Elections 2010 Hii ya kugawa fedha kuvunja makundi -ubungo imekaaje?

Kwa nini hayo yafanyike kipindi hiki tena cha uchaguzi tena kwenye jimbo lenye ushindani mwingi.
Changanya na zako............
 
Aliye kurupuka ni yule anayeshindwa kutofautisha posho na rushwa. Yaani hujui kuwa si kila mkusanyiko , au kikao lazima kiwe na malipo? ndo maana mnashindwa kujua kuwa fedha ambazo zingeingia kwenye miradi, zinalipa upuuzi huu!


nakubaliana nawe kuwa si kila mkusanyiko au kikao lazima kiwe na malipo,lakini je ni nani anayepanga kuwa kikao hiki kiatakuwa na malipo au la(najua ni waandaaji).Na hii inategemea na sababu kadhaa,mfano uchumi wa chama,n.k
nafikiri waandaaji wa kikao hawakutakiwa wakuone wewe ili uwashauri wawalipe wajumbe posho au la.
 
Du, jamani tuwe wa tunaongea bila ushabiki.
Nafikiri kujadili pesa wanazopewa watu kwenye vikao vya ndani ya Chama kwamba ni rushwa si haki.
Tungeiita rushwa kama ingekuwa ni kwenye kampeni au ni kikao kinachohusisha watu wa nje,yaani ambao si wanachama.
Kwa mawazo yangu hiyo naiona kama sitting allowance,mbona CHADEMA kwenye vikao vya ndani watu wanalipwa posho,je ni rushwa?

Vyama vyote vinatoa sitting allowance ni jambo lililo wazi.
 
What if it was a sitting allowance for the kikao?

Have looked into this differently.

Kafanye research yako kwanza kabla ya kubandika hapa:hand:!!

Chadema walipofanya kikao cha kuteua wagombea wa viti maalum walitoa posho ambayo mimi naita sio rushwa. Wanachama hawawezi kujigharimia kwa kila kitu. Kumbuka kuna wanachama maskini lakini ni wakereketwa ambao hawana nguvu ya fedha ya kununua chakula, soda na hata nauli ni jambo linaloweza kutikisa bajeti zao. Ni lazima vyama vikawa na mfumo wa kuhakikisha wajumbe wanakula au wanasafiri kutoka sehemu moja au ingine bila kutumia fedha zao za mfukoni.
 
Usikurupuke na kutoa upupu, mi ni muelewa ninaye jua kuwa hiki ni kikao nahiki si kikao bali ni kampeni. walio husika kwenye kikao ni watu kutoa maeneo mbalimblai wanao pinga uteuzi wa aliye pitishwa. si wajumbe maalum au wawakilishi bali ni watu wenye influence na aliye shindwa. Sasa kudai kuwa ni posho! hii ni aibu. Posho zinaendana na mpangilio wa vikao na wadau, na si kutafuta baadhi ya watu na kuwamiminia fedha huku ukidai ni posho. Hivi we huwezi kutofautisha kati ya posho na rushwa!

Kweli wajinga ndio waliwao

wewe ndiye hujui kutofautisha rushwa na posho
 
Back
Top Bottom