Elections 2010 Hii ya huyu waziri ni kiboko!

Kale kajamaa kanaonekana kastaraabu kumbe wapi bwana ila sijui kama hii ni kweli kafanya hivyo. He isn't civilised!!
 
kweli yaani huyu ndio alikuwa waziri tena wa mambo ya ndani wa JMT, pesa zote alizokuwa analipwa yaani anang'oa vitasa vya milango ??
huyu ndio tuliyempa dhamana ya kutuongoza..inasikitisha sana kwani wala sihitaji kusikia watu kama hawa..
Hii ndio aina ya Viongozi tunaowapa dhamana ya Kutuongoza. Kwani angeviacha angepungukiwa na nini? Usikute siku alipoviweka kulikuwa na sherehe ya kumshukuru kwa mchango wake!
 
Thamani anaweza kutoa kama alinunua...kama tv,computer,seti makochi mmmm ila si vitasa jamani duuuuu....
 
Dalili za ufisadi hizo!Mbona sisi wananchi hatujamnyang'anya shangingi alilopewa la ubunge kwani lilitokana na kodi zetu! Kanaonyesha jinsi kasivyo juwa gharama za siasa. Na asirudi miaka ijayo kutuomba ubunge-atashangaa kitakacho mtokea!
 
mnyonge mnyongeni haki yake mpeni vitasa kakosea kung'oa ila vifaa vingine ni haki yake kuvichukua manake aliviweka vimrahisishie shughuli zake jimboni sasa c mbunge , ila isijekuwa alinunua na fedha za mfuko wa jimbo
 
Kwa nini hatujiulizi ilikuwaje hadi aweke vitasa vyake mwenyewe? Samani kuweka zake mtu unaweza kuelewa lakini vitasa! Sitoshangaa kama nae alipokabidhiwa ofisi alikuta milango haina vitasa au vitasa feki ambavyo kila funguo inafunguwa milango yote. Ni dalili ya uzembe uliokithiri katika utendaji kazi wetu. Kama ilikuwa hivyo, Masha ana haki ya kuving'oa na kutuma ujumbe kuwa usalama wa ofisi ni vitasa.

Amandla........
 
Back
Top Bottom