DASA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 1,031
- 301
Habari zenu members. Sijui hili kama limeshawahi kuongelewa humu. kwa wale madereva mtaniambia hili. Kuna wakati mtu unaweza ukafanya kosa barabarani, inaweza ikawa hata ni kwa bahati mbaya au kutoona signs fulani hasa ukizingatia barabara zetu nyingi bado hazipo kwenye kiwango, au wakati mwingine hata hujui kama umefanya kosa. Sasa Askari wa barabarani anakukamata, mara nyingi kama sio zote ataanza kukwambia umpe leseni yako, sasa kinachoniboa zaidi badala ya kukuandikia fine ukalipe, ataanza kukuzungushazungusha katika harakati za kutengeneza mazingira ya rushwa kwa vile atakuwa ameshika leseni yako. Sasa jamani muda ni mali sana. Askari kama hawa dawa yao ni nini jamani.