Hili la wanawake wa Arusha ni kali ya mwaka!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Kwa kuogopa kugombezwa na pengine kupewa kichapo na waume zao kwa kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, wanawake wa kijiji kimoja mkoani Arusha wamekuwa wakiwadanganya waume zao kuwa hivyo ni vidonge vya kuongeza damu.

Kutokana na uongo huo, waume zao wamejkuta nao wakitumia hivyo vidonge wakiamini damu zao zitaongezeka. Huu ni ukweli wala sio utani na niliusikia jana kwenye redio na kuona kwa tv usiku wa jana. Bado binafsi sijajua madhara ya kiafya kutokana na wanaume hao na kwa vizazi vyao vya baadae kutokana na kutumia vidonge hivi.

Ama kweli dunia bado inakua.
 
Tunaweza kucheka kuhusu hilo kumbe baadaye watanzania wote tutalia, pls saidieni watu hao wamama wapewe njia zingine za kupanga uzazi kwa kushirikiana na waume zao kwanini wafiche kama za kupanga uzazi wanatembea nje ya ndoa nini?
 
Tanzania: Ukimsomesha mwanamke umeelimisha jamii
Arusha: Ukimwonesha vidonge vya uzazi mwanaume, umeelimisha jamii

Tunaweza kucheka kuhusu hilo kumbe baadaye watanzania wote tutalia, pls saidieni watu hao wamama wapewe njia zingine za kupanga uzazi kwa kushirikiana na waume zao kwanini wafiche kama za kupanga uzazi wanatembea nje ya ndoa nini?
 
Dahhh
Si lazima vidonge wanaweza kupata injection
Na hiyo injection inaweza kukaa miezi 3,6,9
Hata mwaka mzima ni option ya mtu. Injection is more effective than pills..

Tatizo moja la injection unaweza usipate period. Au damu itatoka kidogo sana .
Inategemea kutoka kwa mtu na mtu ..

Uzuri wa injection ukichomwa hiyo moja basi
Mpaka muda uishe.

Njia nyingine ni hizo za
condom za kike
Condom za kiume.
Diaphragm - lakini hii itafanya kazi ndani ya masaa 24 tu ..
Implants - hii unawekewe kwa kutumia surgery na itakaa kwa muda wa miaka 3 hadi 5.
IUD... hii ni kwa wale ambao wanataka kufunga kizazi kwa muda wa miaka 5-10.


Kila nilicho taja hapo juu kina side effect ..
Ukienda kwa doctor wako wata kueleza kwa
Undani zaidi ..


Kwa hao waname wano chukua hizo pills zina weza kuwa effect ..

size ya mapumbu kupungua, ukuaji wa matiti kuongezeka,
upungufu wa sperm, Upungufu wa misuli, upungufu wa kuaji wa
nywele sehemu za siri na kama umetumia kwa muda mrefu sana
mwanaume ataanza kuoneka kama mwanamke ...
 
I am wondering! Kwani hao wanawake hawawezi kuficha waume zao wasione? Mbona wanawake ni wazuri sana kwa kuficha vitu?

This has to stop. Something must be done. wanaume hao wanateketea kama alivyosema Afrodenzi
 
Hii ni kali kuliko, kweli elimu ni muhimu! Wameshindwa hata kusoma vidonge vimeandikwaje?
 
Niliwahi kuweka utafiti mmoja hapa kwamba wanaume nao watatumia vidonge vya majira vilivyogunduliwa hivi karibuni, nadhani huo ni mwanzo katika kuelekea huko..........................
 
Niliambulia mwisho wa taarifa nikakutana na swali la kipima joto kuhusiana na hili la wannaume nao kutumia vidonge hivyo........well kwa kuwa sikuwa na habari kamili sikutilia maanani kujua ni nini hasa ITV wamelenga.....................leo ndio nagundua na nimesikitishwa sana......hii ni hatari kwetu
 
Niliwahi kuweka utafiti mmoja hapa kwamba wanaume nao watatumia vidonge vya majira vilivyogunduliwa hivi karibuni, nadhani huo ni mwanzo katika kuelekea huko..........................


Mhhhhhhhhh! kama ni mwanzo basi tumekosea, kwani kama ni gari basi tumeanza kuondoka na gia ndogo halafu ni mlimani hapo lazima gari ishindwe kupanda mlima na kurudi nyuma. Matokeo yake nadhani unaweza kuhisi yatakuwaje............!
 
Back
Top Bottom