Hii ya Robert Mboma imekaaje wakuu?

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975
Huyu jamaa baada ya kustaafu si alienda kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM na akapigwa chini kwenye kura za maoni? Leo nimemwona kwenye gazeti linalotolewa na TANESCO la Bullet in the umeme jamaa eti anakagua miradi ya Tanesco.

Kuulizia naambiwa eti ndio mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TANESCO. Si ikabidi niende google! niliyoyakuta ni haya;
[h=2]October 26, 2011[/h] [h=3]RAIS KIKWETE AMEMTEUA JENERALI MSTAAFU ROBERT MBOMA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA TANESCO[/h]
Kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma Sura 257 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 (The Public Corporations Act, Cap. 257 of R.E. 2002), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jenerali Mstaafu Robert P. Mboma (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuanzia tarehe 27 Oktoba 2011 baada ya Bodi iliyokuwepo kumaliza muda wake tarehe 26 Oktoba 2011.

Pamoja na uteuzi huo, Mheshimiwa William M. Ngeleja Waziri wa Nishati na Madini kwa Mamlaka aliyonayo amewateua wakurugenzi wanane wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania kuanzia tarehe 27 Oktoba, 2011. Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi ni pamoja na:-

1. Bw. Baruany Elijah A. T. Luhanga
2. Bw. Ridhiwan Ali Masudi
3. Bw. Leonard R. Masanja
4. Bw. Vintan W. Mbiro
5. Bw. Beatus P. Segeja
6. Bw. Hassan Ally Mbaruk
7. Mhe. Victor K. Mwambalaswa (Mb.)
8. Bw. Abdul Ibrahim Kitula

Imetolewa na:
WIZARA YA NISHATI NA MADIN

WAKUU
HAMNA WATU WENGINE WA KUFANYA HIZI KAZI MPAKA TUNAWURUNDIKIA HAWAHAWA? NASIKIA JK ANAOGOPA KUPINDULI WA HII NI KWELI? NAWASILISHA KWA MJADALA.
 
Ukitaka kupata stress na kuaga dunia siku inayofuata fatilia yanayofanyika Tanzania in detail.
 
Mbona Huyo ni Mwenyekiti wa Bodi nyingi za Mashirika ya umma hata TPDC huyo ni Mwenyekiti wake na nafikiri ni Board meMber wa taasisi kadhaa kwa sasa sikumbuki lakini unaweza kupata kwa wengine.
Huyu jamaa baada ya kustaafu si alienda kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM na akapigwa chini kwenye kura za maoni? Leo nimemwona kwenye gazeti linalotolewa na TANESCO la Bullet in the umeme jamaa eti anakagua miradi ya Tanesco.

Kuulizia naambiwa eti ndio mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TANESCO. Si ikabidi niende google! niliyoyakuta ni haya;
October 26, 2011

RAIS KIKWETE AMEMTEUA JENERALI MSTAAFU ROBERT MBOMA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA TANESCO

Kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma Sura 257 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 (The Public Corporations Act, Cap. 257 of R.E. 2002), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jenerali Mstaafu Robert P. Mboma (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuanzia tarehe 27 Oktoba 2011 baada ya Bodi iliyokuwepo kumaliza muda wake tarehe 26 Oktoba 2011.

Pamoja na uteuzi huo, Mheshimiwa William M. Ngeleja Waziri wa Nishati na Madini kwa Mamlaka aliyonayo amewateua wakurugenzi wanane wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania kuanzia tarehe 27 Oktoba, 2011. Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi ni pamoja na:-

1. Bw. Baruany Elijah A. T. Luhanga
2. Bw. Ridhiwan Ali Masudi
3. Bw. Leonard R. Masanja
4. Bw. Vintan W. Mbiro
5. Bw. Beatus P. Segeja
6. Bw. Hassan Ally Mbaruk
7. Mhe. Victor K. Mwambalaswa (Mb.)
8. Bw. Abdul Ibrahim Kitula

Imetolewa na:
WIZARA YA NISHATI NA MADIN

WAKUU
HAMNA WATU WENGINE WA KUFANYA HIZI KAZI MPAKA TUNAWURUNDIKIA HAWAHAWA? NASIKIA JK ANAOGOPA KUPINDULI WA HII NI KWELI? NAWASILISHA KWA MJADALA.
 
