Hili la TTCL ni hujuma ya wazi, lazima lichunguzwe

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
Mbunge wa Mpanda Mjini (CHADEMA) leo aliuliza swali kuhusu uuzwaji wa hisa za TTCL mwaka 2000. Inawezekana baadhi ya tarakimu hapa nikizikosea, lakini bado msingi wa hoja yangu ukawa usiathirike.

Wakati Naibu Waziri (bila shaka wa mawasiliano) akijibu swali hilo alisema kwamba wakati wa makubaliano ya uuzwaji wa TTCL, ilionekana kwamba mwaka 1999 TTCL walipata FAIDA ya sh. Bilioni 7 ( au Bilioni 5 kama sikosei).

Hivyo basi, makubaliano ilikuwa kwamba TTCL ingeuzwa USD 120m endapo mwaka 2000 wangeendelea kupata faida LAKINI endapo wangepata HASARA basi wangeuza chini ya hapo!!! Ajabu ni kwamba, wakati 1999 TTCL walipata faida kubwa sana, mwaka uliofuata ambao ungeamua bei wakapata hasara ( Je, ili wapate sababu ya kuiuza kwa bei ya kutupa?!) ya Sh.Bilioni 5 ( au Bilioni 7 kama sikosei)

Kutokana na makubaliano ambayo waliyaweka kabla (kwamba endapo kampuni ingepata hasara basi bei isiwe USD 120m) kampuni ya TTCL ikauzwa kwa USD 65m, almost juu kidogo ya nusu ya bei!!!!!! Sio siri, baada ya majibu hayo ya mHeshimiwa Naibu Waziri, nikabaki na maswali mengi zaidi kuhusu DEAL hiyo kati ya Serikali na wanunuzi wa TTCL.

Je, ilikuwaje kampuni 1999 ipate faida ya USD 7m( or 5m) na mwaka uliofuata wapate hasara kubwa kiasi hicho? Hivi nikiwa ni mashaka kwamba hasara ya mwaka 2000 ilikuwa ni ya kutengenezwa ili TTCL iuzwa kwa bei ya kutupa itakuwa sio sahihi?
Hivi hili suala sio la kiuchunguzi? Binafsi ningependa uchunguzi ufanyike dhidi ya hili suala.Kuna kila dalili kwamba kuna mchezo mchafu ulifanyika.

Hapa nazani uchunguzi unahitaji kwa watendaji wa wizara pamoja na waliohusika na uandaaji wa Balance Sheet ya TTCL kwa mwaka 1999 na 2000 ili kuangalia endapo hawaku-temper na figure ili malengo ya TTCL kupata hasara 2000 na hatiame kuuzwa kwa nusu bei yafikie!
 
Back
Top Bottom