Hii tabia ni mke wangu tu au?

Yaaani mbavu sina,unajuwa JF ni more than nothing,haya mambo mie yameshanitokea sana na nikafikiri kuwa ni wa kwangu tu ndio yuko hivyo,nimeshamuacha mara kibao lakini hakomi,mwishowe nimeamua ninyamaze tu maana mpaka saa nyingine namuonea huruma,akishasikia nimewasha gari anajua ntamuacha tu hivyo kidogo inamfanya awahishe kujipodoa,sasa hivi nimeamua awe anaanza yeye kuoga halafu baada ya dakika kama 10 ndio na mimi naingia bafuni ili angalau inapofikia muda wa kutoka tutoe droo.Anyways leo ni me-proove kuwa ni tabia yao kwani inanikumbusha hata mama yangu naye alikuwa anazozana sana na mzee wangu kwa jambo hili.God create dem women we must treat dem tenderly and i do adore my wife so dearly n won't treat her harsh anymore.

Ni kweli mwanzoni huwa inatiaga hasira sana, ila kama ulivyosema we must treat them tenderly and love them .If you love her then you wont see it as problem , you will learn to cope with it.
 
GF wangu ananijua vyema kwani nimeweka kuwa ni utaratibu kama anachelewa kwa sababu za kike kike ananikuta nimeshaenda zangu.

Baada ya kumuacha mara kadhaa, sasa ananijua. Nikimwambia nampitia nikifika huwa ameshajiandaa. Mambo haya ukimzoesha mwanamke ipo siku utapoteza dili la milions sababu ya ufukunyuku wa wife. Mzoeshe kuwa strict kwenye ratiba otherwise atakufundishia ugoigoi watoto wako.

Huu mpango wa mwanamke akili zake slow wala sio mpango. Mfundishe kwa vitendo madhara ya kuwa goigoi
kwenda zako wewe ugoigoi anao huyo wako ,ugoigoi unahusikaje hapa un atokwa maneno tuuuu bangi za mchana bwana ,milioni na laki ipi kubwaaaa.............
 
Sisi tunatumia gari moja namshusha ofisini kwake na jioni nampitia tunarudi.. sasa asubui toka tunaamka mpaka tuaondoka yeye ni kutoa maagizo tu..... sasa kali zaidi wakati ndo tunatoka ndani kuelekea parking..Men, it takes another 5 to 10 mnts mpaka afike. Anaanza upya, - mmenielewa?...usahau.... watoto muhakikishe.....usafi ...

Sasa na wakati wa kumpitia jioni kurudi nyumbani nampigia simu namwambia baada ya nusu saa nitakua hapo.. yaani nikifika it will take another 15 mnts atoke huko ofisini.. ukimuuliza eti nilikua nazima computer.... mwanzoni ilinipa shida sana ila imebidi nizoee tu... kama nawai mahali lazima nianze kuondoka 1hr before.

But ilove her to death.


All human females are the same
 
Hehehehe... mkuu unatisha.. yaani mimi nikijaribu ndani ya nusu saa simu ya mama angu inaingia. Na nitapata semina kila siku si chini ya mwezi mmoja..aisee Du!

hizo ni dalili umelelewa na mama peke yake (mtoto wa mama)
 
Sisi tunatumia gari moja namshusha ofisini kwake na jioni nampitia tunarudi.. sasa asubui toka tunaamka mpaka tuaondoka yeye ni kutoa maagizo tu..... sasa kali zaidi wakati ndo tunatoka ndani kuelekea parking..Men, it takes another 5 to 10 mnts mpaka afike. Anaanza upya, - mmenielewa?...usahau.... watoto muhakikishe.....usafi ...

Sasa na wakati wa kumpitia jioni kurudi nyumbani nampigia simu namwambia baada ya nusu saa nitakua hapo.. yaani nikifika it will take another 15 mnts atoke huko ofisini.. ukimuuliza eti nilikua nazima computer.... mwanzoni ilinipa shida sana ila imebidi nizoee tu... kama nawai mahali lazima nianze kuondoka 1hr before.

But ilove her to death.

....."for better or worse....!" si ulitamka NDIO? Sasa nini tena unaanza kumeng'eneka?
 
Ndivyo walivyo. Mimi wa kwangu nilimpa funzo mara mbili na alishabadilika. Siku ya kwanza chakula kilichelewa kwa kujizungushazungusha na wasaidizi wake, nikawasha gari nikaenda kula nyama choma. Siku nyingine akachelewa kujiandaa kwenda kazini na kutoa maelekezo ambayo mengine yangetolewa jioni, nikawasha gari nikaondoka na nikapita ofisini kwao na kugeuza gari na kwenda ofisini kwangu. Niliporudi jioni nikaja na kilo ya kitimoto ikiwa imesheheni chilli, tomato sause na kachumbali, kicheko juu. Hadi leo ana panctuality ya hali ya juu
ONYO
Tafadhali usiige mbinu hii maana kwa wanawake wengine hii inaweza kuleta mgogoro mkubwa sana

Umetisha kaka Police ha ha ha ha ha ha
 
Hehehehe... mkuu unatisha.. yaani mimi nikijaribu ndani ya nusu saa simu ya mama angu inaingia. Na nitapata semina kila siku si chini ya mwezi mmoja..aisee Du!
uwiiiiiiiiiiiii kama ni hivyo, bora tu kumsubiri, simu mwezi! u have made me to laugh out loud! lol!
 
kwenda zako wewe ugoigoi anao huyo wako ,ugoigoi unahusikaje hapa un atokwa maneno tuuuu bangi za mchana bwana ,milioni na laki ipi kubwaaaa.............
nivea mi-like ya kutosha hiyooooo, tena wanaume wa hivi anaongea hapa tu, mbele ya mkewe thubutu!
 
Last edited by a moderator:
sisi tunatumia gari moja namshusha ofisini kwake na jioni nampitia tunarudi.. Sasa asubui toka tunaamka mpaka tuaondoka yeye ni kutoa maagizo tu..... Sasa kali zaidi wakati ndo tunatoka ndani kuelekea parking..men, it takes another 5 to 10 mnts mpaka afike. Anaanza upya, - mmenielewa?...usahau.... Watoto muhakikishe.....usafi ...

Sasa na wakati wa kumpitia jioni kurudi nyumbani nampigia simu namwambia baada ya nusu saa nitakua hapo.. Yaani nikifika it will take another 15 mnts atoke huko ofisini.. Ukimuuliza eti nilikua nazima computer.... Mwanzoni ilinipa shida sana ila imebidi nizoee tu... Kama nawai mahali lazima nianze kuondoka 1hr before.

But ilove her to death.
hili tatizo lipo hasa kwa wanawake wanaojiona wanakipato KIKUBWA kuliko waume zao.
 
Hapa Bishanga na Mtambuzi sijawaona haya mambo yanawahusu vile,jamani wanaume tuwavumilie wake zetu wana majukumu mengi sana kwnza wanalala wamechoka sana still asubuhi inawasubiri huo muda anaamka we umevuta shuka tena ukute mwanaume mlevi hajui hata watoto wake kama wamekula au lah anarudi usiku wa manane,majukumu yote yanamuelemea mama dah poleni sana,wanunulieni magari waende wenyewe ikitokea amechelewa kama kweli unampenda na kumjali coz vikwapa vya kwenye daladala navyo ni balaa
 
Tabia ya kuchelewa ni tabia ya % kubwa ya wanawake, hapa kwa sababu sarikoki kamuongelea my wife wake baadhi ya wachangiaji wanajaribu kujificha nyuma ya majukumu ya mwanamke aliye na familia watoto nk, hebu kuweni wakweli mseme kinachowachelewesha mabinti ambao hawana familia au ambao hawawajibiki na mambo ya usafi na upishi ktk familia zao! Kwa yeyote ambaye amepitia maisha ya chuo atajua kuwa hata huko tabia ya kuchelewa kwa mabinti ni sugu kwelikweli, au na huko wanakuwa wanatoa maagizo ya usafi, vyakula nk?! Kuna vitabia vya hovyo ambavyo mara nyingine ingefaa mhusika atafute namna ya kuachana navyo badala ya kutafuta visingizio na kuvihalalisha.
 
JF mwanzo mwisho. Mume wangu angekuwa member ningesema leo kaamua kutoa siri za ndani; maana huyu wife wa jamaa ana tabia kama zangu; mume wangu akija nipitia job analalamika eti kwa nini sikuzima computer na amenipigia kuwa anakuja.

Jamani; yani nizime computer wakati sijuhi exactly utachukua muda gani kwenye foleni; kuweni fair kidogo. Wakati mwingine nasema ngoja nifuate masharti basi nazima; afu nakaa saa nzima jamaa hajatokea.

Kuna siku ilikuwa tunatoka jioni; sasa yeye si unajua tena akitia t shirt yake na jeans kamaliza; mimi niangalie hereni ziko wapi, wanja lipstick sijuhi nini; huwezi amini alisusa. Namwambia twende, ooh nimegaili naangalia mechi.
Nkamwambia lete funguo mi najisikia kutoka... mbona alichanganya miguu kuelekea garini.

Hiyo ndo raha ya ndoa; lazima mtu akubore bana kidogo, otherwise kila kitu kikiwa kwenye mstari maisha yatachosha. Lol.

ni kweli tatizo hilo lipo sana kwa wanawake,lakini mara nyingi nimeobserve nikaona mama anaamka ahakikishe kila kitu kipo sawa nyumbani ndipo atoke wakati mwanaume anajiandaa na mara nyingi anaweza kunywa chai wakati mke wake hapati huo muda.atatoka nje honi kwa wingi.saidia majukumu mnapoamka itapunguza kuchelewa.pendeni wake zenu
 
Kuna dada alinihusia kutotumia magari tofauti bila ya sababu; kuna wasubiri lift shaurilo. Lol.


shoste kama ni mfanyakazi uchumi ukikukalia vizuri nawe unanunua hata nissan march ili uwe na amani hata kwenda sokoni kununua vitu vya wiki inakuwa soo
 
Two experiences.
My mother is that way. Baba atasema weee, yeye kimya tu anamalizia mambo yake. Akimharakisha sana huwa anasema ungekuwa na haraka ungewahi jana. Kuna siku moja walikuwa wanaenda sehemu moja baba akamuacha hakuondoka kabisa.
Anajitahidi ila mambo ni mengi.
Mine thanks God he understand, ila na yeye analalamika mara chache. Thank we are not women of make ups and we can take bath in short time, i guess it could be horrible if we could add those.
 
mnunulie kagari kake, kivitz au kasuzuki swift, bei sawa na bure. na hizo kero zote zitaisha
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom