Hili kutoka kwa houseboy nalo ni neno hasaa!!

NIME QUOTE TOKA KWA HOUSEBOY:

Hivi mbona katika jamii forum watu wengi mnawasakama sana Kikwete na Mwinyi tu,katika kila kitu,mbona hoja mnazoleta hazina hata miguu,kuna ushaidi wa hili?au mambo mnayomsingizia huyu jamaa?.mbona mjomba wenu alipokua anajipa mali za umma mlikua hampigi kelele au mbona hakuna hata hoja moja ya kudai jamaa arudishe hela na viwanda alivyojiuzia au fafa la Rada alilonunua mbali na bunge la uingeleza kupinga.kelele zinakuwepo kila raisi anapokua muislamu tu,au mbona viinzi vya mwanakijiji na data nyweti za ndani ya gov zinakua hazipatikani wakati wa Mkapa?.hakuna kitu kibaya sana kama kutoa data za uongo au za kizushi,kuna watu humu ndani wao wanaona kila kitu ni udini tu.Tanzania tatizo lake si kikwete au Mwinyi,Tatizo la bongo ni umasikini wa kutupwa ambao umeletwa na na kuendelezwa na viongozi wabovu bila kujali dini zao,mfano wakati wa Mwalimu (My God bless him) watanzania walikua wanakufa na njaa,tulikua tunapanga foleni masaa 8 au siku nzima kungojea kilo moja ya unga,au mchele,watu tulilazimiswa kuamia katika vijiji vya ujamaa matokeo watu wengi walikufa,ulikua ukisema tu kitu kumpinga mwalimu ndani na watu wengi walipotea kwa kuchukuliwa kiaina,tasisi na mashilika ya umma yalijaa ukabila mtupu,akaja mzee ruska akafanya alichofanya kama raisi na kumpa kijiti mkapa na kufanya alichoweza na sasa ni zamu ya kikwete .kwa mtazamo wangu bila unazi wala nini jamaa wote hawa ni wabovu .ni muhimu kuwa na data za kikweli na si ushabiki .
acha upofu wewe rada imeongelewa sana ila tunarudi kwenye swala lilelile Kikwete hataki Mkapa ashitakiwe na kama Jamiiforums ilianzishwa baada ya utawala wa Mkapa utatakaje waongelee suala lake wakati internet haikuwepo wakati huo? na mbona Lowassa alisemwa na anasemwa sana hata sasa na hata alikuwa chanzo cha Jambo forums kufungwa? Humu ndani hamna udini ni makosa na rushwa zako kama mtawala!
 
Nyerere pia ameshambuliwa sana hapa jamvini, wapo waliosema alikuwa mdini na Mkapa pia wakati wa kashifa za ufisadi alishambuliwa hapa JF na kuhusishwa na mgodi wa kiwira. Kinachompata kikwete sehemu kubwa ni kurithi baadhi ya matatizo ya awamu ya Mkapa ambayo baadhi yake leo hii imekuwa ni kauli mbiu ya wapinzani kwa mfano...UFISADI.... katika ufisadi wanaotuhumiwa ni waislamu na wakristo kama vile Andrew Chenge, Rostam Azizi, Edward Lowassa, Nazil karamagi, Gray Mgonja, Ibarahim Msabaha, Basil Mramba na Daniel Yona na wengineo.

Kumshambulia Rais aliyepo madarakani kuna athari kwa watu wa dini zote kama ilivyoelezwa katika mfano wa ufisadi hapo juu. Kashfa anazotupiwa Mkapa zinawahusisha na waislamu pia katika ununuzi wa ndege ya Rais na vifaa vya jeshi kama vile Tamil somaia na vithlan aliyekimbia nchi. Hii ina maana kwamba, kumashambulia Mkapa hakuna maana unaushambulia ukristo na kumshambulia kikwete hakuna maana ni kuushambulia uislamu kwa sababu waathirika wa mashambulio hayo ni waislamu kwa wakristo.

Naona tujenge hoja za nguvu kupinga mashambulio hayo badala ya kufikiri kwamba ni ubaguzi wa kidini. Utakapoendeza mambo hayo kuna mwingine atainuka atasema kujiuzulu kwa Lowassa na kuondolewa kwa Sitta ni chuki za kidini. Tujenge hoja za kupinga au kuunga mkono kwa kuzingatia kadhai zinazowapata wanasiasa kama vile tuhuma za Richmond au Bunge kujitenga na msimamo wa chama chenye wabunge wengi, CCM.







Wewe ndio umeandika, hapa si udini ishu ni kuwa kila kiongozi ukiwa madarakani tegemea watakusema tu, ni mambo ya kawaida...hongera sana kwakuwa mwana JF unayejadili issues kama thinktank
 
Tatizo watu mmevamia tu majukwaa mktaka history ya watu kuzungumziwa angalieni threads zingine zilizopita. Pia mind you hatupo katika kulinganisha uwiano bali tunajadilu burning issues kama unazo leta tutajadili.
 
Back
Top Bottom