Hili la Loliondo tulifikiria au tulikurupuka!

Watanzania wengi tu vipofu, mpaka tufunguke macho sumu itakuwa tayari inafanya kazi vizuri mwilini. Zinduka we mtanzania.

Ni wewe tu, kumbe umejigundua eehee! Mimi na watanzania wenzangu siyo vipofu. Sijui hata umewezaje kusoma hii thread.
 
Watanzania wengi tu vipofu, mpaka tufunguke macho sumu itakuwa tayari inafanya kazi vizuri mwilini. Zinduka we mtanzania.
Sio vipofu tu, naona kuna wengi ambao ni viziwi vile vile. Hawataki kusikia mtu anampinga the so called babu na icho kikombe chake. Wanakuwa wakali ka mbogo!
 
Kibajaj!!!!!! wait a minute, kuna kila kila kitu cha kujiuliza kiimani, kisayansi etc etc katika tiba hii ya Loliondo lakini watu wameteseka sana na UKIMWI, pressure, kisukari etc etc kama babu anaclaim kuponya na watu wamepona basi ndicho tunachotaka hata mie I am collecting evidences on the same kama nikiwa convinced nitakwenda mie na jamaa zangu tukainywe tupone. Kama wewe hauna imani kaa kimya nenda hospitali na uendelee kufanya hivyo na usidhani au kusema waendao huko are pretty fools!!!
 
Ni miezi kadhaa sasa tangu jina la Loliondo lilipojipatia umaarufu mkubwa Afrika ya mashariki.Kwa kadiri ninavyoelewa mimi,uganga wa kienyeji ni kitu cha kurithi katika ukoo. Japo babu,baba na wewe hamkuwa waganga lakini kama kuna uganga kwenye ukoo unaweza ukawaruka wote hao ukaja tokea kwa mjukuu wako bila kujali nafasi yake katika dini,elimu na jamii kwa ujumla.
Endapo mizimu hii ya uganga itamtaka awe mganga wakati yeye tayari ni padre,mchungaji shehe ua imamu na akaanza kutenda miujiza nani anaweza kuwashawishi watu kuwa miujiza ile haitoki kwa mungu wakati muhusika yuko katika nafasi fulani ya dini? au kuanza kufuatilia background ya mtu huyu kwa kinaga ubaga?Au watu wanakurupuka tu na kufanya mambo kwa ushabiki bila kujua mafanikio au madhara ya kufanya hivyo?
Kwa wale wenzangu na mimi niwaulize chloroquine iliyokuwa dawa maarufu ya malaria ilitumika kwa miaka mingapi na baadaye kuja kugundulika kuwa ina madhara kwenye mwili wa binadamu? Kwa nini serikali ikurupuke na kuanza kusema dawa imepimwa na TFDA haina tatizo hivi badae ikagundulika ina tatizo serikali itaficha wapi uso wake?
Sawa ni suala la imani lakini tusikurupuke.

acha kuchemka hamna dawa ambayo haina madhara kikubwa ni muda ambao madhara hayo hutokea baada ya kunywa dawa,ni miaka mingapi,kama ni beyond human time scale it becomes insignificant and negligible.
 
sababu kubwa ninayoiona mimi kuhusu loliondo imani na mgunduzi wa dawa hiyo,kumekuwepo na shutma nyingi juu ya ujio wa matabibu wengine kama bibi wa morogoro na wengine kuwa naiga alicho kianzisha babu.Nina shukuru kwamba walichokiazisha ni sawa na kile alicho anzisha babu,ila tujiukize siku babu atakapo kuja na wazo la tu ili atibiwe ato sadaka ya damu ya mtu na ikithibiti watu kuponywa kpitia tiba hiyo.....serikali itakaa kimya kama ilivyo sasa?
LISEMWALO LIPO,KAMA HALIPO LINA JONGEA
 
Kibajaj!!!!!! wait a minute, kuna kila kila kitu cha kujiuliza kiimani, kisayansi etc etc katika tiba hii ya Loliondo lakini watu wameteseka sana na UKIMWI, pressure, kisukari etc etc kama babu anaclaim kuponya na watu wamepona basi ndicho tunachotaka hata mie I am collecting evidences on the same kama nikiwa convinced nitakwenda mie na jamaa zangu tukainywe tupone. Kama wewe hauna imani kaa kimya nenda hospitali na uendelee kufanya hivyo na usidhani au kusema waendao huko are pretty fools!!!