Mimi ndo napata habari hii leo. La msingi umeme uwepo, Hili la kuwateua, katiba yetu dhaifu inampa mamlaka hayo bila kuhojiwa na mtu yeyote ikiwepo Bunge - I think so.
 
Mwenye nacho huongezewa na asiyenacho hunyang'anywa! (maandiko yanaeleza hivyo.)
 
Hawa wazee wameshika nafasi kubwa sana kiusalama, haiwezekani wakastaafu ukawaacha tu vijiweni. Ni vizuri kuwaweka bussy. Majirani zako wanaweza kuwashawishi na kuwatumia dhidi yetu.
 
kweli nchi kwishny! hivi kweli tutafikaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa? Kwa nini tusifanye walau mabadiliko tuwaondoe hawa magamba?
 
Ukiwa kiongozi legelege lazima ujue mbinu ya kuziba weakness yako, huyu wa kwetu analitumia jeshi kufanikisha hilo.
 
Ukiwa kiongozi legelege lazima ujue mbinu ya kuziba weakness yako, huyu wa kwetu analitumia jeshi kufanikisha hilo.

Mimi sjawahi kusikia duniani Jeshi linauza matrekta kwa kushirikiana na mtuhumiwa wa wizi wa pesa ya umma(EPA)
 
Mimi sjawahi kusikia duniani Jeshi linauza matrekta kwa kushirikiana na mtuhumiwa wa wizi wa pesa ya umma(EPA)
Jeshi linafanya biashara ya madini Meremeta.
Tanzania ukitaka kuiba na mtu asihoji tumia jeshi hata bunge halina ubavu.
 
Mimi ndo napata habari hii leo. La msingi umeme uwepo, Hili la kuwateua, katiba yetu dhaifu inampa mamlaka hayo bila kuhojiwa na mtu yeyote ikiwepo Bunge - I think so.

Mkuu ukiwa mwanasiasa unatakiwa uwe unalijua hili siyo I think so, ndivyo ilivyo.
 
Kagame kapiga chini majenerali watatu kwa kujihusisha na magendo ya madini tena ya CONGO...uku jenerali mzee tena mstahafu asiyekua na utaalamu wa maswala ya umeme ndo anateuliwa kusimamia bodi aya si maajabu? Tanzania kwa sasa tunamatatizo makubwa ya umeme bado hawekwi mtu mwenye taaluma husika sio upupu huu? Hivi akibolonga hatawajibishwa kweli sababu sio fani yake? na sheria inasemaje kuhusu utumishi wa umma mtu ukishastastaafu bado anatokea mtu aliyepewa mamlaka anateua tena ata km aliyeteuliwa uwezo wake umepungua kutokana na uzee wake....TANESCO kwa sasa haihitaji bombs, missiles, jetfighter, ballistic missiles wala ICBM kinachohitajika ni watu makini wenye taaluma zao ili watusaidie watanzania.....next time utasikia Rais kamteua daktari wa mifugo akasimamie TFF
 
hivi kashifa ya sukari kati ya yeye na Idd Simba iliishaje? watu kwa kubebana bwana huyu mzee mnasumbua wa nni wacheni akalime mashamba yake lukuki kule Pugu kajiungeni, kwa nini asimuige makamba kufuga kuku? Ongera Makamba Ongera sana hawa wasitafu uje uwape shule waache kug'angania madaraka tusije waondoa kwa mijeredi maana hawa hawakomi kukomba vijisenti vyetu.
 
usingechana passport haya maumivu ungeshayapata na kuyasikia siku nyingi nakushauri usiwaze kurudi tena tanzania wenzio tumeshazoea haya mwaya
 
Mboma altumiwa na magamba kuficha ufisadi wao kwa kisingizio cha siri za jeshi, wanampa ulaji ili asije akashindwa maisha akatoa siri.
 
Back
Top Bottom