HIJJA:saudia inavuna USD 8.5 bil kwa siku tano TU

kaachonjo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
203
68
mwaka 2014, nchi ya saudi arabia ilivuna mapato yanayokaribia $18.6 bilion sawa na 40.6 trion za kitanzania. mapato yatokanayo na hijja yanafuatia baada ya mauzo ya mafuta kwa nchi ya saudi arabia ambayo ni sawa na $213 billion. mwaka huu saudia inajiandaa kupokea zaidi ya mahujaji 1.98 mil sawa na ongezeko la kawaida la 3% kila mwaka. kwa mwaka huu inakisiwa kuwa huenda kila hujaji akatumia mpaka $4,363 kwa siku tano tu la zoezi zima la ibada hapo october mwaka huu.
SOURCE: International Business Times.
--->
8cae37cc-6b23-46d6-9905-512351e2a150.jpg

kimsingi utagundua kwamba biashara inayohusiana na imani za dini na ibada ni biashara imara sana kwa kuwa watu kila kukicha wanahimizwa kumcha mungu.mfano nchini marekani yaliruhusiwa makampuni 80 tu kupeleka watu hijja mwaka 2014 ambapo kifurushi{travel package} cha gharama ndogo zaidi kwa kila hujaji ilikuwa ni $6,000. naamini kwa tanzania makampuni hayafanya kazi yao sawa sawa na hivyo ni fursa nyingine ya kuwekeza !
 
Back
Top Bottom