Hili linanitatiza

hicho ndo kinanichanganya kabisa, kwamba pesa yake ye anafanyia nini? mara nyingi nafikiria sana na kuona its so unfair mwishowe naishia kuwa stressed na kuwa very bitter

its ok do anything to fight for ur ndoa,make sure unazungumza na mumeo hadi mpate muafaka mzuri,tumia busara na hekima dia,usisahau kumwomba mungu
 
kama hii ni ngumu basi aombe uhamisho ili awe jirani na mume wake.

hapo sawa,imajin anaacha kazi na mume anakata matumizi kama anavyofanya sasa,si atapata kichaa dada wa watu! Watoto watateseka sana pia.
 
its ok do anything to fight for ur ndoa,make sure unazungumza na mumeo hadi mpate muafaka mzuri,tumia busara na hekima dia,usisahau kumwomba mungu

ikishindikana basi peleka kwa wazazi au watu wa dini kama ni kanisani au msikitini.
 
da, i feel your situation sister. ngoja nitafakar, but really you are not alone.
 
Pole sana mama,

Usiache kazi kabla ujapata kazi nyingine ushauri wangu wa kwanza kwa upande wa kazi ndio huo.

Kwenye swala la ndoa kusema kweli kutengana kwa umbali wowote sio rahisi maisha yaendelee kuwa ya kawaida na pia kumbuka mna watoto hawa watoto wanahitaji malezi yenu wote wawili.Kukaa na watoto peke yako umejibebesha mzigo mkubwa sana na unaweza kupata stress ambazo zita kuaribia utendaji wako wa kazi na mwisho ukachukua maamuzi mengine ya ajabu.

Muhimu umueleze kwamba mwanzo wakati umempa taarifa ya kuhamishwa alikubali kushirikiana na wewe lakini hali haiko kama hilivyo.Sasa mwambie unatafuta kazi Dar au kama utaweza kupata transfer urudishwe pale pale ulipokuepo mwanzo hili muweze kuishi pamoja tena.msikilize atasema nini kama mchango wake utakuwa wa kukuweka mbali na wewe au atakubaliana na mawazo yako ya kutafuta kazi dar hili muishi kama mwanzo kwani mambo hayajaenda kama mlivyotegemea.kama akitoa mawazo ya kukuweka mbali basi ujue kuna tatizo zaidi jamaa anatafuta uhuru wa kufanya mambo yake mengine.
 
Pole sana mpendwa muombe mungu akupe hekima ya kutambua kinachoendelea na mumeo apate kurudisha upendo wake wa mwanzo kwako, jarib kujizuia usipate hasira kwa hilo, tumia busara na hekima kuzungumza naye. ila mwamini mungv kwan hakuna linalo shindikana kwake.
 
Kwanza pole kwa hayo yote dada angu,
Sina familia lakini kwa hali ya kawaida sidhani kama hio ni sahihi kwa baba kuwa wa staili hio.

Najua hapa utapata ushauri mzuri tu, lakini na mbaya pia.
Sasa ili uweze kuchanganya ushauri utakaoupata hapa na akili zako mwenyewe hebu, jaribu kumshirikisha Mungu.

Ingia chumba chako cha ndani, moyoni mwako I mean, muombe Mungu, akuongeze katika kupata majibu ya hili tatizo lako.
Halafu omba utulivu wa moyoni, hakikisha moyoni una utulivu, usiwe na hasira, chuki wala lawama juu ya baba huyo.

Imagine hivi, Angekuwa ametangulia mbele ya haki (si ombei) usingeweza kuhudumia watoto wako na wewe mwenyewe?
Jitengenezee confidence ndani yako, kwamba you can without him.

Ukifanikiwa hapo, andaa safari na mpango mzuri tu, wenye hekima na unyekekevu ndani yake.
Ukae na huyo baba/mume wako mpendwa, uzungumze nae, msikilize, mueleze vile unavyojisikia, hapo nadhani na Mungu akiwa upande wako,
Utamuelewa tu nia yake ni nini hasa.

Kumbuka hekima ya pekee inatakiwa hapa dada, zingatia utulivu moyoni, utaipata tu nia yake.
Ukisha fahamu nia yake hata kama haitakuwa nzuri kwako, still usikate tamaa,
utaumia lakini usikate tamaa kamwe, kumbuka unaweza, Yes you can even without him. Maana hata sasa umeweza.

Umetoa ushauri mzuri sana, lakini hapo kwenye nyekundu nadhani umeteleza kidogo
 
kama uko serikalini ni rahisi kwa wewe kuomba uhamisho na ukapata. grounds unazo nyingi.kwanza ni haki yako ww kuwa karibu na mumeo, pia unapata wk mgumu kulea watoto peke yako,tatu malezi bora ya watoto yanatkiwa kuwa na wazazi wote na mwisho unahofia kuvunjika kwa ndoa yako andika na jinsi unavoshindwa kumudu kulea peke yako,ipeleke kwa boss wako na nakala peleka utumishi.kama ukoprivate mwone human resouce office wako na pia boss wako ukiwa na hiyo barua na pia waeleze personally kilio chako lazima itasikilizwa ili uweze kuhama fasta.Mungu mkubwa atakutangulia.usisubiri wakijibu fuatilia kila mara hadi kieleweke.
 
hicho ndo kinanichanganya kabisa, kwamba pesa yake ye anafanyia nini? mara nyingi nafikiria sana na kuona its so unfair mwishowe naishia kuwa stressed na kuwa very bitter

ndugu hapo ndio kuna tatizo lako. usiangalie sana pesa zake, utakonda na hata kufa kwa stress. angalia ndoa yenu, na watoto wenu. kama umejaliwa pesa inayokuruhusu kuish na watoto, mshukuru Mungu, usianze kujiletea mawazo na stress kwa pesa za mwenzio.

hiyo ni nyongeza tu kwa ushauri wa LD. zaidi sana angalia ushaur wa dada LD hapa chini, umejitosheleza

Kwanza pole kwa hayo yote dada angu,
Sina familia lakini kwa hali ya kawaida sidhani kama hio ni sahihi kwa baba kuwa wa staili hio.

Najua hapa utapata ushauri mzuri tu, lakini na mbaya pia.
Sasa ili uweze kuchanganya ushauri utakaoupata hapa na akili zako mwenyewe hebu, jaribu kumshirikisha Mungu.

Ingia chumba chako cha ndani, moyoni mwako I mean, muombe Mungu, akuongeze katika kupata majibu ya hili tatizo lako.
Halafu omba utulivu wa moyoni, hakikisha moyoni una utulivu, usiwe na hasira, chuki wala lawama juu ya baba huyo.

Imagine hivi, Angekuwa ametangulia mbele ya haki (si ombei) usingeweza kuhudumia watoto wako na wewe mwenyewe?
Jitengenezee confidence ndani yako, kwamba you can without him.

Ukifanikiwa hapo, andaa safari na mpango mzuri tu, wenye hekima na unyekekevu ndani yake.
Ukae na huyo baba/mume wako mpendwa, uzungumze nae, msikilize, mueleze vile unavyojisikia, hapo nadhani na Mungu akiwa upande wako,
Utamuelewa tu nia yake ni nini hasa.

Kumbuka hekima ya pekee inatakiwa hapa dada, zingatia utulivu moyoni, utaipata tu nia yake.
Ukisha fahamu nia yake hata kama haitakuwa nzuri kwako, still usikate tamaa,
utaumia lakini usikate tamaa kamwe, kumbuka unaweza, Yes you can even without him. Maana hata sasa umeweza.

nilitaka kuandika lakini kila nilichotaka kushauri kiko hapa. dada rain angalia na ufuate ushauri huu nawe na ndoa yako mtaishi.
 
Wapendwa, nakwazika na hapa nimekuja kutafuta advice na vilevile kufunguliwa akili.
Nina mume, nikahamishwa kikazi kwenda mkoa mwingine yeye akabaki dar, nilikuwa niko tayari kuacha kazi ili mradi tu tusitengane, au asione nimejali kazi zaidi yake, lakini alinitia moyo na kuniambia niende kufanya kazi, akani assure kuwa kila kitu kitakuwa sawa, tutakuwa tunaonana kila mara maana mikoa hii ni ya jirani. Cha kushangaza mwenzangu hataki kabisa kuja kutusalimia, yani nisipoenda mimi dar basi, yeye wala hashtuki hata weekend, watoto ninao mimi huku, sasa hii inamaanisha nini? kwa ufupi hajihusishi na kitu chochote kuhusu sisi, hatusaidii hata kodi ya nyumba japo yeye dar halipi kodi, wala matumizi wala nini, nothing. hata nikienda kmimi hatoi hata pesa ya nauli ya mimi kurudia huku wala hajali kama nalazimika kusafiri na watoto sometimes ili wamwone baba yao.
Nifanyeje? nimechanganyikiwa hapa nilipo, au ndo njia ya kuget rid of me? kanichoka? au ndo nishawaachia wenzangu huko? niache kazi nirudi tubanane? nipeni tafsiri ya haya, is it normal kwa familia zingine? pls nipeni uzoefu wenu.

Miye sikushauri uache kazi maana kazi zenyewe za siku hizi ni kubembeleza na huwezi kujua labda jamaa ndiyo kishatupa jongoo na mti wake. Inabidi umweke kikao ambacho kwa maoni yangu waliowazidi umri (mfano wazazi wa pande zote mbili) wahusishwe katika kikao hicho ili kuzungumzia hii hali ambayo si kitu cha kawaida kwa wanandoa. Usifanye makosa ya kuacha kazi na kuamua kurudi Dar bila kujua nini kinachoendelea maana hiyo kazi unaweza kabisa kuwa unaihitaji sana kama ndiyo ataamua ndoa basi.

pole sana. be extra careful especially decision ya kuacha kazi. mdogo wangu amevunja ndoa kwa style hii hii
 
Pole dada,
kiukweli nakwazika nikisikia visa vya kwenye ndoa!
Omba Mungu aingilie klati.
 
Umetoa ushauri mzuri sana, lakini hapo kwenye nyekundu nadhani umeteleza kidogo

sorry Kituko kwa hilo, but you know what, maisha ya huyu mama na watoto lazima yaendelee kwa sababu yoyote ile,
Whether huyo baba yupo au hayupo. So ile tu kujiamini moyoni kwamba anaweza akiwa anaongozwa na Mungu inatosha,kumpa fursa ya ku deal na hilo tatizo.

What if akajiwekea kuwa hawezi bila yeye, halafu kumbe baba wa watu ndo kashaamua kumuacha na watoto wake.

Je ajiuwe, akubali kuchanganyikiwa hadi awe kichaa, au....

RAIN UNAWEZA, TUNAISHI KWA NEEMA YA MUNGU TU. Kwamba mwanaume hayupo Asante Mungu, yupo Asante Mungu.
Maisha lazima yaendelee.
 
Only God can! asikuchanganye saaaaaaana...
 
anadha marriage viktim! dah pole sana dada. acha nikachukue brifkesi langu la ushauri. brb.
 
Huo ubusy hauwezi kuongezeka baada ya wewe kuhamia huko uliko lazima kuna kitu Behind the scene!!! Chunguza lazima tu utabaini ukweli lakini kama una moyo wa Plastic mshitukize siku moja uende bila taarifa mostly iwe weekend, jitahidi hata watoto wasijue maana wanaweza kuharu deal ila ujiandae Mama uisije kuzimia bure maana anaweza akarudi Kesho yake saa 11 alfajiri na mwenzio!!!

Pole lakini!!!!!
 
Back
Top Bottom