Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,894
Date: 9/8/2009
DC: Nyama iliyokamatwa ilikuwa kitoweo cha Mwenge
Na Waandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya Mvomero Fatma Mwasa, amesema kuwa nyama ya wanyama saba aina ya swala waliokamatwa na maafisa wanyapori kutoka kwa wawindaji waliowapata ndani ya hifadhi ya wanyama pori ya Wami Mbiki Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, walikuwa kitoweo kwa wakimbiza mbio za mwenge.
Akizungumza jana na Mwananchi alisema uamuzi wa kutafuta kitoweo hicho cha swala kwaajili ya shughuli ya mbio za mwenge ulifikiwa na kamati ya maandalizi ya mbio za mwenge.
Mwenge huo wa Uhuru ulikuwa mkoani humu kuanzia Agosti 27 hadi Septemba 2 mwaka huu.
Askari wa hifadhi hiyo waliwatia mbaroni watu wanne wakiwa na gari la serikali na wanyama saba aina ya swala wakidai wametumwa na DC Mwasa.
Mwasa alisema kwamba, hakumtuma mtu kwenda kuwinda mnyama wa aina yoyote katika hifadhi hiyo na kwamba hahusiki hata kidogo na uwindaji huo.
Mimi sihusiki katika kashfa ya ujangili na taratibu za mwenge zinajulikana, ninachokataa ni kwamba sijahusika hata kidogo, sijui wameenda kuwindwa mbuga gani na mimi sijaenda, alisema DC Mwasa na kuongeza:
Alisema uamuzi wa kutafuta wanyama ulitolewa na kamati ya maandalizi ambayo wajumbe wake ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (Ded), DC na hata jeshi la polisi na sio kama ni mtu mmoja tu.
Kikao halali kilifanyika cha kamati, kumbukumbu za kikao zipo, idara husika ilipewa jukumu la kutafuta wanyama hao. Sijui walienda pori gani au kama kuna barua iliandikwa, alisema DC Mwasa na kuongeza:
Wakati huo huo Jumuiya ya Hifadhi ya Manyama pori ya
Wami-Mbiki mkoani Morogoro imemshitaki mkuu huyo wa wilaya kwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili kwa njia ya simu, Katibu wa Jumuiya hiyo, Majaliwa Saidi Kayanda, alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya mkuu huyo wa wilaya kushinikiza jumuiya hiyo imtake radhi na kukanusha tuhuma zinazomkabili.
Katibu huyo alisisitiza kuwa jumuiya hiyo haiko tayari kuomba radhi na kukanusha tuhuma hizo huku akimtaka mkuu huyo wa wilaya kuomba radhi kutokana na tuhuma ya kuwatumia raia kuwinda katika msitu wa hifadhi wa Wami-Mbiki kinyume cha sheria.
Kayanda alisema kuwa wamelazimika kumshitaki kwa kumwandikia barua Waziri wa Maliasili na Utalii na nakala kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya za Morogoro na Pwani juu ya suala hilo ili kulitafutia ufumbuzi kutokana na kitendo cha mkuu wa wilaya hiyo kuwatisha viongozi wa jumuiya hiyo. Imeandikwa na Samuel Msuya na Venance George, Morogoro na Salim Said.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi