Hili la CUF, Nyani haoni Kundule??

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
275
:thinking::sad:
Nimemsikia bwana mmoja wa CUF (Khalifa Suleiman Khalifa) akihojiwa na Mhelela wa BBC leo saa tatu kasorobo usiku huu. Anasema hawawezi kuungana na CHADEMA kwa sababu hawataki CHADEMA hawataki kuchaguliwa marafiki. Sikiliza toka link ifuatayo kuanzia dk ya 13:57.

Media Player ya BBC

Ninajiuliza kama huyu jamaa anaongea kwa niaba yake mwenyewe au ni msimamo wa CUF.

Je CUF kuchaguliwa rafiki na CCM ni sawa lakini CHADEMA no!!?? Mbona huko Zanzibar wameunda Serikali wenyewe na CCM bila kukihusisha chama kingine??

Kati ya hao wapinzani wengine ni nani wa kuungana naye. CUF wenyewe walimtimua Cheyo kwenye nafasi ya uwaziri kivuli. Sasa hao hao wanataka CHADEMA wamwingize kwenye ushirika. Hapo nasema hapana. CUF sasa hivi naona wamekuja kiuvurugaji zaidi. Nafikiri wanajikomba kwa Kikwete ili washirikishwe kwenye serikali ya JMT au wana agenda ya Siri.

Nafikiri kuna haja ya kuwepo muafaka wa Bara kwani wenzetu kule kwao wametengeneza sasa wameamua kuvuruga huku. Nahisi wazanzibar sasa hawana moyo na JMT kwani kule kwao tayari kuna serikali kamili. Jamaa wanakuja kutafuta posho.
 
Msimamo wale ndio mbegu iliyopandwa ndani ya chama hawezi kuongea kitu kilichopangwa nje ya chama banaa atakuwa amewakilisha akili za wana cuf.
 
CUF sasa hivi ni ccm B,wanajikomba ili wapewe nafasi jmt,kwa walivyo sasa naamini kabisa hawa jamaa walikuwa wanatafuta ajira na si lingine,watanzania tuwe macho,tuendeko si kuzuri tukiwa na viongozi kama hawa wa cuf taifa litaingia kwenye udini,
 
Back
Top Bottom