Hili tukio limenigusa sana: Bibi kizee wa miaka >100 abakwa kwa zaidi ya masaa 8!!

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Wiki hii nimekutana matukio mawili ambayo pamoja na umri wangu huu yamenitoa machozi. Tukio mojawapo ni hili la bibi kizee mwenye umri wa miaka zaidi 100 kubakwa kwa zaidi ya saa 8 (hadi usiku wa manane) na kutelekezwa bila matibabu.

Tukio hili limetokea hivi karibuni huko Nzega, Tabora; katika kijiji cha Mwantoba, kata ya Bukene na kuripotiwa na Pendo Omary katika gazeti la Dira ya Mtanzania la 21-23 Novemba 2011. Bibi huyo amepata maumivu makali ya kifua, sehemu za siri na pia alichomwa na mti kwenye mguu. Mbaya zaidi ndugu na jamaa zake wamekosa shilingi 25000 (elfu ishirini na tano tu) kwa ajili ya kumpatia matibabu. Pia polisi wamekataa kumchukulia hatua mbakaji na pia uongozi wa kijiji nao hauna mpango wa kumsaidia huyu bibi ingawa mhusika yuko pale pale kijijini anatanua!!

Hili tukio si tu limenigusa bali limenisababishia kero ya aina yake kwa kuona jinsi ambavyo watu waliopewa dhamana ya kusimamia uhai na maslahi yetu wanavyofurahia mateso ya bibi, mama, dada na ndugu zetu wengine.

Kwa wale ambao watapenda kumsaidia huyu bibi walau apate matibabu au msaada wa kisheria, wawasiliane na Mhariri wa gazeti (Dira ya Mtanzania, 0655 063 839 au diramtanzania@yahoo.com) au mwandishi mwenyewe (Pendo Omary, 0716 3728 07 au Ommygarl@yahoo.com).
 
Mmmh, mbakaji alikuwa binadamu mmoja au walikuwa wengi?

Ni mtu mmoja tu..Inasemekana alimkuta bibi anatoka chooni usiku na kwa vile haoni vizuri, akajidai kumsaidia. Katika huo mchakato akampeleka kichakani kuanza kumbaka kuanzia mida ya saa 4 hadi aliposikia jogoo anawika.

Si tu kwamba alimbaka, ila pia alimpiga sana na kumuumiza kifua kwa kumlalia!!

Hata sikuamini kama nilisoma story ya kweli!!

Kweli dunia ya sasa ni bangi tupu!
 
dah nahisi kuna ushirikina ndani yake
huyo bibi pole zake na tumsaidieni jamani...
so sad ,tunakuwa wanyama sasa
 
dah nahisi kuna ushirikina ndani yake
huyo bibi pole zake na tumsaidieni jamani...
so sad ,tunakuwa wanyama sasa

Ahsante The Boss,

Kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo na imani za kishirika katika hili tukio!

Natamani watu wengi wangejitokeza kumsaidia huyu bibi.. Lakini pia natamani wadau wa kutetea wanyonge wangejitokeza kushinikiza mbakazi achukuliwe hatu na polisi + viongozi wa kijiji ambao wanaonekana kumkingia kifua huyo mhalifu asiye nahuruma!!
 
Maskini bi kizee wa watu! Hilo jitu lazima litakuwa ligonjwa la akili tu manake haiwezekani kabisa mtu mwenye akili timamu kumlala bi kizee mwenye umri huo achilia mbali kumbaka. Yaani hata puli inavutia mara 100 zaidi ya huyo bi kizee.

Sasa mtu na akili zako timamu eti umbake bi kizee? Haiwezekani. Ana hitilafu kubwa kichwani huyo mwanakharamu.
 
jamani sorry lakini nimejikuta najiuliza kitu kuhusu wanawake...hapa..

kama bibi kizee wa miaka 100
ana survive sex ya masaa nane....

na hawa vijana wanapojifanya 'wamechoka' na dakika kadhaa je?
na vidume vinavyojisifia na saa nzima????kwa wadada ambao ni very young?
vinajidanganya sio?????lol
 
Maskini bi kizee wa watu! Hilo jitu lazima litakuwa ligonjwa la akili tu manake haiwezekani kabisa mtu mwenye akili timamu kumlala bi kizee mwenye umri huo achilia mbali kumbaka. Yaani hata puli inavutia mara 100 zaidi ya hata huyo bi kizee.