They are pretty fools!
 
Hapa tulikurupuka!
Sisemi eti sizipendi dawa asili la hasha!. Isipokuwa tumejikuta hata serikali nayo ikipoteza uelekeo baada ya kufanya utafiti tukajikuta nao wanamfanyia matangazo ya biashara babu. Mimi napatwa na butwaa kuamini magonjwa ambayo babu anatibu and "if it cannot be proved scientifically, then leave it". Nani mwenye magonjwa sugu kapona kwa imani, watu wetu wanaibiwa pesa, hili la babu angekuwa ni sheikh Yahya, tungeambiwa moja kwa moja kuwa ni nguvu za giza. Watanzania tumepoteza mwelekeo, si amini hata kidogo kuwa ugunduzi wa dawa dhidi ya magonjwa 5 hayo sugu utapatikana africa, sina hakika hata kidogo. Lakini, tuzipe nafasi dawa zetu za asili kwa kuwa hii ndiyo asili yetu waafrica na ni utamaduni wetu.

Jambo la kwanza ambalo lazima ufahamu ni kwamba Babu wa Loliondo sio mganga wa kienyeji. Ameonyeshwa tu njia ya uponyaji kwa kutumia mti huo anaoutumia. Pili, hafanyi biashara kama unavyotaka ku-suggest. Hajawahi kujitangaza, ila watu wanaenda kwake kutokana na ushuhuda wa wagonjwa waliopona magonjwa sugu. Hao ni wengi sana, kwa taarifa yako. Serikali ilichunguza dawa hiyo ili kujiridhisha kwamba haina madhara kwa binadamu, na ndicho ilichofanya. Kwa hiyo suala la madhara hapa ni out. Kilichobaki ni ushauri tu kwa wale wenye magonjwa mbalimbali kwenda kwa Babu kupata kikombe ili wapone. Basi!
 
Mdau kama ni hoja wewe ndio umekulupuka mdau,ila sio mbaya kwani pia ni sehemu wewe pia kama unapenda ufahamu na uwa unakubali kujuzwa basi utajuzwa.

Katika mambo ambayo Serikali imepata kuwajibu wananchi kwa usahihi na kwa haraka japo mwanzoni kuna viongozi baadhi walitaka kuipotosha ni kule kumruhusu MCHUNGAJI aka BABU kuendelea na TIBA yake na kumpa support kwa hali na mali.

Watanzania tufike sehemu tuwe WATANZANIA ndani ya UAFRIKA na SIO WATANZANIA ndani ya UZUNGU.Kuendelea kwa maana ya ustaarabu [CIVILIZATION] sio kuacha JADI,mkataa JADI huyo ni mtumwa.Haya potelea pote tuchukulie huyo huyo wewe umeoteshwa na MUNGU kuwa BABU anatumia UGANGA.

Kwani kuna Kosa gani kwa BABU na SERIKALI watakuwa wamelifanya dhidi ya WATANZANIA, ambao wanasheria yao dhidi ya Waganga wa JADI ambayo pia ni sheria halali iliyotungwa na BUNGE LA WATANZANIA,na kwa faida yao.

Mungu yuko popote una uhakika gani kama wadau wengine walivyokujuza hapo juu, dawa za awari za kutibu malaria baadae zilikuja kuonekana si kweli kuwa zinatibu ugonjwa huo.

Matumizi ya miti hiyo ambayo BABU anyotumia ambayo ni ya kienyeji,ni njia tu ambayo MUNGU amechagua MTUMISHI huyo kuitumia.Makanisa yote yanatumia vikapu vya UKINDO vilishonwa kwa UKILI [A strip of plaited palm lief].Mbona ujajiuliza njia hiyo ya Kienyeji [Utamadunisho] inatumika kupokelea sadaka ya MUNGU.Upeo ni kuelewa MUNGU achagui kufanya kazi kwa kuangalia asimame kwenye aina hipi ya kifaa au muonekano ili wewe,yule,mimi na mwingine tuwezekuamini.

