Hili la mwandishi Privatus Karugendo

ARV

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
4,865
6,786
Katika gazeti la Raia mwema la jana May 2, ana makala yenye kichwa cha habari 'Mwalimu Nyerere amefufuka.Yuko Sumbawanga'katika aya ya pili ya makala yake anaandika,"kisa ninachokisimulia kwenye makala hii ni cha kweli na kimetokea mbele ya macho yangu pamoja na watu wengine niliokuwa nao kwenye gari.Tumekutana na Mwalimu Nyerere! akiwa mzima."

Haya mambo ya 'kusadikika' kwa nini yanapewa nafasi katika magazeti haya makini? Kwa nini yasipelekwe kwenye vile vigazeti vya udaku?
 
Ndugu,

Nikiri kwamba sijaona gazeti tajwa (Raia Mwema), Nikiri kumfahamu mwandishi tajwa (Privatus Karugendo) kwa kusoma makala zake na kwa kufahamiana naye, Nikiri gazeti tajwa kuwa makini kati ya magazeti yaliyopo kwa sasa. Siamini kama Karugendo (ex-Padri) anaweza kuandika hayo na gazeti makini likachapisha. Kwa upande mwingine ARV utudhibitishie kwamba umesoma kwa makini kati ya msitari na mstari lakini pia umezingatia lugha ya picha/fasihi simulizi.
 
ARV!

Inawezekana kabisa hujamuelewa vizuri Karugendo, huyo mwandishi ni bingwa wa kutumia fasihi simulizi kinoma, ukisoma makala zake kijuju unaweza usimwele kabisa!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hiyo ndo shida ya kusoma kitu kishabi shabiki.
Karugendo hayuko Ulaya useme hawezi ulizika kama una shaka na alicho kiandika.
kwa kawaida yake huwa anaweka mawasiliano yake mwisho wa makala zake,muulize kisha njoo hapa!
 
Katika gazeti la Raia mwema la jana May 2, ana makala yenye kichwa cha habari 'Mwalimu Nyerere amefufuka.Yuko Sumbawanga'katika aya ya pili ya makala yake anaandika,"kisa ninachokisimulia kwenye makala hii ni cha kweli na kimetokea mbele ya macho yangu pamoja na watu wengine niliokuwa nao kwenye gari.Tumekutana na Mwalimu Nyerere! akiwa mzima."

Haya mambo ya 'kusadikika' kwa nini yanapewa nafasi katika magazeti haya makini? Kwa nini yasipelekwe kwenye vile vigazeti vya udaku?
ARV, Nimesoma hiyo article ya Karugendo na sijaona ni wapi amekosea. Kama umesoma 'headline' peke yake utapata dhana potofu, lakini kubwa kama hujaenda shule basi unaweza kupata tafsiri potofu.

Anachoongelea Karugendo ni 'legacy' ya Mwl Nyerere kupitia vijiji vya ujamaa alivyoanzisha huko Sumbawanga. Na kwa maoni yake Karugendo ni kwamba initiative hiyo ya vijiji vya ujamaa ilifanikiwa na sana huko Sumbawanga na hadi sasa watu wanaishi kwenye huo mfumo. Na anashangaa ni kwa nini ;'sucess story' hiyo haijawafakia watanzania sehemu zingine!

Kwa kifupi, inabidi usome kwa makini makala nzima ili upate kile anachojaribu kusema.
 
Last edited by a moderator:
Nimeisoma hiyo makala......ARV inaelekea umezoea kusoma makala nyepesi nyepesi sana hivyo hujamuelewa Karugendo......ni bingwa wa fasihi
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Tatizo la kutokupenda kusoma ndo linamsumbua, akishasoma kichwa cha habari tayari amemaliza kila kitu. Kwa mwaandishi kama Karugendo unatakiwa utulie tena sana ndo utaelewa makala zake. Ni moja kati ya waandishi wanaojua kutumia nguvu ya hoja kuelezea kitu.
 
Wewe ndio umekurupuka,hujamuelewa. Tatizo umesoma heading na kajisehemu tu. Nenda kaisome yote ndio utamuelewa vizuri. Sisi tuliosoma yote wala hatujaona tatizo
 
Tehe, inaonekana ARV ni mwenzangu na mie ambao ni mabingwa wa kusimama pembezoni mwa barabara kusoma vichwa vya habari magazetini then tunaishia kusema "aah! waandishi bwana" bila kununua gazeti na kusoma yaliyomo ndani.
 
Siwashangai watu kama huyu ARV wao wameshazoea magazeti yao yenye heading kama Kanumba aonekana Tabata, Okwi, Boba Sunzu watakiwa Chelsea, Kikwete Chaguo la Mungu na a lot of the same rubbish.

Sasa kama ameshindwa kumuelewa muhandishi huyo je anaweza kumuelewa Jenerali Ulimwengu? halafu ningependa kuuliza hiyo Makala imeandikwa na Padri Privatus Karugendo au Prudence Karugendo? maana hawa ni watu wawili tofauti.
 
Katika gazeti la Raia mwema la jana May 2, ana makala yenye kichwa cha habari 'Mwalimu Nyerere amefufuka.Yuko Sumbawanga'katika aya ya pili ya makala yake anaandika,"kisa ninachokisimulia kwenye makala hii ni cha kweli na kimetokea mbele ya macho yangu pamoja na watu wengine niliokuwa nao kwenye gari.Tumekutana na Mwalimu Nyerere! akiwa mzima."

Haya mambo ya 'kusadikika' kwa nini yanapewa nafasi katika magazeti haya makini? Kwa nini yasipelekwe kwenye vile vigazeti vya udaku?

Hakuna makala kama hiyo kwenye gazeti na tarehe ulilolitaja, labla kama unafanya mzaha, ambapo hapa si pake. Yafuatayo ndio makala yanayopatikana Raia Mwema la tarehe uliyotaja.

[h=2]Makala[/h] Pinda alifanya kosa, asirudie kosa

Msomaji Raia

Tume ya Warioba isije ikawa kama Tume ya Warioba

Utata kifo cha Karume: Chuki binafsi au mapinduzi? IV

CHADEMA wana wananchi CCM ina dola

Mizengwe hadi bungeni

Wana usalama na nguvu yao kwa viongozi

Evarist Chahali

Shivji na mapambano ya wanyonge

Ahmed Rajab

Mgogoro wa ardhi sasa wapambanisha wageni

Mwandishi Wetu

Huyu leo, kesho mimi au wewe ni maisha kama vile hakuna tatizo

Hidaya

Toleo la 237

Watanzania wajitose katika mafuriko gani, ya Sunami au mtoni?

Ayub Rioba

Wakubwa wapagawa

Waandishi Wetu

Arumeru bado kwafukuta

Paul Sarwatt

Msipandishe tena bei za vinywaji - Mbunge

Mwandishi Wetu

Waziri mkuu asiye waziri mkuu, serikali iliyobinafsishwa: hatuendi ko kote

Jenerali Ulimwengu

ama Zitto katumwa na Rais Kikwete; Jakaya Kikwete katumwa na nani?

Msomaji Raia

KAMILI!
Hiyo makala iko gazeti la raia mwema ya May 2, kama nilivyosema awali, page no.18. Naona unataka kutuchanganya zaidi, nadhani tatizo huna nakala halisi unasomea kwenye internet ambako makala zingine huwa hawaziweki. Tafuta hilo gazeti utaiona hiyo artical ya 'Padri' Privatus Karugendo..
 
Hili ndo tatizo la wabongo wengi, kukurupuka. Isome vizuri hiyo makala kabla hujaleta ***** humu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom