Hili Suala la Mto Tigite limeishia wapi jamani?

Kiresua

JF-Expert Member
May 13, 2009
1,184
259
WanaJukwaa,

Poleni kwa majukumu yenu ya kila siku,

Muda mfupi uliopita nilikuwa naangalia kipindi maalum kilichokuwa kinarushwa na runinga ya MLIMANI kwa ushirikianao na Jumuiya ya Makanisa CCT kuhusu wananchi walioathirika na madhara ya sumu iliyokuwa ikivuja kutoka mgodi wa madini unaomilikiwa na Kampuni ya Madini ya Barrick kwnye mto TIGITE. Ilitia simamzi sana kuona jinsi watu walivyoathirika na wengini kupoteza maisha, mifugo kufa achilia mbali viumbe wa majini (kwani hakuna kuimbe kilicho himili sumu ile) na hata sasa hali bado ni tete(?)

Waziri Kagasheki aliwahi kutembelea akadanganywa, na akagundua amedanganywa akawaka sana... na kilichooendelea makijua wenyewe. Muungano wa dini nao ulitembelea waathirika na kupandekeza kwa serikali lakini Mhhh jamani wamepuuzwa na hawa PIA!! Mwaka jana Kuna Mbunge aliuliza swali Bungeni ni Hatua zipi serikali ilizichukuwa ikiwepo kulipa fidia walioathirika kama sheria za madini zinavyotaka.. Kwa masikitiko waziri alijibu hakuna tathmini iliyokwisha fanyika kuhusu watakaolipwa fidia (in 3 yrs period??) serikali haiwajali watu wake???? aahhhh!!!! (hata kama mgodi ni wa Bush? lakini sio hivi) ipo siku mtalipa kwa kwa kuwakosea watu wetu haki yao-mnafikiri Mungu alikosea kuwaweka Tanzania? your days are numbered!!

Kwa kuona hii jitihada ya MLIMANI TV na CCT, nikaona siwezi kuliacha lipite unnoticed/unattended. we have to speak about this again and again and again!!! Tutimize wajibu wetu, wadau hata kama watawala watafunga masikio wasisikie tuandelea kusema, HAMTENDEI HAKI WATANZANIA. Dr Mwakyembe amegusishwa kitambaa tuu dunia nzima ilijua na kusema, waandishi wote wnannadika habari yakehadi leo... jee mwannchi wa Tarime (a VOICE LESS) nani anayemsemea kama si mm na wewe!!?

CDM na vyama vingine, CSOs, Wanaharakati, LHRC na wengine mko wapi!!?? jamani hata kama lilikwisha kuzungumzwa hapo nyuma, lakini tuwaunge mkono kuliibua tena hili suala

Naomba kuwasilisha
 
Si kwamba maji ya sumu yanavuja.

Maji ya sumu yanaachwa kwamakusudi kutiririka katika mto kwa sababu ni Utamaduni wa Barrick gold Mine kuto jari mazingira na maisha ya watu katika nchi zote wanakochimba dhahabu isipokuwa USA.

Serikali inajua kwa undani tatizo hilo lakini haiwezi kulishighulikia hata siku moja kwa sababu ni moja kati ya mambo waliyojifunga katika mkataba haramu kule hotelini.Rais Kikwete na viongozi wa juu serikai Wali kura Rushwa ili Barrick Goldmine waachwe wafanye kile kinacho wapa faida bila kubughudhiwa.

Barrick Goldmine wanachimba dhahabu hapa Marekani na wanatumia Technolojia hiyo hiyo wanayoitumia Tanzania kuchuja dhahabu lakini hapa USA kamwe hawawezi kuachia maji kuingia katika mito bila kuiondoa sumu kwanza. Vile vile serikali huwalazimisha kueleza waziwazi utaratibu wanao tumia kuondoa sumu hiyo.

Hata aende nani huko TIGR River Barrick Gold Mine wataendelea kumwaga sumu hiyo katika mto Tigite vile wapendavyo.
viongozi wa serikai yetu wamewekwa katika viganja vya Barrick Gold mine.
 
Kiukweli yapo mambo mengi tu ambayo hayako sawa kwa sera nzima ya madini, ndio maana inazaliwa mikataba isiyojali kabisa wenyeji hata serikali yao. Madhara ya "wawekezaji" a.k.a. wezi, yapo kwenye maeneo karibu yote yenye migodi ingawa viwango vya madhara vyatofautiana.

Kwa hilo la Mto Tighite lilishaongewa sana, kama ni kuchukua hatua zingepaswa kuwa zilishachukuliwa kitambo. Unapofika kwenye point kama hii ndio Watz sasa wachanganye na akili zao kama ilivyokwishaelezwa. Sijui sirikale haina hela au sijui haipati kitu kutokana na mgodi huo (kwa mujibu wa mkataba ambao umegongwa muhuri wa "top secret"), au ni ulevi wa viongozi wetu wanaosafiri na dola, laptop 3, smg & pistol, na passport 2 japokuwa safari ni ya mumu humu nchini isiyovihitaji vyote hivyo.

Pengine tuombe utokee uchaguzi mdogo pande zile za Tarime, labda wahanga wanaweza lipwa/fidiwa chap chap, manake kipaumbele ni chama kwanza, halafu wananchi waliokipigia kura za "kishindo" baadaye!
 
Back
Top Bottom