Hillary Clinton kutembelea Kenya. Wakenya watupiga bao.

Masanja,

..angetembelea Rwanda definetely ungekuja na reaction tofauti.

..kilimo chetu hakiwezi kuendelea kwa ziara moja ya Mama Clinton.

..lakini hii ziara tells us something about kilimo na biashara ya hawa ndugu zetu Wakenya.

..tena usije ukashangaa moja kati ya bidhaa ambazo wenzetu wanauza Marekani kupitia AGOA ni Tanzanite yetu. yaani they are making more profit out of it kuliko Watanzania.

..kwamba waziri wa mambo ya Nje wa USA anatembelea Kenya na theme ya ziara yake siyo Al-Qaeda pamoja na kwamba Kenya wameshambuliwa mara mbili, au Somalia pamoja na kwamba wamepakana nayo, bali anakwenda kujadili KILIMO na BIASHARA ni suala la kuwapongeza watani wetu wa jadi.

NB:

..Obama amekwenda Ghana ku-acknowledge jinsi walivyoendesha uchaguzi wao kwa ustaarabu wa hali ya juu.

..sasa mnapowabeza Waghana mna uhakika kwamba demokrasia Tanzania iko matured kuliko ya Ghana?

Mkuu you can spin it the way you want. Tulishakubaliana kutokubaliana. Ndo maana watu kama akina Kagame wanapambana na huu mtindo wa kutembeza bakuli. I wonder whether watani wa jadi "walilalamika" Bush alivyokuja TZ akakaa four days na hakupita kwao!

I will always give credibility where it is due. Kama mtu anafanya juhudi kuwakomboa watu wake..I cant cling to the past and these stupid CNN and BBC telling me what I already know. Naona Clinton tunampa image kubwa ambayo hana in actual sense. Hizi bla bla za delegation sijui what not what..to say the least I dont subscribe to them. Do you think angekuja bongo...kingebadilika nini?

Kweli now I know..kwa nini sisi na wakenya tunaitana watani wa jadi!

Iam sorry to say..lakini mimi sioni umuhimu mkubwa sana wa Hillary kuja Tanzania. Viongozi wangapi tena wa mataifa makubwa wamekuja bongo? and what did we get?

Juzi tuli-host mkutano wa Sullivan-meeting of all meetings-am told..I dont know where we stand (by the way Jokaa Kuu..Rwanda ambao ndo ingebidi wauhost huo mkutano mwaka huu..wamechomoa kwamba ni gharama kubwa for no good reason!)

Wakuu hebu tuwe makini na tufikirie mara mbili mbili...Yaani leo..kweli taifa la vichwa million 40..bado tunasikitika kutotembelewa na Foreign minister hata angekuwa wa sayari ya Jupiter? Hivi niulize..Hillary akikutana na Kibaki ataongea naye dakika ngapi? and do you really believe that investors watakuja Kenya simply because mama Clinton kapita na delegation yake? Aliyekuwa na mpango wa kuja atakuja ambaye alikuwa hana mpango..ndo hivyo..ataenda kwingine..tuache hizi siasa za kutojiamini!

By the way..priority kubwa ya mama Clinton ni SOMALIA..Infact atakutana na raisi wa Transitional government Nairobi..na kama umeangalia US..wamedhamiria kuwasaidia hii serikali and how can you do it without Kenya in the equation?

Achana na mmarekani bwana..he knows what he wants and how to get it....Ni sisi tuu..memory span yetu ni fupi..hatuangalii mbali.

Otherwise Jokaa kuu naheshimu mijadala yako sana..ndo maana nimesikitika kuona huu mtundiko umewekwa na wewe...
 
Yaani ndio unazidi ku perpetuate falsafa yangu ya Miafrika Ndivyo Tulivyo.
Yaani it's like we can't do anything on our own bila msaada wa wazungu. Upuuzi mtupu.

Yaani huyu Joka kuu kaniudhi sana inaonyesha jinsi gani Miafrika ilivyo sasa anababaika nini? JK kaenda kuonana na Obama mkasema tumewapiga bao lakini angalia nini tumepata zaidi ya kuendelea kuishi katika dimbwi la umaskini wa kutupwa....hata angekuja hapa bongo huyo mama hakuna kitu ambacho tungefaidi.
 
