Hili la wazanzibari kuchoma baa limekaaje?

Zanzibar sifahamu kulivyo, lakini miji ya bara biashara ya bar inakera. Baa zinarudisha nyuma maendeleo. Inatakiwa kodi ya uendeleshaji mabar iwe juu sana na kuhimiza maduka ya rejareja watu wanunue na kunywea majumbani kama wenzetu wafanyavyo. Bei ya bia ikiwa juu mno kwenye mabaa watu watalazimika kununua bia na kunywea majumbani hapo ulevi utapungua. Halafu watoa leseni hawaangalii kama sehemu kuliko mabaa ni makazi ya watu hivyo ni kuleta usumbufu kwa watu wenye familia.
Sheria za mabaa ni kwamba yawe mbali na makazi ya watu, mbali na nyumba za kuabudia, mbali na huduma za umma kama mahospitali nk. mbali na shule.
Lets stay sober

Candid, kunywea nyumbani ni sawa lakini watoto wetu? Huoni kwamba wataanza kujifunza ulevi mapema? Watasoma kweli?

Tatizo lililopo miji yetu haijapangwa na hakuna anayejali kuhusu kitu gani kifanyike wapi! Baa, masoko, gereji, hoteli, maduka viko kila mahali!! Nililazimika siku moja kuchukua sheria mkononi kwa kuzima umeme ili walokole wasipige kelele na maspika yao mtaani kwetu saa moja usiku! Jirani tena kuna mtu akafungua night club usiku kucha utafikiri uko counter ikafungwa baada ya kuwakomalia! Tatizo sheria zipo utekelezaji! Watoa leseni hawajali!
 
Hatua hii ya kachoma mabaa ni ya kupongezwa kwa sababu zifuatazo:

1) Baa ni mahala salama kwa kuchochea uzinzi na madanguro na kusababisha UKIMWI kuenea kwa haraka!
2) Baa ni mahala wanapokutana majambazi na wezi na hapo ndipo mikakati ya uhalifu husukwa!
3) Baa hukutanisha mafisadi papa na nyangumi!
4) Baa huchangia sana kuharibu Afya ya Binaadamu kwa kulewesha watu na kuchangia maendeleo ya jamii kudorora!
5) Baa huchangia kuharibu maadili na utu wa binaadamu kwa kuuza pombe na kusababisha walevi wachafue mazingira kwa kukojoa ovyo barabarani!
6) Baa husababisha ajali za barabarani kwa mlevi kuendesha gari na kusababisha roho za watu kupotea!
7) Baa husababisha umasikini kwa mlevi kutumia fedha zake kwa pombe badala ya kununua chakula kwa familia yake!
8) Baa husababisha mifarakano ya familia na kusababisha talaka!
9) Baa ni mahali pa ugomvi na vita visivyokuwa na msingi!
10) Baa unaweza kujipatia pombe na hata madawa ya kulevya na mengi machafu!

Kama Wazanzibari wameanza kuchoma moto baa na madanguro ya walevi, basi ni tendo la kuungwa mkono na kila mwenye kuwatakia mema ndugu zetu wa huko! mimi nadhani hatua hii imechelewa kuchukuliwa kwani ilitakiwa ianze siku nyingi!

Nashindwa kuelewa ni vipi Ukristo unahusishwa na Pombe wakati BIBLIA inakataza unywaji wa Pombe?

Usiwe miongoni wanywao pombe!
mithali 23:20

Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo;miongoni mwao walao nyama kwa pupa
kwa maana mlevi na mlafi huingia umasikini!

na utepetevu humvika mtu nguo
mith 23: 30

ni nani aliye na macho mekundu?
niwale wakaao sana kwenye mvinyo waendao kutafuta divai iliyochanganywa!
usitizame mvinyo iwapo ni nyekundu mwisho wake huuma kama nyoka macho yako yataona mambo mageni na moyo wako utatoa yaliyopotoka!

Hivyo sio Uislamu peke yake unapiga vita pombe bali hata Ukristo umeharamisha Pombe bali viongozi wa Dini ndio wameruhusu kwa ulafi wao!
Angalia madhara ya pombe:
Long-term effects of alcohol - Wikipedia, the free encyclopedia

Mwisho nashauri hatua kama hiyo ya kuchoma Baa za pombe pia zianze Tanzania Bara kwani Pombe na Baa zimezagaa kama uyoga! na Changudoa na ukimwi umekuwa donda ndugu! Tuanze kuchoma Baa zote zilizoko maeneo wanaoishi familia zenye watoto na wanafunzi ili kupunguza vichocheo!!!!
 
Sasa unawatiliya watu, kitumbuwa chao mchanga! hivi bila Divaj itanogage sherehe ?
 
kwa taarifa tu znzb sio nchi huru kwenye suala la kuabudu. Na kwa utamaduni wao wanaoiga nchi za kiarabu, znz itaendelea kuwa maskini milele.
 
Hatua hii ya kachoma mabaa ni ya kupongezwa kwa sababu zifuatazo:

1) Baa ni mahala salama kwa kuchochea uzinzi na madanguro na kusababisha UKIMWI kuenea kwa haraka!
2) Baa ni mahala wanapokutana majambazi na wezi na hapo ndipo mikakati ya uhalifu husukwa!
3) Baa hukutanisha mafisadi papa na nyangumi!
4) Baa huchangia sana kuharibu Afya ya Binaadamu kwa kulewesha watu na kuchangia maendeleo ya jamii kudorora!
5) Baa huchangia kuharibu maadili na utu wa binaadamu kwa kuuza pombe na kusababisha walevi wachafue mazingira kwa kukojoa ovyo barabarani!
6) Baa husababisha ajali za barabarani kwa mlevi kuendesha gari na kusababisha roho za watu kupotea!
7) Baa husababisha umasikini kwa mlevi kutumia fedha zake kwa pombe badala ya kununua chakula kwa familia yake!
8) Baa husababisha mifarakano ya familia na kusababisha talaka!
9) Baa ni mahali pa ugomvi na vita visivyokuwa na msingi!
10) Baa unaweza kujipatia pombe na hata madawa ya kulevya na mengi machafu!

Kama Wazanzibari wameanza kuchoma moto baa na madanguro ya walevi, basi ni tendo la kuungwa mkono na kila mwenye kuwatakia mema ndugu zetu wa huko! mimi nadhani hatua hii imechelewa kuchukuliwa kwani ilitakiwa ianze siku nyingi!

Nashindwa kuelewa ni vipi Ukristo unahusishwa na Pombe wakati BIBLIA inakataza unywaji wa Pombe?

Usiwe miongoni wanywao pombe!
mithali 23:20

Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo;miongoni mwao walao nyama kwa pupa
kwa maana mlevi na mlafi huingia umasikini!

na utepetevu humvika mtu nguo
mith 23: 30

ni nani aliye na macho mekundu?
niwale wakaao sana kwenye mvinyo waendao kutafuta divai iliyochanganywa!
usitizame mvinyo iwapo ni nyekundu mwisho wake huuma kama nyoka macho yako yataona mambo mageni na moyo wako utatoa yaliyopotoka!

Hivyo sio Uislamu peke yake unapiga vita pombe bali hata Ukristo umeharamisha Pombe bali viongozi wa Dini ndio wameruhusu kwa ulafi wao!
Angalia madhara ya pombe:
Long-term effects of alcohol - Wikipedia, the free encyclopedia

Mwisho nashauri hatua kama hiyo ya kuchoma Baa za pombe pia zianze Tanzania Bara kwani Pombe na Baa zimezagaa kama uyoga! na Changudoa na ukimwi umekuwa donda ndugu! Tuanze kuchoma Baa zote zilizoko maeneo wanaoishi familia zenye watoto na wanafunzi ili kupunguza vichocheo!!!!
Mkuu why don't you attack the cause instead of the effects? Shida ni baa au watu? Think about it! Bila baa watu waacha kupigana? Bila baa watu wataacha uzinzi? Bila baa watu wataacha kuuana? Wanaouana na kuvunja nyumba kule kwa nduguzu ni baa au watu?
 
Ok, wewe unatetea kuwepo kwa Mabaa labda ndio nyinyi wamiliki wenyewe! na sishangai unapopinga hilo! ila kumbuka baa inachukua asilimia kubwa kwa kuchochoea maovu! yes! kama baa zitafutwa au kupunguzwa basi uhalifu mwingi utapungua kwa kiasi kikubwa! na Mzizi wa fitina ni hiyo pombe kuuzwa kiholela bila ya udhibiti!
Hao ndugu zako wazungu wanaoaminika kwa kutengeneza pombe na kunywa, hawana mabaa ktk kila kona za mitaa wanayoishi watu! bali baa zimetengewa sehemu maalum na kwa wakati maalum! huku kwetu utakuta baa ziko mitaani ovyo na saa 12 asubuhi zimeshafunguliwa na kufungwa mteja wa mwisho anapoondoka karibia na alfajiri! sasa unategemea taifa kuendelea kweli!

Wenzenu huko Ulaya mtoto chini ya miaka 18 marufuku kununua pombe dukani! sasa huku kwetu na zaidi watani wangu Uchagani wao mtoto akizaliwa leo ananyweshwa mbege aina ya Uchumale! ambayo huchanganywa na ndulele! sasa unategemea huyu mtoto baadae awe na uchungu na nchi!

Matokeo ya kulea watoto ktk mabaa na pombe ndio haya tumeona nchi imekosa maendeleo kwa sababu za ufisadi, umaskini, ujinga na maradhi!

Mimi naishauri Serikali ya CCM na CUF huko Visiwani ili nchi yao iendelee kimaadili, kiuchumi, nk. haina budi kupiga marufuku Pombe! kwanza Zanzibar Waislamu ni 99% na Uislamu Pombe ni haramu! hao 1% kama Dini yao inaruhusu Pombe na madanguro basi waruhusiwe kufungua baa zao kwenye nyumba zao wanazoabudia! lakini kuruhusu mabaa ktk maeneo ya Wakazi ni kusababisha hasira za Wananchi na Baa zitachomwa Moto kwa Sana!

Huku kwetu Bara naishauri Serikali idhibiti leseni za Baa na iwe marufuku baa ktk makazi wanamoishi raia! kwa sababu si haki kabisa baa iwe karibu na nyumba yangu halafu mziki wa sauti kubwa na kelele za walevi zikisababisha mimi na watoto wangu tusipate usingizi na watoto kuchelewa shuleni na kusababisha wafeli mtihani na baadae wawe walevi nao!

Kwa kuwa tumeamua kuwa na Taifa la kilevi basi Serikali ichukue hatua hizi haraka kabla wananchi hawajaanza kuchoma Baa moto!
1) Leseni za baa zitolewe kwenye maeneo maalum ambazo raia hawaishi!
2) Baa zifunguliwe baada ya saa za kazi na mwisho wa kuuza pombe iwe saa 5 usiku ili watu wakalale mapema kuwahi kazini! ila siku za weekend ziruhusiwe kuwa wazi mpaka saa 8 usiku!
3) Iwe marufuku kumuuzia pombe za kawaida mtoto wa chini ya miaka 18 na pombe kali kuanzia umri wa miaka 25!
4) Iwe marufuku kumuuzia pombe mlevi aliyelewa chakari kwa sababu kuendelea kumuuzia pombe ni kummaliza kiafya na anaweza kufa!
5) Iwe marufuku kutumia spika za nje ya baa kupiga muziki kwani ni usumbufu kwa wengine na pia wagonjwa!

Serikali ikianza kudhibiti baa basi huenda Taifa letu likapona toka ktk maradhi ya Ukimwi, umaskini, maradhi na ujinga!
Madanguro yatapungua, uzinzi nao utapungua na kusababisha HIV kupungua! Pia watu watawahi kazini bila ya kupata hangover na kupunguza watu kulala makazini!
 
Ok, wewe unatetea kuwepo kwa Mabaa labda ndio nyinyi wamiliki wenyewe! na sishangai unapopinga hilo! ila kumbuka baa inachukua asilimia kubwa kwa kuchochoea maovu! yes! kama baa zitafutwa au kupunguzwa basi uhalifu mwingi utapungua kwa kiasi kikubwa! na Mzizi wa fitina ni hiyo pombe kuuzwa kiholela bila ya udhibiti!
Hao ndugu zako wazungu wanaoaminika kwa kutengeneza pombe na kunywa, hawana mabaa ktk kila kona za mitaa wanayoishi watu! bali baa zimetengewa sehemu maalum na kwa wakati maalum! huku kwetu utakuta baa ziko mitaani ovyo na saa 12 asubuhi zimeshafunguliwa na kufungwa mteja wa mwisho anapoondoka karibia na alfajiri! sasa unategemea taifa kuendelea kweli!

Wenzenu huko Ulaya mtoto chini ya miaka 18 marufuku kununua pombe dukani! sasa huku kwetu na zaidi watani wangu Uchagani wao mtoto akizaliwa leo ananyweshwa mbege aina ya Uchumale! ambayo huchanganywa na ndulele! sasa unategemea huyu mtoto baadae awe na uchungu na nchi!

Matokeo ya kulea watoto ktk mabaa na pombe ndio haya tumeona nchi imekosa maendeleo kwa sababu za ufisadi, umaskini, ujinga na maradhi!

Mimi naishauri Serikali ya CCM na CUF huko Visiwani ili nchi yao iendelee kimaadili, kiuchumi, nk. haina budi kupiga marufuku Pombe! kwanza Zanzibar Waislamu ni 99% na Uislamu Pombe ni haramu! hao 1% kama Dini yao inaruhusu Pombe na madanguro basi waruhusiwe kufungua baa zao kwenye nyumba zao wanazoabudia! lakini kuruhusu mabaa ktk maeneo ya Wakazi ni kusababisha hasira za Wananchi na Baa zitachomwa Moto kwa Sana!

Huku kwetu Bara naishauri Serikali idhibiti leseni za Baa na iwe marufuku baa ktk makazi wanamoishi raia! kwa sababu si haki kabisa baa iwe karibu na nyumba yangu halafu mziki wa sauti kubwa na kelele za walevi zikisababisha mimi na watoto wangu tusipate usingizi na watoto kuchelewa shuleni na kusababisha wafeli mtihani na baadae wawe walevi nao!

Kwa kuwa tumeamua kuwa na Taifa la kilevi basi Serikali ichukue hatua hizi haraka kabla wananchi hawajaanza kuchoma Baa moto!
1) Leseni za baa zitolewe kwenye maeneo maalum ambazo raia hawaishi!
2) Baa zifunguliwe baada ya saa za kazi na mwisho wa kuuza pombe iwe saa 5 usiku ili watu wakalale mapema kuwahi kazini!
3) Iwe marufuku kumuuzia pombe za kawaida mtoto wa chini ya miaka 18 na pombe kali kuanzia umri wa miaka 25!
4) Iwe marufuku kumuuzia pombe mlevi aliyelewa chakari kwa sababu kuendelea kumuuzia pombe ni kummaliza kiafya na anaweza kufa!
5) Iwe marufuku kutumia spika za nje ya baa kupiga muziki kwani ni usumbufu kwa wengine na pia wagonjwa!
Ni vizuri kujifariji
 
Save Water Drink Beer. "Alcohol doesn't solve any problem,
But, if you think again, neither does milk."

mkuu nilikua nakunya kwa ajili ya leisure...nimesoma avatar yako... naomba nisitishe ... kwani hata hiyo leisure sitaipata solution yake
 
Yaani hata JF pia ni ulevi mtindo mmoja! sasa si ungengoja kwanza pombe ikutoke kichwani ndipo upost comments zako?
 
ha haaaaa....mods and zubeda... i stand to be corrected..... nakunywa .. i am sorry for any inconveniences ..... uungwana zaidi hapa JF
 
waache unafki hao Wazanzibari mbona hawachomi moto hoteli za kitalii zinazouza pombe na nyama ya nguruwe pia? au uadui wao upo kwa Wazanzibari/Wabara wenzao wenye mabaa?

Jee wewe unaona sawa kufanyiwa kelele usiku wa manane wakati umepumzika, au pengine una mzee wako mgonjwa hapati amani kwa fujo za baa?

Hoteli za kitalii hawaruhusu maCD kufanya fujo au kupiga muziki kwa sauti ya juu kwani wao watajishushia hadhi.

Tatizo nyinyi Bara kila munalofanyiwa hata la uonevu na kunyang'anywa haki zenu munalalamika pembeni na kuendele kusononeka moyoni.

Hebu angalia Sinza ilivyo na mabaa kila kona na kelele nyingi bila kiasi lakini kimyaaaaa!
 
Where is religious tolerance? Hamad na CUF wapo wapi? Tunaomba Opinions...

Unamaana gani by religious tolerance? hapa panazungumzwa Baa na madanguro! unamaana wamiliki wa hizi baa na madanguro wana dini? na dini yao ni ipi ambayo haivumiliki kwa tabia yake ya kufungua baa na kuuza pombe?
 
Wazenj kiasi chao kunungunika, kwani wadai Mabaa ni balaa la Muungano na wameletewa na Wabara na ushahidi ni wanaoteteya Mabaa ni Wabara! hivi kweli Haimkiniki Mbara hajapatapo kulewa maishani mwake?
 
Wacha kasumba weye! Kama hujui Zenj ka kimya!
 
Kwa nini mtu alazimishwe kutokunywa pombe. Mambo ya dini ni mtu na Mungu wake. Kama nakunywa pombe wacha nihukumiwe na Mungu lakini siyo mwanadamu. Hili la kuchoma Bar ni kosa la jinai ambalo linatakiwa kulaaniwa na kila mtu. Mbona waislamu kunakunywa nao kila siku jamani?
hili swala la kuwepo bar kila mahali linaudhi sana, baa katikati ya makazi ya watu halafu usiku ni mikelele,wadogo zetu wanaona mambo ya kikubwa pindi wateja walevi wanafanya ngona kwenye kuta za jirani na baa.

HATUPINGI UWEPO WA BAA ila zizingatie makazi ya wanaichi.
 
Zanzibar sifahamu kulivyo, lakini miji ya bara biashara ya bar inakera. Baa zinarudisha nyuma maendeleo. Inatakiwa kodi ya uendeleshaji mabar iwe juu sana na kuhimiza maduka ya rejareja watu wanunue na kunywea majumbani kama wenzetu wafanyavyo. Bei ya bia ikiwa juu mno kwenye mabaa watu watalazimika kununua bia na kunywea majumbani hapo ulevi utapungua. Halafu watoa leseni hawaangalii kama sehemu kuliko mabaa ni makazi ya watu hivyo ni kuleta usumbufu kwa watu wenye familia.
Sheria za mabaa ni kwamba yawe mbali na makazi ya watu, mbali na nyumba za kuabudia, mbali na huduma za umma kama mahospitali nk. mbali na shule.
Lets stay sober

Can you say with evidence?
Nimetembelea miji kadhaa hapa Tanzania, na kwa muonekano, miji yenye baa nyingi haiko nyuma kimaendeleo...
Tena inawezekena ipo mbele zaidi ya baadhi ya miji yenye baa chache.
Kwa jinsi ninavyoweza kuichambua kwa haraka haraka, kati ya miji niliyotembelea Tz bara yenye baa chache ni Mtwara, Bukoba, Singida, Tanga.
Miji yenye baa nyingi niliyowahi kutembelea ni Moshi, Arusha, Morogoro, Mwanza, Mbeya.
Unaweza mwenyewe kutuambia kama hizo zenye baa chache zina maendeleo zaidi au la!
Nimewahi kutembelea pia miji kadhaa ya Znzb. Kwa mfano mjini Chakechake Pemba, kuna baa moja tu ambayo ni mesi ya jeshi. Zingine ni katika Hotel za kitalii maeneo ya ufukweni, mbali na makazi ya watu. Asikudanganye mtu, kati ya watu kumi utakaopishana nao pale Chake, nane wamevaa yeboyebo (huu ni mfano tu lakini maisha kwa ujumla ni umaskini uliokithiri). Ingekuwa kwa kutokunywa pombe watu wanaendelea, znz ingekuwa Ulaya...
 
Jee wewe unaona sawa kufanyiwa kelele usiku wa manane wakati umepumzika, au pengine una mzee wako mgonjwa hapati amani kwa fujo za baa?

Hoteli za kitalii hawaruhusu maCD kufanya fujo au kupiga muziki kwa sauti ya juu kwani wao watajishushia hadhi.

Tatizo nyinyi Bara kila munalofanyiwa hata la uonevu na kunyang'anywa haki zenu munalalamika pembeni na kuendele kusononeka moyoni.

Hebu angalia Sinza ilivyo na mabaa kila kona na kelele nyingi bila kiasi lakini kimyaaaaa!

Nisivyoona raha kupigiwa kelele na mziki wa baa usiku au mchana, ndivyo pia nisivyoona raha kupigiwa kelele na wahubiri mitaani na wanaofanya adhana. Kama tunakataza baa kwa sababu ya kelele, basi tukataze pia makelele ya adhana na mahubiri kwenye nyumba za ibada zilizojengwa karibu na makazi yetu...
 
Hili la wanzibar kuchoma baa limekaa vibaya sana na linahitaji kukemewa, huwezi kuchoma baa wakati wamiliki wake wanalipa kodi. Na si mfano wa kuigwa hata kidogo. Kwa sababu mambo kama hayo ndio yanayorudisha maendeleo Nyuma, huwezi kuwalazimisha watu waishi kama watu wengine wanavyotaka, mtu atatandikwa gombo la chuo kama likimwingia atabadilika mwenyewe na kuchoma baa sio suluhisho la kuwabadili watu.
 
Can you say with evidence?
Nimetembelea miji kadhaa hapa Tanzania, na kwa muonekano, miji yenye baa nyingi haiko nyuma kimaendeleo...
Tena inawezekena ipo mbele zaidi ya baadhi ya miji yenye baa chache.
Kwa jinsi ninavyoweza kuichambua kwa haraka haraka, kati ya miji niliyotembelea Tz bara yenye baa chache ni Mtwara, Bukoba, Singida, Tanga.
Miji yenye baa nyingi niliyowahi kutembelea ni Moshi, Arusha, Morogoro, Mwanza, Mbeya.
Unaweza mwenyewe kutuambia kama hizo zenye baa chache zina maendeleo zaidi au la!
Nimewahi kutembelea pia miji kadhaa ya Znzb. Kwa mfano mjini Chakechake Pemba, kuna baa moja tu ambayo ni mesi ya jeshi. Zingine ni katika Hotel za kitalii maeneo ya ufukweni, mbali na makazi ya watu. Asikudanganye mtu, kati ya watu kumi utakaopishana nao pale Chake, nane wamevaa yeboyebo (huu ni mfano tu lakini maisha kwa ujumla ni umaskini uliokithiri). Ingekuwa kwa kutokunywa pombe watu wanaendelea, znz ingekuwa Ulaya...

kaka hapo na mimi nimekupata vizuri.
ingefaa pia ungefanya tathmini ya kutosha juu ya mikoa inayoongoza kwa kuwa na waathirika wengi wa UKIMWI.
1.0 IRINGA 2. MBEYA 3. MOSHI. 4.0 MWANZA. 5.0 DSM (KINONDONI). 6. ARUSHA.
Na mikoa ambayo ina idadi ndogo ya waathirika wa ukimwi = Zanzibar.
Halafu ungefanya pia utafiti wa mikoa ambayo katika sakata la EPA na ufujaji wa Rasilimali za nchi aka MAFISADI ni ipi imeongoza. MOSHI NA ARUSHA.
Mungu alisema ukweli: "Ndani ya pombe kuna manufaa kidogo lakini madhara yake ni makubwa kuliko manufaa yake".
Napongeza ndugu zetu kuchoma mabaa.
Ni aibu kuhusianisha pombe na Ukristu.

Back
Top Bottom