Sasa mtu na akili zako timamu eti umbake bi kizee? Haiwezekani. Ana hitilafu kubwa kichwani huyo mwanakharamu.

Dunia hii imekengeuka ndugu yangu,

Najaribu kumfuatilia mwandishi anitumie makala yote niibandike hapa...Nikifanikiwa nitaiweka!

Bibi kizee aliongea maneno mazito sana ambayo nilitegemea yangemfanya mbakaji si kumwacha bibi wa watu bali pia kumrudisha nyumbani kwake..Alimwambia kwamba, "na uzee wangu huu, ngozi imenikauka na kusinyaa, umevutiwa na nini mwanangu hadi unifanyie unyama huu"...Badala ya kuyasikia hayo maneno yanayochoma, jamaa alipandisha mori zaidi, kumziba mdomo, kipigo juu na kuendelea na kumbaka!

Picha ya huyo bibi kizee itachukua muda kunitoka kichwani!
 
Duh! hao jamaa walikuwa na Lager ngapi kichwani mpaka waone wamuone bibi bado kigoli. hizo zitakuwa imani za kishirikina tu.
 
jamani sorry lakini nimejikuta najiuliza kitu kuhusu wanawake...hapa..

kama bibi kizee wa miaka 100
ana survive sex ya masaa nane....

na hawa vijana wanapojifanya 'wamechoka' na dakika kadhaa je?
na vidume vinavyojisifia na saa nzima????kwa wadada ambao ni very young?
vinajidanganya sio?????lol

Mhhhh Mkuu,

Umefikiria nini hadi unafika huko...Anyway, hilo nalo ni mjadala unaojitosheleza...
 
He is psycho...

Bibi yangu yu hai mpaka leo na ana miaka karibia 100 hata kushuka kitandani ni kazi anaona kama anatumbukia kwenye shimo. sasa na-imagine mtu kama huyo amtokee bibi yangu ambake kwa masaa 8??? Vitu vingine ni laana na dhambi zisizosameheka kwa kweli mbele ya Mungu na mwanadamu.
 
Maskini bi kizee wa watu! Hilo jitu lazima litakuwa ligonjwa la akili tu manake haiwezekani kabisa mtu mwenye akili timamu kumlala bi kizee mwenye umri huo achilia mbali kumbaka. Yaani hata puli inavutia mara 100 zaidi ya hata huyo bi kizee.

Sasa mtu na akili zako timamu eti umbake bi kizee? Haiwezekani. Ana hitilafu kubwa kichwani huyo mwanakharamu.

...umeona ee? halafu imagine masaa yote hayo, khaaa? kwa raha gani?!
mgonjwa wa akili huyo, akiachiwa atambaka hata mke wa mwenyekiti wa kijiji...!

ila nimesikitishwa na kukosekana shs 25,000/= tu za kumsaidia huyo bi kizee....dahhh?
hata mwandishi wa nakala hii kashindwa jitolea kweli?....
 
Sasa bi kizee na mambo ya lubrication sijui ilikuwaje tu.
 
...umeona ee? halafu imagine masaa yote hayo, khaaa? kwa raha gani?!
mgonjwa wa akili huyo, akiachiwa atambaka hata mke wa mwenyekiti wa kijiji...!

ila nimesikitishwa na kukosekana shs 25,000/= tu za kumsaidia huyo bi kizee....dahhh?
hata mwandishi wa nakala hii kashindwa jitolea kweli?....

Unaweza kuwa sahihi kabisa,

Kwa mujibu wa mwandishi, inaonekana jamaa anaweza kuwa serial rapist.. Mwandishi alielezwa kuwa mbakaji alionekana pale kijijini siku moja kabla ya mwandishi kukutana na mwenyekiti wa kijiji na alikuwa amemba mwanamke mlemavu kwenye baiskeli. Mwandishi anasikitika sana kwamba huyo jamaa inawezekana ni mbakaji mzoefu na anawalaghai wanawake wasiojiweza!

Kuhusu hiyo 25000/=, sina hakika kama mwandishi alishindwa kutoa ila wanaomba michango ya wasamaria wema kwani bado bibi kizee anahitaji msaada zaidi! Pia mwandishi alisafiri kutoka Dar hadi Nzenga. Huo nadhani pia ni mchango mkubwa sana!
 
Back
Top Bottom