Angekuja mtu akasema ameoteshwa na ana dawa katika muundo wa mfumo wa vidonga au kimiminika [PILLS or TABLETS] hakika wewe ungekuwa MWAMINI WA KWANZA, kwa kuwa imetengenezwa tu katika mfumo wa mazoea yako kuwa dawa rasmi [Official kwa maana ya Maabala za Wazungu] ni ile iliyotengenezwa kwenye kiwanda huko Ulaya.Utaki kufikiri nje ya uzio na ukauvaa Uafrika na ukafikiri kiafrika [Think Outside the Box].

Naishukuru Serikali kwa hili ilifikiri kwa haraka na kutoa majibu ya haraka ambayo leo hii yameleta unafuhu na kumfanya BABU kufaya kazi ya UTUMISHI wake kuwa na aueni na ya msaada kwa wale wenye uitaji wa huduma hiyo.

Mwisho hata kama BABU angekua ni MGANGA wa KIENYEJI bado Serikali ilikua na wajibu wa kumpa Msaada kwa kuwa walioamini na watakaoamini kwenye TIBA hiyo ya BABU ni Watanzania ambao chini ya Serikali yao [Kwa Mujibu wa KATIBA aina Dini] ingelazimika kusimamia IMANI YA HAO [WENYE IMANI HIYO AMBAYO SERIKALI AINA TOFAUTI YA KUWAHUDUMIA KWA KUWA AINA DINI] kuhakikisha kuwa hilo wanalohangaikia kulipata kwa IMANI YAO hiyo na MALIDHIO YAO wanalipata, na kwa maridhio hayo yao wenyewe, na kuwa Serikali itasimamia mazingira na mchakato wote, kama ambavyo ingetoa POLICE KUSIMAMIA MECHI YA MPIRA au ULINZI kwenye Sherehe yoyote ile iwe Harusi yako, au ngoma ya kumtoa Mwali mtaani kwako.

Ama ujui kuwa ni haki yako ukienda Polisi na ukaomba ulinzi watakupatia,nakumbuka miaka ya nyuma nilipata kuwa Organizer Shuleni, wakati wa Sherehe za Mahafari [Graduation] tulikua tunaandika barua Polisi kuomba ulinzi, tulipewa ulinzi kwa kulipa kama sikosei Elfu tano. Cha msingi ilikua kuahakikisha Polisi wale wanapataka chakula na usafiri kuwarudisha kituoni baada ya shughuri yetu kwisha.

Hivyo jukumu la Serikali kushiriki kwenye swala la babu sio lilikua ni KUKULUPUKA bali ILITIMIZA kile KINACHOMAANISHA NINI MAANA YA SERIKALI kuwa SERIKALI NI KWA AJILI YA WATU NA WATU HAO NDIO HAO BAADHI WAMEAMINI KATIKA TIBA YA MCHUNGAJI.

JIPANGE [Think Outside the Box]
 
jambo la kwanza ambalo lazima ufahamu ni kwamba babu wa loliondo sio mganga wa kienyeji. Ameonyeshwa tu njia ya uponyaji kwa kutumia mti huo anaoutumia. Pili, hafanyi biashara kama unavyotaka ku-suggest. Hajawahi kujitangaza, ila watu wanaenda kwake kutokana na ushuhuda wa wagonjwa waliopona magonjwa sugu. Hao ni wengi sana, kwa taarifa yako. Serikali ilichunguza dawa hiyo ili kujiridhisha kwamba haina madhara kwa binadamu, na ndicho ilichofanya. Kwa hiyo suala la madhara hapa ni out. Kilichobaki ni ushauri tu kwa wale wenye magonjwa mbalimbali kwenda kwa babu kupata kikombe ili wapone. Basi!

kitu gani kinacho mtofautisha na mganga wa kienyeji? Kwasababu amefunuliwa? Hata mizimu huleta ufunuo wao/
 
Back
Top Bottom