Jokakuu,

Heshima mbele mwenzangu.

Hii nyuzi umeianzisha kwa madhumuni mazuri lakini watu wengi
wanatiwa kichefuchefu na hio kauli ya 'kupigwa bao'. Maybe you are
right or maybe you are wrong but I'm not going to be the judge.

Ukweli ni kwamba despite what people are trying to say, we cannot live
in isolation in this world of today. The economies are all intertwined into
one market place and it is those with an eye to take advantage of
situations who will benefit. Kama ni kumake tie na marekani to that regard
so be it. If anything the rise of the money economy in the last 4 centuries
has been set in such a way as to ensure, the 'money' doesnt leave the
hands of its inventors. Kisha you can continue form there.

Huu msafara wa Clinton will benefit Kenyan from the get go maana kuna
hela kibao wata-spend katika mahoteli and such. Kumbuka Kenya are
big on tourism and they like hosting these kind of delegations. Kisha I
believe there will be more pledges that will come up in terms of Agricultural
cooperation and trade. Agriculture and tourism have been the main stay
of the Kenyan economy for long and that is what they are banking on on
this trip. Kisha nasikia tetesi kua Kenya is set to build the biggest windfarm
in Africa...these were part of Obama's policies when campaigning. Kwamba
the world has to look for alternative sources of energy and get
away from the dependence on oil. Huoni kama hapo kuna mtu Kenya
ameona mbele akijua kwamba with such a project, funding will be highly
likely from the donors.Na Bongo je?...watu ni ziiiiiiiii!!!

Obama might have snubbed Kenya on the first trip to Africa but mtu
asijidanganye kua huyu jamaa does not think about Kenya. He has his
family there na anajua Raila should have been the President of Kenya right
now had Kibaki not stolen the election. It is this muddy situation that he
does not want to wade in lakini atawatuma mawaziri wake ku-make sure
Kenya has a chance to compete on the global market when it comes to
trade.Kikwete might have been the first African visitng head of State to
meet with Obama, lakini usidhani kua jaluo hajua kua nyumba ya JK imejaa
fisadis left, right and center.

Kwa hivyo hio kauli ya kupigwa bao might be misplaced but with time I
believe you will be vindicated.

Regards.
 
Last edited:
Jibu la haraka ni hapana. Nitakusimulia kisa kimoja. Alipokuja rais Kikwete NY 2006 kuna dada mmoja ambaye wazazi wake walimehamishwa ili Barrick ichimbe dhahabu huko Mara alisimama kuuliza swali. Alieleza kuwa wazazi wake wamekuwa na shamba hilo miaka nenda rudi na sasa wanahamishwa. Rais alimjibu kuwa afadhali dhahabu ichimbwe kuliko kilimo. Sasa unadhani huyu akisema kilimo ni uti wa mgongo anaaminika?

This is very sad to say the least. Huyo mwanadada, je walipata
compensation for being relocated?..and if so walifikiaje uamuzi wa bei?
 
Maybe you are right or maybe you are wrong but I'm not going to be the judge.

Kwa hivyo hio kauli ya kupigwa bao might be misplaced but with time I believe you will be vindicated.

Angalia watu wasiojua kujieleza hawa! Mara kasema hatoi hukumu, kafika mwisho wa senti mbili zake kasahau alichoanza nacho, kam support Jokakuu na lugha za "kupigwa bao" eti kwa vile Mzungu anakwenda Kenya. Lugha za mashambani za watumwa wa tumbaku karne ya 17 kusini mwa Marekani. Mzungu akikukubali basi unafurahi, plantation mentality.

Watumwa wenzako wakikwambia tutafute njia za kujikomboa, tutoroke hapa shambani kwenye maisha tegemezi ya kitumwa haya, unamuuliza tutoroke twende wapi, kuna nini duniani cha zaidi ya hapa shambani? Unaenda kumripoti mwenzio kwa bwana, anachapwa mikia ya taa mpaka anakufa. Kisa, unaishi ndani ya kathri la Mwinyi Fuadi, umeridhika, unatupiwa tupiwa mabaki ya mezani kama mbwa, unalala kwenye dari, au chini ya nyumba kwenye mabomba ya maji machafu. Mara moja moja, bwana wa watwana anamjamia mkeo kwa nguvu, unalia, unanyamaza, unataka utumwa. Omba omba. Unakula mbuzi unalipa ng'ombe, unafikiri unapendwa.

Unataka USA akupende, "acknowledge." Msituambia "tumepigwa bao," pigweni bao wenyewe na Wazungu hao.

..leo wanasikia Kenya wamechangamka kuliko sisi, na wanakuwa acknowledged na USA
 
l dont share the same opinion with those who think hillary clinton going to key is a point to think that kenya is in any advantage over Tanzania, first we need to think of the reasons beahind such trips, and always remember that the americans have samething potential behind each and everything they do, so let concentrate on our national goal and builb our nation with our hands

sirily mtui
 
Angalia watu wasiojua kujieleza hawa! Mara kasema hatoi hukumu, kafika mwisho wa senti mbili zake kasahau alichoanza nacho, kam support Jokakuu na lugha za "kupigwa bao" eti kwa vile Mzungu anakwenda Kenya. Lugha za mashambani za watumwa wa tumbaku karne ya 17 kusini mwa Marekani. Mzungu akikukubali basi unafurahi, plantation mentality.

Watumwa wenzako wakikwambia tutafute njia za kujikomboa, tutoroke hapa shambani kwenye maisha tegemezi ya kitumwa haya, unamuuliza tutoroke twende wapi, kuna nini duniani cha zaidi ya hapa shambani? Unaenda kumripoti mwenzio kwa bwana, anachapwa mikia ya taa mpaka anakufa. Kisa, unaishi ndani ya kathri la Mwinyi Fuadi, umeridhika, unatupiwa tupiwa mabaki ya mezani kama mbwa, unalala kwenye dari, au chini ya nyumba kwenye mabomba ya maji machafu. Mara moja moja, bwana wa watwana anamjamia mkeo kwa nguvu, unalia, unanyamaza, unataka utumwa. Omba omba. Unakula mbuzi unalipa ng'ombe, unafikiri unapendwa.

Unataka USA akupende, "acknowledge." Msituambia "tumepigwa bao," pigweni bao wenyewe na Wazungu hao.

DAMN...... AB-tichaz just got ethered, go get yo A game AB, these young guns should know how to respect their ''elders''.
 
Nyani,
I really wish we were doing our thing kivyetu. The problem is we are doing nothing. We are just reacting, copying, cutting, and pasting. Soma ile post ya Rev. Kishoka jinsi Tz ilivyoamua kutoa stimulus package kwa kampuni ambazo hazifanyi kitu then you will see what I am saying. I wish we were really doing something. I would have been a very proud Tanzanian.

We?
If you are not doing anything Jasusi, there is one thing that you need to have it with you - a mirror!
 
This is very sad to say the least. Huyo mwanadada, je walipata
compensation for being relocated?..and if so walifikiaje uamuzi wa bei?
The answer is no. Na hata kama Barrick walitoa malipo nadhani yaliishia mifukoni mwa wakubwa. Nakumbuka kule Bulyankulu kuna wakati nilifuatilia hali ya wale small miners waliokuwa displaced nikagundua kuwa Barrick walilipa compensation kwa serikali ili wawagawie lakini fedha hazikurudi kutoka Dar. It is very sad indeed. Ndiyo Tanzania yetu hii ya kasi mpya.
 
Angalia watu wasiojua kujieleza hawa! Mara kasema hatoi hukumu, kafika mwisho wa senti mbili zake kasahau alichoanza nacho, kam support Jokakuu na lugha za "kupigwa bao" eti kwa vile Mzungu anakwenda Kenya. Lugha za mashambani za watumwa wa tumbaku karne ya 17 kusini mwa Marekani. Mzungu akikukubali basi unafurahi, plantation mentality.

Watumwa wenzako wakikwambia tutafute njia za kujikomboa, tutoroke hapa shambani kwenye maisha tegemezi ya kitumwa haya, unamuuliza tutoroke twende wapi, kuna nini duniani cha zaidi ya hapa shambani? Unaenda kumripoti mwenzio kwa bwana, anachapwa mikia ya taa mpaka anakufa. Kisa, unaishi ndani ya kathri la Mwinyi Fuadi, umeridhika, unatupiwa tupiwa mabaki ya mezani kama mbwa, unalala kwenye dari, au chini ya nyumba kwenye mabomba ya maji machafu. Mara moja moja, bwana wa watwana anamjamia mkeo kwa nguvu, unalia, unanyamaza, unataka utumwa. Omba omba. Unakula mbuzi unalipa ng'ombe, unafikiri unapendwa.

Unataka USA akupende, "acknowledge." Msituambia "tumepigwa bao," pigweni bao wenyewe na Wazungu hao.

Oh, Dilunga!
JF would never be the same without you.
 
hapa hakuna kupigwa bao mazee, kwani ataleta nini cha ziada?so alipokuja clinton, bush, mke wa bush tumewazidi nini wakenya? au ndo mentality kuwa kaj mzungu kwao kawaletea mizawadi kibao!! poor tzs, hatuwazi ya maana tunawaza kuletewa duh!aje asije kama hatjabadili attitude hasasidii lolote,mbona hawaendagi iran lakini wairan wametuzidi?tena far away?huyo mtoa mada najisikia aibu kwa senior kama yeye!!labda hajala mchana km yupo tz mwoneeni huruma
 
Masanja said:
Mkuu you can spin it the way you want. Tulishakubaliana kutokubaliana. Ndo maana watu kama akina Kagame wanapambana na huu mtindo wa kutembeza bakuli. I wonder whether watani wa jadi "walilalamika" Bush alivyokuja TZ akakaa four days na hakupita kwao!

I will always give credibility where it is due. Kama mtu anafanya juhudi kuwakomboa watu wake..I cant cling to the past and these stupid CNN and BBC telling me what I already know. Naona Clinton tunampa image kubwa ambayo hana in actual sense. Hizi bla bla za delegation sijui what not what..to say the least I dont subscribe to them. Do you think angekuja bongo...kingebadilika nini?

Kweli now I know..kwa nini sisi na wakenya tunaitana watani wa jadi!

Iam sorry to say..lakini mimi sioni umuhimu mkubwa sana wa Hillary kuja Tanzania. Viongozi wangapi tena wa mataifa makubwa wamekuja bongo? and what did we get?

Juzi tuli-host mkutano wa Sullivan-meeting of all meetings-am told..I dont know where we stand (by the way Jokaa Kuu..Rwanda ambao ndo ingebidi wauhost huo mkutano mwaka huu..wamechomoa kwamba ni gharama kubwa for no good reason!)

Wakuu hebu tuwe makini na tufikirie mara mbili mbili...Yaani leo..kweli taifa la vichwa million 40..bado tunasikitika kutotembelewa na Foreign minister hata angekuwa wa sayari ya Jupiter? Hivi niulize..Hillary akikutana na Kibaki ataongea naye dakika ngapi? and do you really believe that investors watakuja Kenya simply because mama Clinton kapita na delegation yake? Aliyekuwa na mpango wa kuja atakuja ambaye alikuwa hana mpango..ndo hivyo..ataenda kwingine..tuache hizi siasa za kutojiamini!

By the way..priority kubwa ya mama Clinton ni SOMALIA..Infact atakutana na raisi wa Transitional government Nairobi..na kama umeangalia US..wamedhamiria kuwasaidia hii serikali and how can you do it without Kenya in the equation?

Achana na mmarekani bwana..he knows what he wants and how to get it....Ni sisi tuu..memory span yetu ni fupi..hatuangalii mbali.

Otherwise Jokaa kuu naheshimu mijadala yako sana..ndo maana nimesikitika kuona huu mtundiko umewekwa na wewe...

Masanja,

..ziara ya Mama Clinton Kenya inahusu KILIMO, AGOA,na Somalia.

..tunaelewa kwamba Somalia inapakana na Kenya, kwa hiyo suala lao tuliweke pembeni kwa sasa hivi.

..kuna sababu zinazomfanya mama Clinton akazungumzie masuala ya KILIMO na BIASHARA/AGOA Kenya na siyo Rwanda,Uganda,Tanzania, etc.

..binafsi naendelea kusisitiza kwamba Kenya wamejipanga na kuitumia vizuri fursa ya AGOA na ndiyo maana mama Clinton anawafuata kwao kuzungumzia kilimo na biashara.

..nadhani kuna funzo toka kwa watani wetu wa jadi kwamba siyo lazima nchi za Kiafrika tutembeze bakuli siku zote.

..Tanzania tuna ardhi kubwa na yenye rutuba kuliko Kenya. population yetu ni zaidi yao. tuna vivutio vingi zaidi vya utalii kuliko Kenya. tuna utajiri mkubwa wa rasilimali mfano madini kuliko Kenya.

..pamoja na vigezo vyote hivyo kwanini Kenya wana-export zaidi kwenda USA na kutuzidi Watanzania na nchi nyingine majirani?

..nakuomba uangalie data za biashara kati ya USA na mataifa ya Afrika. bonyeza hapa . linganisha data za Kenya vs Tanzania halafu nieleze kama pamoja na resources tulizonazo if that is something to be comfortable with.

..samahani lakini nadhani hapa Wakenya "wametupiga bao" na hii ziara ya mama Clinton ni uthibitisho wa ukweli huo.
 
Babuyao said:
Siyo kwamba hatuoni umuhimu wa ziara hiyo. Bali kinachokera ni kule kusema "Kenya wametupiku" eti kwa kuwa wametembelewa na hao waheshimiwa. Hakuna tofauti na namna walivyo-react wakeny aKikwete alivyokuwa wakwanza kufika white house kabla ya mwai kibaki. Nao walismema Tz wametupiku. Ni mawazo ya kitoto. Kana kwamba maendeleo yetu yanaletwa na hao bila sisi kufanya kazi. Tukisema "kenya wanatupiku" tuseme tukionesha walivyopiga maendeleo makubwa, siyo kwa kutemebelewa na jamaa wa marekani. Hayo ni mawazo mufilisi sana.

Babuyao,

..nimeitikia wito wako wa kuleta data za biashara kati ya USA na mataifa ya Kiafrika.

..watani wetu wa jadi "wametupiga bao" kwasababu wao wana-export zaidi kwenda USA wakati wana rasilimali chache na population ndogo kuliko Tanzania.

..zaidi KENYA WANAEXPORT TANZANITE KULIKO TANZANIA. inasemekana Tanzanite inakaribia kuisha na hawajamaa wamefaidika nayo kuliko Tanzania.

..data za biashara kati ya USA na Afrika zinapatikana hapa

NB:

..hapo juu naomba isomeke Kenya wana-export thr' official channels tanzanite nyingi kuliko Tanzania. mchangiaji Dilunga ndiyo wa kwanza kuona makosa hayo na amenielekeza ktk posting yake.
 
Last edited:
..zaidi KENYA WANAEXPORT TANZANITE KULIKO TANZANIA. inasemekana Tanzanite inakaribia kuisha na hawajamaa wamefaidika nayo kuliko Tanzania.

Nisaidie kuelewa. Hiyo Tanzanite wanayo export Kenya inatoka wapi?
 
Dilunga said:
Nisaidie kuelewa. Hiyo Tanzanite wanayo export Kenya inatoka wapi?

Dilunga,

..samahani kwa usumbufu.

..nilipaswa kuongeza maneno 'thr' official channels'.

..source ya tanzanite ni Tanzania, lakini inapelekwa Kenya kwa magendo halafu wao wana re-export officially kwa bei nzuri na faida kwa taifa lao kuliko Tanzania.

..again, asante...good observation.
 
Back
Top Bottom