Kwa maoni yangu nafikiri ni vyema viongozi wetu wakuu km raisi na waziri mkuu, wakistaafu wapewe stahili zao ambazo ni sawa kama watumishi wengine wa umma. Taifa lisienndelee kubeba mizigo ya kuwahudumia. Viongozi wetu wastaafu tunawapenda na tungependa waishi maisha marefu baada ya kustaafu uongozi wa kitaifa. Lakini si jambo jema kwa taifa kuendelea kubeba mzigo mkubwa wa kuwahudumia ilhali wameishastaafu kwenye ajira ambayo walilipwa mishahara mikubwa na marupurupu tele.
Akiongea na gazeti la mwananchi juzi, Professa Tigiti Sengo, amesema kwa sasa kuna wastaafu zaidi ya 12 na tz inapoteza mabilioni kila mwaka kuwahudumia hao. Ametoa mfano wa marekani na uingereza ambapo wastaafu hurejea ktk shughuli zao za kiuchumi kujiendeleza.
Hivi hapa tz haya hayawezekani? inakadiriwa tuna wastaafu wa jinsi hiyo zaidi ya 12, na kama nilivyosema hapo awali tunawatakia maisha marefu, je tukiwa nao 50 ama 100 taifa litawezaje mzigo huu?