Hili litawashangaza wanawake………!

...mtambuzi acha kuwatisha wake zetu bana, wikiendi inaharibika huku mkuu!
 
Mwanaume pedezyee anatia presha sana tu, wengi wao ni vicheche balaa, wengine wanafundishwa ukicheche na mapedezyee wenzao.
 

hahaha...she's you biggest fan, eti kila siku lazima akusome!...haya bana...

Kuna wakati naweka thread za kuwapiga virungu wanawake humu JF, Je huzichukuliaje?.............. Nadhani huo ndio wakati wako wa kumgeuzia kibao.........LOL
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mtambuzi,

Tunaomba utupe link inayotupeleka kwenye report ya huo utafiti! Lengo la utafiti ilikuwa ni nini? Acheni uzushi na kujilisha upepo. Tabia mbaya kama mnazo msitumie JF kuhalalisha uozo wenu na kuwabambikia watu wote, eti utafiti umefanyika!!
 
Ni jambo ambalo litawashtua wanawake, hasa walioolewa au ambao wana wapenzi wanaoaminika, kwamba, kila wanaume kumi ambao unakutana nao kila siku, watano kati yao ni lazima wameshakutana na kufanya mapenzi na wanaoitwa makahaba. Ni wepi watano kati ya hao kumi, ni jambo lenye kushangaza zaidi. Unaweza kuhisi kwamba, kati ya hao kumi, ni wale wanaume wahuni na chakaramu, ndio watakaokuwa wamekutana kimwili na makahaba……… Umekosea!

Kwa kawaida kati ya hao kumi, watano ambao watakuwa wameshatembea na makahaba watakuwa ni wale ambao huwezi kuwategemea. Kwa nini? Kwa sababu ni wale wenye kujiheshimu kwa nje, wenye uwezo na pengine waliosoma vizuri. Hapa hata hivyo tunazungumzia makahaba ambao wanajiuza kwa kiwango kinachoweza kukubalika kwa watu wengi wakiwemo wageni kutoka nje. Wale makahaba kama wa Uwanja wa Fisi au Kimboka pale Buguruni hawahesabiwi kama makahaba katika viwango vya kiutafiti kama huu uliofanywa duniani kote.

Kahaba kwa kawaida huhitaji fedha na pengine mahali pa kwenda kufanyia mapenzi na hili linawezekana kwa mwanaume mwenye uwezo kifedha. Kwa hali hiyo, watano kati ya hao wanaume kumi ni lazima wawe ni wale wenye uwezo mzuri kifedha. Kuna tafiti zinazoonesha kwamba, wanaume wanaochukua makahaba angalau mara moja kwenye maisha yao, ni zaidi ya watano kati ya kila kumi. Baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba, wanaume sita hadi saba, huchukua makahaba katika maisha yao, hata kama ni mara moja tu.

Lakini jambo la kushangaza na kusikitisha ni kwamba, imebainika sasa kuwa, wanaume wanaochukua makahaba, nusu yake ni wanaume ambao wameoa au wana wapenzi wanaowaamini sana. Kwa haraka mtu anaweza kuichukulia taarifa hii kama jambo lisilo na maana sana au lisilo jipya, lakini ni taarifa isiyopendeza kwa wanandoa au wapenzi.

Tofauti na nyumba ndogo, kuchukua kahaba kunaweza kumfanya mwanaume asikamatwe kwa maisha yake yote, kwani kahaba na mnunuzi wake humaliza biashara huko huko. Kwa wale wakazi wa jijini Dar wanajua vizuri kwamba, makahaba wengi hufanyia mapenzi kwenye magari na hata makaburini na wanaofanya nao kuna miongoni mwao wanaoheshimika katika jamii. Ndio maana wanawake ambao wana waume wenye uwezo kifedha hawapaswi kujidanganya kwamba, waume zao hawawezi kutembea na makahaba. Kwa sehemu kubwa tafiti zinaonesha kwamba, uwezekano huo ni mkubwa sana. Kama watano kati ya kila kumi wanaweza kufanya hivyo, basi idadi ni kubwa
this is s very good thread....
 
Jamani shetani kafanya kazi kubwa, sasa hivi hao makahaba hawana shoo/ladha, wanaume sikuhizi wanakula wanaume wenzao tena wanafurahi tendo hilo kuliko kwa wake zao au hao mnaofikiri ni Makahaba.

Sasa sisi akina mama tunapambana na wezi wetu wanawake siku limekufika unakuta wako anakua houseboy sijui utakamatana na mwanaume kakuchukulia mume!

GOD HAVE MERCY!!!!!
 
Pesa mwanaharamu yakhe! Unashangaa pedejee kuopoa kahaba? wengine wanakulana viboga na midume wenzao!!
 
Hata mie nilihisi tu kuwa hizo takwimu Mtambuzi kazichakachua.............labda kama atakuw ame-base kwenye vigezo vya Kimagharibi..................

Katika eneo hili la mapenzi kuna watu humu wana hasira sana. Sipati picha huko makwao maisha yakoje?
 
Mumeo akiwa na mapesa, kuwa mpole ukijifanya njuaji utaishia kunawa kila siku, kwikwikwikwiiiii! Na ndoa itaota mabawa pia
 
Jamani kina dada, sisi wanaume ni 'watoto wakubwa' tuchukulieni taratibu na kwa stah. Maumivu ya nyuma kamwe usiyahusishe na maisha yako mapya. Ukifanya hivyo utajikuta siku zote unamchukia mumeo tofauti na ulivyoapa mbele ya kiongozi wako wa dini siku mliooana.

Ila kumbukeni usemi wa mwanamke mwenzenu: 'wawili wanapooana, mwanamke huamini mwanaume atabadilika huku mwanaume anaamini mwanamke hatabadilika'. Ifikirieni hii kauli ya mwanamke mwenzenu, ina maana kubwa sana ktk mahusiano ya wawili ambao tayari wako ndani ya ndoa.
 
Back
Top Bottom