Hii ya leo kali!

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
MKAZI wa kijiji cha Monuna kilichopo kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti, James Juma [22] amekufa baada ya kumwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto na wakazi wakijiji cha Maburi kwa lengo la kumwokoa baada ya kuvamiwa na kundi la nyuki.

Katika hali isiyotarajiwa watu waliofika kumsaidia walizidiwa na kundi hilo la nyuki na kutoa wazo la kummwagia mafuta ya taa, lakini nyuki walizidi kumshambulia, ndipo kukazuka wazo la kuwasha moto bila kujua kuwa tayari walikuwa wamemmwagia mafuta ya taa na moto ukashika nguo zake na kumuunguza vibaya sana.

Source: NIFAHAMISHE Tanzania news portal
 
Kweli jamani Tanzania kuna vituko!
 
they did wrong thing for right reason,

kwa hiyo ile methali penye wengi hapaharibiki neno hapa haija-apply!
 
sawa sasa twende kisheria, wana kesi ya kujibu au hawana?

...yap, wameua bila kukusudia. Hukumu yake badala ya kunyongwa au kifungo cha maisha, ni miaka 15-30 jela :)
 
Hili sidhani kama ni kosa la kwenda jela, yes ni crime, lakini it is a crime committed out of passion. Which is the ultimate passion itself, LIFE, to save life. Lakini inategemea pia na huruma ya jaji na waendesha mashitaka.
INASIKITISHA SANA, but at least amejua watu walifanya kila wawezalo kumuokoa, literaly. Including wao kuumwa na nyuki.
 
...Mh! Msaada umezua balaa tena....lakini huyo hata kama wangemuacha aendelee kuumwa na nyuki definately angekufa tu nadhani israeli alikuwa anamuhitaji tu.
 
Last edited by a moderator:
Na imani amekufa kwa sumu ya nyuki , kwani huo moto ulikuwaje? wakienda hospital wanapima percentage ya burn kisha wanaweza sema kuwa ulikuwa ni moto uliosababisha kifo au sumu ya nyuki..............ama mchanganyiko .

Duh ila jamaa naona walikuwa hawana jinsi .
 
mi ninavyojua nyuki wanafukuzwa kwa moshi! sijui kwanini hawakuchoma majani yatoe moshi
any way mambo ya ajali
 
Na imani amekufa kwa sumu ya nyuki , kwani huo moto ulikuwaje? wakienda hospital wanapima percentage ya burn kisha wanaweza sema kuwa ulikuwa ni moto uliosababisha kifo au sumu ya nyuki..............ama mchanganyiko .

Duh ila jamaa naona walikuwa hawana jinsi .

si kwamba walikuwa hawana jinsi kiasi cha kusababisha ajali hiyo mbaya ila ni kutokujua. Ni vizuri kutoa elimu ya huduma ya kwanza kwa umma pia vijana kujiunga na 'skauti'. tatizo skauti nayo imefanywa kama sehemu ya siasa! Kwani maafisa ustawi wa jamii wanafanya nini wilayani, katani na vijijini?
 
sawa sasa twende kisheria, wana kesi ya kujibu au hawana?

Heshima yako Nziku, Kumbuka kisheria, kuna suala la kuua bila kukusudia( manslaughter) nahisi wanaweza kushtakiwa katika kifungu hicho.

kwa hiyo, kesi ya kujibu wanayo.
 
MKAZI wa kijiji cha Monuna kilichopo kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti, James Juma [22] amekufa baada ya kumwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto na wakazi wakijiji cha Maburi kwa lengo la kumwokoa baada ya kuvamiwa na kundi la nyuki.

Source: NIFAHAMISHE Tanzania news portal

Natamani kucheka ...(ha ha ha ...kwikwi-inabidi nichekee kwapani!) lakini kwa heshima ya Ndg Juma inabidi nikatishe, na Mungu amrehemu.
Hawa jamaa wa Serengeti ni kiboko!!!
 
mzee hapo ndio unatusababishia kwikwi zako za kucheka
 
Back
Top Bottom