Hii Ya Katibu wa Mbunge Lema Imekaaje?

Tatizo cdm mnatetea hata visivyotetewa kisa ni mtu wa cdm, inawezekana kabisa hata huyo Lema ni jambazi mi naamini na kama sio basi aende mahakamani kudai fidia hata ya shilingi moja kwa kuchafuliwa na Zombe! khaa! na kama ni majambazi wao sio cdm! kwani CCM wote ni mafisadi? mi sipendi kutetea ujinga kisa eti ni mtu wa cdm! inamaana kama ni majambazi na wanaendeleza wizi basi waachwe tu kisa cdm? inaudhi sana!

Hapo nakuunga mkono nami nashangaa sana wana CDM kutetea mtu msiyemjua jifunzeni wa CCM maana wao wamekubali kuwa wana mafisadi na lazima wajivue gamba lakini nyinyi mnatetea mtuhumiwa wa Ujambazi je ikija kuthibitishwa kama ni jambazi mtawaambia nini wananchi.

Tuache kutetea uovu kila mtu abebe zigo lake mwenyewe kama kweli Lema ni jambazi au katibu wake jambazi tuwaache wabebe mizigo yao wenyewe maana ni ya kwao sio ya CDM

Na CCM vile vile isiwatete mafisadi tuwaache wabebe mizigo yao. Siasa inayotakiwa ni chama gani chenye muongozo wa kuwaokoa wananchi na shida walizo nazo na kuwaletea maendeleo mimi nadhani hii ndio siasa safi

Vyama vya siasa ndivyo vinavyoipeleka Tanzania shimoni leo CCM wanaitwa mafisadi kesho CDM wataitwa majambazi hili halitoisaidia nchi jamani
 
Wana JF,

Kumbe sakata hili la wizi lilikuwa ni la kitambo sana wizi au uhalifu huo ulifanyika muda ulisha pita sasa katika kumbamba muhusika mmoja huko mbauda kama nilivyo ambiwa ndio kuminywa na kuanza kutoa habari na ndipo wakaanza kufuatilia mstari wa tukio na ndivyo kupata report ya tukio liliko tokea na kugundua gari lililo tumoka ni huyo aliyekuwa katibu wa mbunge kisa ni kuwa alitoa gari.

My Take:

Kwa hali ilivyo huko Arusha sasa ni mtu yeyeote na umaarufu wako au usiwe na umaarufu kuwa makini katika kukodisha garia au kumpa mtu kutumia gari ati atakurudishia baada ya muda maana itakula kwako esp kwa wanasiasa/wafanyabiashara wanaowindana kwa vijiba vya korosho
 
huyo Mtu anayetuhumiwa kwa ujambazi aliwahi kuwa katibu wa mbunge ila alitimuliwa kazi several months ago. mwandishi wa habari hii kwa sbb tunazozijua wote ameonelea amhusishe Mh Lema ili kupata soko la gazeti hilo ambalo kila mtu anajua limedoda,isingekuwa taasisi za umma kulazimishwa kuyanunua basi wangekuwa hawaingizi hata senti. CDM hawawezi kutetea ujambazi au majambazi ,huyo mtu kama kweli ni jambazi ashughulikiwe vilivyo. shida ni kwamba vyombo vingi vya umma viko corrupt na hakuna mtu wa kuintervene.

corrupt watendaji wa serikali+legelege viongozi wa kisiasa serikalini=corrupt legelege government.
 
Hivi hawa CCM wamekosa kabisa jambo la kulipa uzito! Je ingekuwa ni gari ya Mbunge Lema imehusishwa kwenye huo Ujambazi, si tungemwona Mpaka Mkweree, Mkewe na Mitoto yao imejazana TBC1 ikiihubiri hiyo habari!

Shame on you CCM shame on you CCM Magamba Original. Tafuteni jinsi ya kurudisha japo kaimani kidogo toka kwa wananchi baada ya kuendelea kututesa kwa muda wote huu na maisha magumu badala ya kufanya Katibu Bandia wa Lema kama Mtaji wenu wa Kisiasa.

Kweli Washirikina Mmeishiwa sera baada ya kufa yule Mshirikina mwenzenu mkuu wa pale Magomeni.
Mkuu, inaonesha umekasirika sana. Jazba kibaaaaoooooo!
 
