Hii sio nzuri sana!

Escobar

JF-Expert Member
Sep 16, 2011
574
440
Nilikuwa naelekea maeneo ya Tegeta wakati nakaribia stendi ya daladala kukawa kunaingia magari aina ya coaster yamebeba nadhani wafuasi wa magamba kwa vile yalikuwa yamepambwa kwa rangi za njano na kijani.

Cha kusikitisha ni kwamba yalipofika tu eneo hilo la stendi ambalo lina watu wengi sana kwa vile kuna soko pia, vijana na watu waliokuwa maeneo hayo wakalipuka kwa kuzomea kitu ambacho sikukipenda sana maana kila mtu ana haki ya kupenda anachokiamini hata kama hakiaminiki tena!

Tujifunze kauvumilivu jamani hata kama hatupendi
 
unalolisema ni kweli ila kwa siasa za kuona mtu kadhulumiwa ni kazi sana kuwa na uvumilivu wa kisiasa japo inabidi watu wavumiliane.. hata humu jamvini pia
 
Kuna mambo ya kuvumilia mkuu,we know about political tolerance lakini hili la watu kufanywa misukule afu wanashangilia, inabidi wazomewe au wapigwe mawe ili waamke
 
......and the spirit of this age is "brimful" with negations, and drainage to the fast drop is the power of faith....klaat youth!
 
Hata kuzomea ni haki, kwasababu unaonyesha hisia zako. Kifupi huna hoja majitaka
 
Lakini ukweli unabakia pale pale, pamoja na maisha magumu yanayosabishwa na MAGAMBA kwa sababu ambazo zipo wazi wazi kabisa, kumuona mtu ambaye anafurahia hiyo hali lahasha naye anauonja huo ufisadi wa MAGAMBA, mtu wa namna hii hana budi kuzomewa. Sitakubali suala la kuwapiga na mawe!. Ila la kuzomewa ni sahihi kabisa.

Nawapa heko sana hao watu wa Tegeta.
 
Suala ni kuzomewa tu ama kuna kingine,mbona hilo ni jambo la kawaida sana na wasipokuwepo watu wa kuzomea patakuwa na matatizo.Kuzomewa ni changamoto tu wala zisikuumize kichwa.
 
Jiulize katika maisha yako... watu wanaozomea wanakuwa na akili za namna gani?
 
Nami nawaunga mkono kwa vitendo, yaani wanafurahia tukiibiwa!!!!! Nape oooooooh! iiiiih!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom