Hili ndilo vazi la Taifa

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Wadau wa JF
kwa kuanzia tu maoni yangu ni kama yaonekanavyo ktk picha hapo chini
ibra.jpg ibra1.jpg
Vazi la Taifa liwe kama lionekanavyo ktk picha hapo juu

KARIBUNI WENYE MAONI
 
Kama kweli hilo ndilo vazi la Taifa basi tuna matatizo makubwa! Kwa vipi hicho kizibao kiwe vazi la wamasai, wabena, wakwere, wachaga, wapare waluguru etc? Na litavaliwa wapi? Mshono wake (hasa shingo) unatafauti gani na kaunda suti za Mwl. Nyerere, Mzee Malecela na wengine? Tofauti hapa ni rangi na hiyo picha ya twiga.

Kwa maneno mengine concept ya hicho kizibao hakina tofauti na masharti ambayo yamekuwa yanavaliwa na wananume kama sehemu ya vazi la taifa. Sasa kulikuwa na haja gani kuunda tume just kubadilisha rangi? Wanawake nao watavaa hicho kizibao?
 
sasa hiyo kaunda suti ndo waliokuwa wanajadiliana kila siku na kupeana posho kazi kweli kweli.....
 
Sioni umuhimu wa hilo vazi,nadhani tuna mambo mengi zaidi ya kufanya zaidi ya kukaa na kulipana mabilioni kwa vazi ambalo hata nikilivaa halitanifaidisha kitu."ni maoni yangu tu haya".
 
Kama kweli hilo ndilo vazi la Taifa basi tuna matatizo makubwa! Kwa vipi hicho kizibao kiwe vazi la wamasai, wabena, wakwere, wachaga, wapare waluguru etc? Na litavaliwa wapi? Mshono wake (hasa shingo) unatafauti gani na kaunda suti za Mwl. Nyerere, Mzee Malecela na wengine? Tofauti hapa ni rangi na hiyo picha ya twiga.

Kwa maneno mengine concept ya hicho kizibao hakina tofauti na masharti ambayo yamekuwa yanavaliwa na wananume kama sehemu ya vazi la taifa. Sasa kulikuwa na haja gani kuunda tume just kubadilisha rangi? Wanawake nao watavaa hicho kizibao?

sema wewe unataka iweje? lete maoni yako kama hutaki kuleta maoni hilo ndilo litakuwa vazi la taifa kama likipitishwa
 
Sioni umuhimu wa hilo vazi,nadhani tuna mambo mengi zaidi ya kufanya zaidi ya kukaa na kulipana mabilioni kwa vazi ambalo hata nikilivaa halitanifaidisha kitu."ni maoni yangu tu haya".

vazi la taifa lina umuhimu wake bwana,hususani ktk mambo yanayohusu muunganiko wa mataifa mbarimbari,ni vyema ukatinga vazi la Taifa lako kwa kutangaza utamaduni na mila zenu

kwa wale wanaopata nafasi ya kwenda nje ya nchi na kuishi ama kusoma huko wao wanaelewa umuhimu wa kuwa na vazi la Taifa hususani ktk zile sherehe za siku ya africa na wakati wa kuonyesha mavazi ya nchi husika,watu kutoka Tz huvaa Kimasai sasa sielewi je vazi la kimasai ndilo vazi la Taifa letu? na ukizingatia wamasai wengi wanatoka kenya
 
utaifa (utanzania) wa hili vazi uko wapi? Labda bendera na twiga. Kwa mawazo yangu vazi la taifa linge-reflect mavazi na mishono ya asili ya makabila yetu. Wangefanya ubunifu (wa kuchanganya) staili za mavazi na uvaaji walau wa makabila fulani na kutoka na kitu kinachoonekana kipya lakini chenye kuakisi utanzania fulani. Mfano vazi au uvaaji wa kimasai, kisukuma, kigogo, kimakonde, nk ungefanyiwa stadi na kutoka na vazi maridadi. Tuna uvaaji wa kiasili mzuri sana mf. lubega, kikoi, kaniki, nk. Kwa hiyo licha ya matirio ya vazi lilitakiwa mf. livaliwe kama lubega, kikoi au kaniki.
 
sema wewe unataka iweje? lete maoni yako kama hutaki kuleta maoni hilo ndilo litakuwa vazi la taifa kama likipitishwa

@engmtolera, watu wamejadili sana hapa kuhusu vazi la taifa.
Kaunda suti inajulikana ndio vazi la taifa na hata viongozi wengi wamekuwa wanavaa hivyo. Ukiwa mahali popote duniani ukakutana na mwanaume (mwafrika) amevaa kaunda suti uwezekano mkubwa atakuwa mtanzania. Ni vazi lenye historia na harakati za siasa hasa ideology ya ujamaa na kujitegemea. Sina hakika kwa nini wanabuni kitu kingine? Wanataka nini?

Kwa wanawake, kanga inajulikana. Na sio tu kwamba kanga ni kitambaa lakini ili iwe kanga lazima iwe na misamiati ya kiswahili. Kwa maneno mengine kanga inatengenezwa kwa kuzingatia utamduni wa kiswahili. Na ni mtu mwenye kujua kiswahili tu ndio ataelewa kini kimeandikwa kwenye kanga. Kama ilivyo kaunda suti, kanga ina historia katika 'utu wa mwanamke wa kiswahili'. Tofauti na kitenge ambacho kinavaliwa kwa nchi mbalimbali Afrika, ni Tanzania peke yao wanaoweza ku-claim kuwa kanga ni yao. Kenya na hata Uganda wanafuata lakini asili ya kanga ni Tanzania. Sasa kwa nini tunakwenda kwenye hiyo kaniki yenye picha ya twiga?

Ni vizuri ndugu engmtolera kutambua kuwa vazi la taifa haliji kwa kubuniwa tu, linakuwa na historia na jamii husika. Nilipoona hicho kizibao nimeshtuka sana kwa sababu sioni kwa jinsi gani linagusa utamaduni wa mtanzania. Linamhusu mtanzania kwa vipi? Ukiangalia bungeni utaona wabunge na viongozi wengine kama mawaziri wamevaa kaunda suti. Kenya wanavaa suti za kizungu, sisi tayari tunalo vazi letu tunataka nini tena? Au hicho kizibao cha kaniki kinamfanya mtu apendeze (smart) zaidi kuliko kaunda suti?
 
Mbona linataka kufanana na la wanigeria, au mi macho yangu.
 
Kwa hiyo kitu chochote kikichorwa twiga ndio kinawakilisha tanzania? Acheni upuuzi nyie...
Mnatafuta namna ya kula hela za walalahoi tu!!!!! Hatuna hitaji hilo..tunahitaji, huduma bora za afya, maji, barabara, elimu bora, ajira kwa vijana, umeme wa uhakika etc...huu mnaofanya ni upumbavu mtupu!!!!
 
Wakuu hiyo mbona ni kopy and pest ya Nigeria? hapo ni nembo ya twiga tu imebandikwa, na huu mchakato umeghalimu fedha za kutosha,

Na wakisha kaa sana watakuja na mchakato wa kutafuta kiatu cha taifa ili muradi watu watafute njia za kula na badae wataleta mchakato wa kutafuta chupi ya taifa
 
Vazi la taifa halipangwi, linaibuka spontaneously. Habari za kupangiana mavazi zilipitwa na wakati tangu kuanguka kwa ukoministi.

Halafu kwa nini tuwe na vazi la taifa na sio mavazi ya taifa? Mmasai na lubega yake tayari anajulikana kimataifa, kwa nini atafute vazi jingine?

Tulishabonda hapo chini

Vazi la Taifa kwa kamati, imla iso tamati
 
Back
Top Bottom