Simba Mkali
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 620
- 239
Kuna basi moja linafanya kazi ya kusafirisha abiria kati ya Dar es Salaam hadi Mwanza, linaitwa Muro kila siku linalaza abiria njiani, yaani bovu ile kinoma. Mbaya zaidi linapoharibika hakuna msaada wowote unaotolewa na wahusika, hapo ndipo inapokuwa mwisho wa mchezo, aidha abiria watafute usafiri mwingine au walale kwenye basi (kama ni usiku) hilo hadi kesho yake. Jamani haya si mateso jamani. Kwani linaruhusiwa kutembea au ni la mkubwa. Nani anayejua habari zake atuhabarishe?