Baada ya ccm kupoteza majimbo kwa miji mikubwa km Mwanza,Arusha,mbeya,Iringa na kwa sehemu Dar.Mkakati uliopo ni kuivurug
a Cdm.Hayo ya Arusha ni kidogo,mkakati mkubwa unapikwa Mwanza kama mnafuatila gazeti la mtanzania pekee limekuwa likiripoti yanayojiri Mwanza

Wana JF,

kwa mtu mwelewa ataijua CCM vyema kwani CCM na viongozi wake wapo kimaslahi binafsi na chama hata chama kukijali ni 20% kabisa, Viongozi wa CCM wao wako kujali kupata majimbo tuuuuu ila kuongoza wananchi wao walaaa hilo haliwahusu kabisa hivyo basi naungana na hoja yako ya msingi kuwa CCM wao ni kurudisha visasi vya kushindwa kwa kupanga mikakati ya kuchafua huko kwenye majimbo waliyo shindwa kwa aibu zao ilikutaka kujichukulia mercy kwa Public hilo waliondoe kichwani utakuwa kama Gaddafi kuwalazimisha watu wa Libya wakupende kumbe hawakupendi ndio hayo yaliyotokea leo hao hao watu waliokuwa wana kusupport ghafla wako kwa wapinzani wako ndio CCM itakavyo kuwa huko mbeleni na si muda mrefu.

Mfano mzuri tu JK anajitakasa yeye kama yeye na ndipo wabunge wake wanamshukia sasa
 
Acha waseme tunasubiri siku 30 za kuingia ofisi ya mkurugenzi wa manspaa Arusha maana vurugu zoote za siasa za Arusha ni mkurugenzi.
 
Nafikiri ni habari za kutaka kumchafua Mbunge wa Arusha kwani kosa ni kuwa huyo jamaa alikodisha gari na hiyo gari ikaenda kwenye tukio sasa haya ni mambo ya kawaida na haswa watu wanaomiliki tax ,bajaji na hata pikipiki na magari ya kukodisha kukutwa na mambo kama haya ila magazeti ya serikali na lile la CCM wameamua kuwa hiyo ndio habari kubwa na badala ya kusema ukweli wao wakapotosha kwani Lema katibu wake tangu tarehe 16/06/2011 ni mdada kwani huyu bwana aliacha kazi na hata RPC wa Arusha alipelekewa barua ya kumjulisha kuhusu hilo ila SIJUI KAMA WATAKUBALI KUJA HADHARANI NA KUSEMA JUU YA HILO NA KUWEKA UKWELI WAZI.
 
<BR>Barua yenyewe ya kuacha kazi ni kama hiyo na hii ni iliyotumwa kwa RPC Arusha <IMG id=vbattach_35800 class=previewthumb alt="" src="https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=35800&amp;stc=1" attachmentid="35800">
 
Mkuu Freedom Of Flag.

Kwa heshima kubwa lazima tukubali watu,ndugu,jamaa na marafiki tunaowapenda wanaweza kuwa wahalifu bila jamaa zao wa karibu kufahamu na wakati mwingine hata wakifahamu watajaribu kupooza kwa namna yoyote bahati nzuri kiswahili kina misamiati kibao eg kasogeza badala ya kaiba.Hata yale majambazi yanayopigwa mawe/chomwa na matairi na kufa yanakuwa na watu wa kuwalilia na pengine kulaumu kwa unyama walitendewa mara nyingi hawapendi kusikia au kuambiwa ubaya wa mtu wao na ndicho ninachokiona hapa.

Habari za Mheshimiwa Mbunge Lema kuhusishwa na ujambazi hazikuanzia kwa kamanda Zombe kama baadhi ya wanajamvi wanavyolazimisha tuamini zilianza siku nyingi sana pengine umekuwa mvivu hapa jamvini.Tunajua Mgonja aliwahi kushika wadhifa wa katibu wa mbunge jimbo la Arusha mjini.Katibu wa mbunge ni mtu wa karibu sana kwa vyovyote alishiriki kuanzia mwanzo wa kampeni hadi mwisho akapewa jukumu la kumsaidia mbunge.Umetufahamisha kwamba katibu wa mbunge ni Bwana Gabriel Mbuki.Hakuna ubishi kwamba Mbuki hakuanza kazi ya ukatibu wa mbunge mara baada ya Lema kushinda ubunge hivyo tunakubaliana Mgonja alianza kazi ya ukatibu na baadae sana sijui mwezi uliopita au mwaka jana Mbuki akampokea kijiti.

Ikiwa Mgonja kahushishwa na ujambazi lazima abebe zigo la dhambi zake hakuna haja ya kumtetea kwa namna yoyote.waandishi wa habari wana haki kabisa ya kufichua maovu bila kujali uhusiano wa mtuhumiwa au wadhifa wa mtuhumiwa.Sina tatizo na mwanahabari kufichua wadhifa wa mtuhumiwa wala Lema hata kuwa mwanasiasa wa kwanza kufanyiwa hivyo.Sidhani kama mbunge alimtuma Mgonja kufanya uhalifu kinachonikera ni aina ya utetezi wa hovyo kabisa ambao umekuwa ni sehemu ya utamaduni hapa jamvini.

Tuache waandishi wa habari wafanyekazi kwa uhuru wa kutosha hakuna mtu aliyealazimishwa kuisoma kama huitaki acha wengine watasoma.


Mkuu Ngongo,

hatuhitaji kujadili ubora wa habari, sifa na elimu ya mwandishi wa habari hizi.
ninachoelezea ni kwamba mwandishi wa habari ameupotosha ukweli kuhusu habari yake.
Nimeelezea kwamba aliyekamatwa siyo katibu wa mbunge
Aliyekamatwa anaitwa Mgonja, wakati katibu wa Mbunge Lema anaitwa GABRIEL MBUKI
wasomaji wa magazeti na watazamaji wanatakiwa kupewa habari za ukweli, siyo udaku. hii habari imekaa kishabiki sana, inaonyesha dhahiri mazingira ya chuki.
 
Barua yenyewe ya kuacha kazi ni kama hiyo na hii ni iliyotumwa kwa RPC Arusha View attachment 35800

Duh! kweli siasa za bongo zina mambo, sasa kama Zombe alishasema ooh! Lema alikuwa Jambazi, hawa habari leo wamekuja na hii ya katibu wake jambazi halafu yote yanaonekana ni uzushi and then wanaCCM wanaamini kabisa watu wataichukia CDM na kuipenda CCM huko Arusha??????
 
Vipi mkuu mbona povu linakutoka najua habari kama hizi hamzipendi kabisa lakini nakwambia zitakuja mchana kweupeeeeeeeeeeeee.

I concur with you broda. Huyu jamaa kinamuwasha kila suala la Lema linaposurface. Inaonekana upande anaoshabikia uligaragazwa vibaya sana ulingoni.
Pole Ngongo. Maisha ndivyo yalivyo.
 
Umeachiwa mikoba ya Sheikh Yahaya bwahaaa haaaaa aaa.

Unajua Ngongo record yako kuwa against Lema hata mtoto mdogo angejiuliza why????????? I told u before swallow ya pride and move on!!!!!! Lema ndiyo mbunge yule jamaa yako wa TLP au sijui ndiyo wewe mwenyewe asubiri mpaka hiyo 2015 kama siyo 2020. Na hii andama andama isiyo na kichwa wala miguu ndiyo inazidi kumjenga hahah ahahah ahahaha!!!!!!!
 
Hata mwana wa mengi aliambiwa anauza dawa za kulevya!
<BR><BR><BR>Usisahau, Kesi hiyo mpaka leo kimya. Nini maana yake kama siyo usanii wa vyombo vya dola? Na usanii wa serikali yo yote iliyoka madarakani&nbsp;ni mauti yetu. That is very serious.
 
Vipi mkuu mbona povu linakutoka najua habari kama hizi hamzipendi kabisa lakini nakwambia zitakuja mchana kweupeeeeeeeeeeeee.

Mkuu unapaswa kuelewa hakuna anayetetea uhalifu lakini hizi stailiwalizotumia akina Mugabe miaka ya 80 zimepitwa na wakati, kama ni utabiri wa anguko la Lema umeshasema hii ni zaidi ya mara mia and the guy still stands out from the crowd!!!!!!!! Ni aibu kama great thinker unaunga mkono hizo political motivated dirty tricks!!!!!!!!!
 
Barua yenyewe ya kuacha kazi ni kama hiyo na hii ni iliyotumwa kwa RPC Arusha View attachment 35800

Nafikiri ni habari za kutaka kumchafua Mbunge wa Arusha kwani kosa ni kuwa huyo jamaa alikodisha gari na hiyo gari ikaenda kwenye tukio sasa haya ni mambo ya kawaida na haswa watu wanaomiliki tax ,bajaji na hata pikipiki na magari ya kukodisha kukutwa na mambo kama haya ila magazeti ya serikali na lile la CCM wameamua kuwa hiyo ndio habari kubwa na badala ya kusema ukweli wao wakapotosha kwani Lema katibu wake tangu tarehe 16/06/2011 ni mdada kwani huyu bwana aliacha kazi na hata RPC wa Arusha alipelekewa barua ya kumjulisha kuhusu hilo ila SIJUI KAMA WATAKUBALI KUJA HADHARANI NA KUSEMA JUU YA HILO NA KUWEKA UKWELI WAZI.

Mbona kuhusu huyu Katibu wa Mbunge kuna mkanganyiko? Mara siju Mbuki mara anakuja huyu Lucia Francisco mara mwanzoni alikuwepo Mgonja!! Yupi ni yupi? Barua inasema Mgonja amepata kazi nyingine!!!! huenda ndio hiyo sasa!!!

Mkuu Mpaka Kieleweke nadhani kuhusishwa kwa Lema kuna logic. Logic yenyewe ni kwamba Zombe alishasema kwamba Lema ni Jambazi na Lema amewahi kuwa na uhusiano na Mgonja kama Katibu wake na Mgonja amehusishwa na ujambazi. Basi mkuu hapa nadhani mwandishi alitaka kuonyesha kuwa kama A=B na B=C basi A=C!!!
 
Back
Top Bottom