.Nas
4.Rakim Allah
5.Krs One

Huwa napenda Kuwapanga Hao watano Kama Ma Mcee wakali Wa muda wote...

Mimi huwapanga, kwa namna mashairi yao yanavyogusa jamii, namna wanavyoishii na kuutetea utamaduni wa hip hop, uwasilishaji wa kazi zao, jinsi wanavyokubalika miongoni wa wana hip hop,

1.Ready To Die
2.Ilmatic
3.All Eyez On Me

Hizi Ni Albamu bora za wakati wote za Hip Hop
 
According to billboard awa ndio mcs wakali kuwai kutokea duniani




1. BIG POPA

2. Jay Z

3. Eminem

4. Rakim Allah

5. Nas

6. Andre 3000

7. Lauryn Hill

8. GhostFace Killa

9. Kendrick Lamar

10. Lil Wayne
Kuna Kijana Anaitwa " 2pac", Kma Huyu Kijana Hayumo Kwenye Listi, Mpka Nakufa Sitaikubal Hiyo Listi..Hao Bilbord Wamechemka Au Vigezo Vyao Kma Mashindano Ya Miss TZ?? "
 
Hii thread isiwe ya kuleta majibizano yasiyo na maana watu wana mitazamo tofauti na siku zote mashindano ya nani bora huwa hayaishi ,kwenye michezo,muziki(Pele Vs Maradona,Yanga Vs Simba, Diamond vs Ali Kiba,Messi vs CRonaldo,BIG Vs 2Pac)
lakini naamini mjadala utakuwa mpana kila mtu atatoa maoni yake.Ningependa pia tujadili na Hip Hop ya hapa kwetu na changamoto zilizopo
 
album kali kila shabiki wa hip hop anatakiwa kuskiliza
nas- illmatic
lupe fiasco- food and liquor
kanye west-college drop out
jayz- the blue print
kanye west -My Beautiful Dark Twisted Fantasy
Kendrick lamaar- good kid mad city.
 
Hip Hop ni pana sana

Hip Hop ni kubwa na nzito hata special thread haitoshi kujadili hip hop

Labda muwe specific upande mmoja mnajadili hiphop music,...hiphop culture....hiphop movement au kipengele kipi??
Karibu man useme chochote kuhusu Hiphop , ni uwanja wetu wana hiphop kujidai.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom