Hii serikali inamuheshimu nani?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,754
Kila dai linalowekwa mbele ya serikali linaburuzwa na kupigwa danadana hadi wahusika wanatishika na kuamua pangine kuachana na madai yao. Machache ni kama haya:
1. Madai ya wanafunzi wa vyuo.
2. walimu (hasa wa sekondari na msingi)
3. wafanyakazi (kama reli)
4. madaktari.
ukiangalia hivyo ni vitengo nyeti sana. Madai ya wadau hawa serikali hujibu kwa nyodo na vitisho ikiwa ni pamoja na kusimamishwa, kufukuzwa, hata kufungwa. Kwa nini serikali yetu hupenda tufike huko? Kama serikali haiheshimu maslahi ya watumishi wake inaheshimu nini? Wakati mwingine unaweza kuona kuwa gharama za kudhibiti hii mitafaruku ni kubwa kuliko gharama za kutekeleza madai. Matokeo yake tunapata majibu kama mtakula nyasi, kula uliwe, wivu wa kike, pigeni mbizi n.k. Hii serikali inamheshimu nani?
 
Serikali corrupt haiwezi kuwaheshimu wananchi wake, serikali ya mabavu siku zote haidumu ipo siku hawa wanaojifanya wamepinda kama Pinda watapindwa tu
 
Kila dai linalowekwa mbele ya serikali linaburuzwa na kupigwa danadana hadi wahusika wanatishika na kuamua pangine kuachana na madai yao. Machache ni kama haya:
1. Madai ya wanafunzi wa vyuo.
2. walimu (hasa wa sekondari na msingi)
3. wafanyakazi (kama reli)
4. madaktari.
ukiangalia hivyo ni vitengo nyeti sana. Madai ya wadau hawa serikali hujibu kwa nyodo na vitisho ikiwa ni pamoja na kusimamishwa, kufukuzwa, hata kufungwa. Kwa nini serikali yetu hupenda tufike huko? Kama serikali haiheshimu maslahi ya watumishi wake inaheshimu nini? Wakati mwingine unaweza kuona kuwa gharama za kudhibiti hii mitafaruku ni kubwa kuliko gharama za kutekeleza madai. Matokeo yake tunapata majibu kama mtakula nyasi, kula uliwe, wivu wa kike, pigeni mbizi n.k. Hii serikali inamheshimu nani?

Mkuu serikali isiyo sikivu na iliyojaa rushwa huheshimu MAFISADI na wala rushwa wakubwa basi. Hawa ndio wadau muhimu wa serikali mbovu popote duniani.
 
for real guys, something unexpected should be done unto this govt.
 
Back
Top Bottom