Hii ya nbc-bank kufungia account za wateja bila taharifa imekaaje?

CPA

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
809
354
Kuanzia wiki iliyopita, watu wengi wamejikuta wamepigwa na butwa kwenye atm, ukiingiza atm card, atm machine inakujibu change status, na wengi wao ni wale wanaotumia card mpya (nbc master card) Ukienda bank ndan wanakujibu account imefungwa wana update customers detail, wanakupa form ya kujaza na kwenda mahakaman au kwa mwana sheria na barua ya kwenda serikali ya mtaa. Sasa 1.walipokuwa wanabadilisha card mpya, nbc master card, kwa nini wasingesema moja ya masharti ni hayo.
2. Kwenye form ile ya kubadilisha card tulijaza namba za simu, kwanin wasinge/wasipige simu kujulisha hayo mahitaji/mabadiliko, badala ya kufunga a/c. Bank kwenyewe folen kubwa, mlolongo mrefu. Sasa nini maana ya kujaza namba za simu au email address? Wameshindwa hata kutuma msg. Na mbaya zaid ili zoez limeanza kipindi cha mishahara! Kwa hili nbc mbadilike!
 
Wanaanza ulevi kwa kuwa na wamepata wateja wengi labda si unajua mbongo akipata ****** hulia mbata!!?
 
Bank nzuri ni Barclays tu nchini zingine ni za walalahoi na huduma kwa wateja ni mbaya sana utadhani ni benki zinazogawa fedha bure na mteja kwao ni mfungwa, hata AC au benchi la wateja hamna, maji ya kunywa hamna.

Tubadilike jamani. Nendeni fungueni account Barclays Bank popote ulipo na utapata ATM card unayoweza kutoa na kuweka fedha popote nchini na nje ya nchi. Barclays utapata maji, chai, kahawa, maziwa kwa wateja, lugha nzuri, customer care iliyo bora kabisa na hamna kuzungusha wateja. Sofa za kukalia wageni na AC. Kwao mteja ni mfalme, na siyo NBISII, NMBII, CRDBII, nk. hovyo kabisa.
 
Tatizo ni waajiri, wanapokuajiri, wanakupa sharti kufungua a/c kwenye bank ambayo kampuni/shirika wana account yao ipo. Mfn serikali taasisi nyingi wanatumia nmb, ukiwa na a/c nje ya bank wanayotumia mshahara kuja kupata ni baada ya wiki 2, wenzia wakaribia kupata mwingine we hata bado kwenye ac yako, haijaingia
 
Jamani mi naona benki kama crdb ni kimeo zaidi maana jana nilitaka kutoa pesa mida ya saa11 jion ktk atm ya pale mabibo hostel atm ikagoma, nikaenda ubungo napo hola, nikaenda azikiwe nako hola, nikajaribu kutumia atm za benki zingine master card inagoma, yaani kero juu ya kero hadi saa2 usiku ndo tukafanikiwa. CRDB HOPELESS KABISA.
 
Bank nzuri ni Barclays tu nchini zingine ni za walalahoi na huduma kwa wateja ni mbaya sana utadhani ni benki zinazogawa fedha bure na mteja kwao ni mfungwa, hata AC au benchi la wateja hamna, maji ya kunywa hamna.

Tubadilike jamani. Nendeni fungueni account Barclays Bank popote ulipo na utapata ATM card unayoweza kutoa na kuweka fedha popote nchini na nje ya nchi. Barclays utapata maji, chai, kahawa, maziwa kwa wateja, lugha nzuri, customer care iliyo bora kabisa na hamna kuzungusha wateja. Sofa za kukalia wageni na AC. Kwao mteja ni mfalme, na siyo NBISII, NMBII, CRDBII, nk. hovyo kabisa.

mh! Wewe ni mrongo! Nbc is the best.
 
Back
Top Bottom